Shule ya sekondari Uraki Halmashauri ya Meru mkoani Arusha yenye wanafunzi chini ya 400 ina walimu kama 50

Shule ya sekondari Uraki Halmashauri ya Meru mkoani Arusha yenye wanafunzi chini ya 400 ina walimu kama 50

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Shule tajwa hapo juu ina wanafunzi chini ya 400 lakini ina walimu wanaofikia 50 kiasi wengine wanakosa vipindi vya kufundisha. Mkurugenzi yupo anafahamu yote haya walimu wako busy na biashara zao maeneo ya Arusha mjini, ktk miji midogo ya Usa-River na Tengeru. Wakati hali ikiwa hivi ktkt shule hii kuna shule za msingi zina walimu 6 pamoja na mwl. mkuu ndani ya Halmashauri hii na ktkt mkoa wa Arusha kwa ujumla.

Ukitembea Tanzania kwa mfano mkoa wa Ruvuma nilifika wilaya ya Tunduru unakuta shule ina walimu 4 pamoja na mwl. mkuu. Je serikali inajua haya yote? Je inajua walimu wamekusanyana sule za mjini na zilizo pembezoni mwa miji mikubwa km Arusha? Wakurugenzi wahusika wanafahamu haya yote ila wanakula rushwa. .

Serikali ifuatilie kwa mfano iondoe walimu pale Uraki iwasambaze kwenye shule zenye upungufu wa walimu wapelekwe hata mikoa mingine kwenye mahitaji makubwa wanakula mshahara bure na kutumia muda wa mwajiri kufanya shughuli zao zingine. Mkurugenzi huyu wa Halmashauri ya wilaya ya Meru amulikwe siyo bure.
 
Lakini serikali imeanza kufanya msawazo wa walimu, so nadhani msawazo huo utawafikia.
 
Ahsante mtoa hoja na nimependa mfano wako halisi, mkoa wa Ruvuma hali huku ni shida hasa hizi shule za vijijini, afadhali kidogo kwenye vijiji/miji kama Peramiho, Hanga, Namabengo, Likuyu Fusi, ila ukija lingusenguse, Mputa (yalikokua makambi ya wakimbizi),wilaya karibu yote ya Tunduru ni shida
 
Back
Top Bottom