Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili baada ya kuingia makubaliano na Kenya

Wana JF naomba tusaidiane hapa. Kila unaezungumza nae kuhusu juu ya hili suala watu wanatoa sababu mbalimbali na nyingi ni za kisiasa.
Natamani kupata sababu za Kitaalam kwanini nchi ya Afrika ya Kusini imeingia mkataba na nchi ya Kenya katika kuchukua walimu wa Kiswahili badala ya Tanzania?

Licha ya uhusiano wetu mzuri tulionao kati ya Afrika ya Kusini lakini katika hili tumebaki midomo wazi kama Taifa.
Je, sababu inaweza kuwa ni ipi?

Kuna wanaosema pamoja na kuwa Afrika ya Kusini wanahitaji walimu wa Kiswahili, lakini walimu wanatakiwa kuwa competent kwenye lugha ya Kiingereza. Na kwasababu hiyo walimu wetu wa Tanzania wana tatizo la Kiingereza ndio maana wakaachwa.

Wengine wanasema, serikali yetu imeshindwa tu kucheza na fursa hii kwa ajili ya vijana wake. Hasa Mabalozi wetu na Wizara ya mambo ya nje.

Je, mtazamo wako ni upi? (Wa kitaalaam)
 
Kwa maoni yangu kama Mkenya, kuna sababu kadhaa ninazohisi zimechangia, baadhi zipo kisiasa.
Kwanza kabisa serikali yenu huwa imezubaa sana kwenye masuala ya kuinadi nchi, kuwa na uhusiano mzuri baina ya mataifa haitoshi, lazima mjifunze kukaa mkao wa kimaslahi zaidi na kujituma kwenye kutafuta fursa, mnajifungia ndani eti kubana matumizi.
Mambo ya uhusiano na kuitana ndugu ni sawa ila unatumia vipi huo uhusiano, unajinadi vipi, mtoko wako vipi.
Pili, Watanzania hampo vizuri kwenye utaalam wa uandishi wa lugha ya kiswahili, kuzungumza kiswahili mtaani ni moja, ila uandishi wake kitaalam ni jambo lingine, jaribu ufanye utafiti wa mtihani wa kiswahili kidato cha nne Kenya na Tanzania, ulinganishe nina uhakika utapata jibu.
Tatu, Watanzania wengi mumeganda kwenye lugha moja ya kiswahili, hamtaki na hampendi kujiongeza, Kingereza kimewapiga wengi chenga, na badala ya kupambana kukijua huwa mnajiliwaza kwamba ni lugha ya mkoloni hivyo nyie sio watumwa...yaani sizitaki mbichi.
Ufahamu wa lugha ya kingereza hufungua fursa nyingi sana kimataifa, wewe hapo unataka ukamfunze mtu kiswahili ilhali huna jinsi ya kuwasiliana naye kwa lugha anayoifahamu kama kingereza, utatemwa tu na kukataliwa.
Mkenya yupo vizuri lugha kadhaa maana ni sera yetu kuwa wajanja wa lugha nyingi, hii imetusaidia sana kwenye kuinadi nchi. Niliona sehemu hata Kichina kitaanza kufunzwa kwenye mtaala wetu mpya.

Mwisho, ifahamike japo huwa hampendi huu ukweli mchungu kwamba Wakenya huwa tunajituma kuzidi Watanzania, hili lipo ndani ya damu yetu na tunazidi kuongeza pengo baina yetu.
 
Tanzania hawazungumzi Kiswahili fasaha, wengi wanazungumza Kiswahili cha mtaani ambacho si cha kufunzia watu. Kingine, hatuna walimu wa kweli hapa Tanzania kutokana na kuwa na elimu duni.
 
Kwa maoni yangu kama Mkenya, kuna sababu kadhaa ninazohisi zimechangia, baadhi zipo kisiasa.
Kwanza kabisa serikali yenu huwa imezubaa sana kwenye masuala ya kuinadi nchi, kuwa na uhusiano mzuri baina ya mataifa haitoshi, lazima mjifunze kukaa mkao wa kimaslahi zaidi na kujituma kwenye kutafuta fursa, mnajifungia ndani eti kubana matumizi.
Mambo ya uhusiano na kuitana ndugu ni sawa ila unatumia vipi huo uhusiano, unajinadi vipi, mtoko wako vipi.
Pili, Watanzania hampo vizuri kwenye utaalam wa uandishi wa lugha ya kiswahili, kuzungumza kiswahili mtaani ni moja, ila uandishi wake kitaalam ni jambo lingine, jaribu ufanye utafiti wa mtihani wa kiswahili kidato cha nne Kenya na Tanzania, ulinganishe nina uhakika utapata jibu.
Tatu, Watanzania wengi mumeganda kwenye lugha moja ya kiswahili, hamtaki na hampendi kujiongeza, Kingereza kimewapiga wengi chenga, na badala ya kupambana kukijua huwa mnajiliwaza kwamba ni lugha ya mkoloni hivyo nyie sio watumwa...yaani sizitaki mbichi.
Ufahamu wa lugha ya kingereza hufungua fursa nyingi sana kimataifa, wewe hapo unataka ukamfunze mtu kiswahili ilhali huna jinsi ya kuwasiliana naye kwa lugha anayoifahamu kama kingereza, utatemwa tu na kukataliwa.
Mkenya yupo vizuri lugha kadhaa maana ni sera yetu kuwa wajanja wa lugha nyingi, hii imetusaidia sana kwenye kuinadi nchi. Niliona sehemu hata Kichina kitaanza kufunzwa kwenye mtaala wetu mpya.

Mwisho, ifahamike japo huwa hampendi huu ukweli mchungu kwamba Wakenya huwa tunajituma kuzidi Watanzania, hili lipo ndani ya damu yetu na tunazidi kuongeza pengo baina yetu.
Asante sana kwa mchango wako huu. Umepanua zaidi ufahamu wa hili jambo
 
Kwa kumsikiza Ben Mwanantala katika Reli TV akizungumzia kuhusu SGR ya Tanzania, utajua pia hamjabobea katika Kiswahili ambayo ni lugha yenu ya Taifa....yeye hupenda Sana kusema 'reri' badala ya reli..na najua si yeye pekee
 
Kama ilivyo kawaida yetu kuchangamkia fursa, Rwanda wamebadilisha katiba na kukifanya lugha rasmi, hivyo kitafunzwa shuleni kwenye mitaala yao, tutiririke huko, halafu poa sana maana Rwanda wao tulishaingia makubaliano nao hakuna cha paspoti wala nini, ilmradi unacho kitambulisho chako.
----------------------

Rwanda lawmakers approve swahili as the official Language of the country, dropping french completely and sidelining english People said: "This is good,really good but such a move leavez the Belgian (the former
 
Funza = Maggot
Kufundisha = teaching.
Soma kiswahili kwanza ndipo upate nafasi ya kufundisha.

Nashangaa sana kuna watu wame-like hii comment yako, ungebahatika kwenda shule ungejua kuna kitu kinaitwa visawe (synonym)
Nomino
funza (wingi funza)

  1. mdudu anayeota kwenye kidole cha binadamu kwa uchafu au kutovaa viatu (1)
  2. onyesha mtu jinsi ya kufanya kitu (2)
 
Funza = Maggot
Kufundisha = teaching.
Soma kiswahili kwanza ndipo upate nafasi ya kufundisha.

funz.a1 kt [ele] educate, teach esp good manners. (tde) funzia; (tdk) funzika; (tdn) funzana; (tds) funzisha; (tdw) funzwa.

funza2 nm ma- [a-/wa-] 1 jigger, sand fleas. 2 larva, maggot, grub.

--
Source: TUKI KAMUSI YA KISWAHILI-KIINGEREZA - INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
cc:
MK254. . .
 
Rwanda na Kenya una njozi... the two don't get along
Unafahamu na tunafamu hili

Rwanda na Tz wana ushirikiano wa kiasi kikubwa kuliko Rwanda na Kenya
So dude don't lie to yourself

By the way hili zoezi la kufundisha Kiswahili Rwanda lilianza kitambo
Kiswahili.chenu kibovu kawadanganyeni WaSouth ( what I know hata hawa watafundishwa na Tz coz wanajua asili ya Kiswahili ni Tz. Kumbuka waSouth Africa waliishi Tz na bado wapo. South Africa na Tz ni dugu moya.. upo hapo??!

Rwanda watafundishwa Kiswahili na WaTz amini hili
Kagame sio wa kupelekeshwa hivyo na WaKenya
 
Nashangaa sana kuna watu wame-like hii comment yako, ungebahatika kwenda shule ungejua kuna kitu kinaitwa visawe (synonym)
funza1

KITENZI ELEKEZI~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

  • 1
    fundisha, hasa mambo ya adabu na tabia.

funza2

NOMINOplural funza

  • 1
    mdudu mdogo kama kiroboto ambaye huingia katika miguu ya watu na wanyama.
Hakuna neno funza lenye kitenzi kwenye kiswahili.
Wewe hujui kiswahili.
Fundisha, kujifundisha, kufundisha nk.
Neno KUFUNZA huwa linatumiwa na wakenya walio wavivu wa kukielewa kiswahili.
 
mi huaganashangaa na watanzania...mnajisifia kiswahili...kumbe kuna na maneno mengine hta hamyajui na wala hamjawai kuyaskia...mwenzako kuna siku hapa jf ilkua hata hajui maana ya kumakinika, hv leo na wewe unaleta ubishi wa kijinga...yani hujui maana ya kufunza
 
funza sio kitenzi ...kitenzi ni fundisha na ukiendelea kunyambulisha unapata vitenzi kama fundishwa,fundishana,fundishia hauwezi kunyambulisha kitenzi funza
 
Hata British English na USA English zipo tofauti muhimu kufahamiana tu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom