Ati marejeo ya Kiswahili fasaha ni wapi! Hilo ni swali au uchochezi?
Lugha fasaha ni lugha inayofuata utaratibu wa kisarufi. Tofauti yetu na wakenya ni kuwa Kiswahili cha Kenya ni kibovu zaidi!
Sikumaanisha kuwa watanzania 'wote' wanazungumza na kuandika Kiswahili kibovu. Baadhi kama sio wengi hawafahamu Kiswahili sanifu!
Matumizi ya "H" na "irabu", "dh" Vs "Z", "S" Vs "th", "R" Vs "L" ni baadhi ya magonjwa sugu ya Kiswahili cha watanzania. Maneno kama alafu- Halafu, hanakuja-anakuja, zamana-dhamana, urisi-urithi, samani-thamani, kasilika-kasirika, ugari-ugali. nk. Hiyo ni mifano michache ya uharibifu wa Kiswahili na sababu yake ni illiteracy tu wala hakuna lingine. (Umbumbumbu wa lugha).