Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili baada ya kuingia makubaliano na Kenya

Kama wewe. Wee ndio Zuzu,wao wanakimbia ukabila wao.
Mimi sio zuzu maana angalau Kiswahili nakimudu vilivyo hata nikiamshwa usiku wa manane siwezi kukosea sarufi!

Wengi wenu hamjui lugha hasa ya maandishi, japokuwa matamshi nayo ni mabovu lakini angalau mnayaficha kwa kuongea haraka haraka!

Ohh tunataka Kiswahili, ohh sijui mabeberu! Kiswahili chenyewe hamkiwezi!! Mnababaisha tu!
 
Kweli mkuu. Watu wa aina hiyo wapo sana TZ
 
True mkuu. Mi Mtz haya mambo yananiuma sana.
 
Mimi mkuu nimesema hapa watu wanatetea. Tx kiswahili kwenye makaratasi ni kitamu sana. Sasa mtafute Mtz tena msomi tu mwambie

Mtanzania unae mkusudia hapa ni yule aliye soma fani ya Kiswahili pweke na mkenya unae mzungumzia ni mkenya alie soma Kiswahili kama fani au ?
 
Wewe ndio unaamini hivyo. Wao wanefanya research kabla ya kuiteua kenya. Wakaona Kenya ndio wapo vzr kuliko nchi yoyote. Wew umebakiwa na kusema kiswahili chetu basi wakatu huna unalolijua

Wakenya wanaoa jua Kiswahili fasaha ni wale ambao wamesomea Kiswahili kama fani pweke na si jambo la ajabu katika ulimwengu wa kielimu.

Ila kwa ujumla watanzania ndio wanaongea Kiswahili fasaha kuliko wengine.
 
Ukweli ni kwamba tunaongea Kiswahili 'kizuri' kuliko wakenya, lakini hiyo haimaanishi kuwa tunaongea Kiswahili fasaha!
 
Mkuu sisi ni wa hivyo sana na hii elimu yetu ya kukibagua kiingereza hivi huko nje utakako kwenda kutafuta hiyo kazi ya kufundisha kiswahili huyo mwenyeji wako nae anajua kiswahili?
 
Ukweli ni kwamba tunaongea Kiswahili 'kizuri' kuliko wakenya, lakini hiyo haimaanishi kuwa tunaongea Kiswahili fasaha!
Marejeo ya Kiswahili fasaha ni wapi ? Vipi kuhusu uzuri wa Kiswahili cha Watanzania una mili wapi ? Katika sarufi au ?

Ndio lazima uonekane ni muongo pindi unapolinganisha Kiswahili cha wakenya kwa ujumla na Kiswahili cha watanzania ?
 
Hiyo ni lugha ya biashara kama ilivyo bata batani kanga moko kiuno ndembe ndembe
 
kun jamaa hapa kasema kiswahili hakiwahusu wabara..kuna wengine wakaanza kutema mapovu...nashuku hao jamaa ni wa kutoka tanzania bara kwel...si wajikubali km wabara wa kenya...wanajikubali km kiswahili hakiwahusu...
KISWAHILI ni lugha ya taifa wewe mama
 
Marejeo ya Kiswahili fasaha ni wapi ? Vipi kuhusu uzuri wa Kiswahili cha Watanzania una mili wapi ? Katika sarufi au ?

Ndio lazima uonekane ni muongo pindi unapolinganisha Kiswahili cha wakenya kwa ujumla na Kiswahili cha watanzania ?
Ati marejeo ya Kiswahili fasaha ni wapi! Hilo ni swali au uchochezi?

Lugha fasaha ni lugha inayofuata utaratibu wa kisarufi. Tofauti yetu na wakenya ni kuwa Kiswahili cha Kenya ni kibovu zaidi!

Sikumaanisha kuwa watanzania 'wote' wanazungumza na kuandika Kiswahili kibovu. Baadhi kama sio wengi hawafahamu Kiswahili sanifu!

Matumizi ya "H" na "irabu", "dh" Vs "Z", "S" Vs "th", "R" Vs "L" ni baadhi ya magonjwa sugu ya Kiswahili cha watanzania. Maneno kama alafu- Halafu, hanakuja-anakuja, zamana-dhamana, urisi-urithi, samani-thamani, kasilika-kasirika, ugari-ugali. nk. Hiyo ni mifano michache ya uharibifu wa Kiswahili na sababu yake ni illiteracy tu wala hakuna lingine. (Umbumbumbu wa lugha).
 
GODZILLA na french nimewafuatilia nimegundua hoja mnazozitoa ni kwa ushabiki na mihemko hamna mnalolijua kuhusu kiswahili
Unafahamu maana ya neno "mihemko"? Umeshaangalia angalau kwenye kamusi kujua linamaanisha nini? Au ulimsikia 'mama dulla' anapayuka na wewe ukalidaka juu juu ukaja nalo Jamiiforums kulitungia sentensi ya majaribio?
 
Naam angalau umeanza kuandika kiswahiki kizuri sasa
Kumbe somo linaingia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…