GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,909
- 10,542
Ni Roza! Kimeandikwa na Mtanganyika haswaaa!Roza mistika.. Ni roza au Rosa? Kitabu kitamu sana hiki.Nilikisoma nilipokuwa kidato cha kwanza Kimeandikwa na mtanganyika?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni Roza! Kimeandikwa na Mtanganyika haswaaa!Roza mistika.. Ni roza au Rosa? Kitabu kitamu sana hiki.Nilikisoma nilipokuwa kidato cha kwanza Kimeandikwa na mtanganyika?
Sawa Nyang'au! Uwe na usiku mwema!anyway...don't take it personal...we are here also to have fun..not only arguing
Wana JF naomba tusaidiane hapa. Kila unaezungumza nae kuhusu juu ya hili suala watu wanatoa sababu mbalimbali na nyingi ni za kisiasa.
Natamani kupata sababu za Kitaalam kwanini nchi ya Afrika ya Kusini imeingia mkataba na nchi ya Kenya katika kuchukua walimu wa Kiswahili badala ya Tanzania?
Licha ya uhusiano wetu mzuri tulionao kati ya Afrika ya Kusini lakini katika hili tumebaki midomo wazi kama Taifa.
Je, sababu inaweza kuwa ni ipi?
Kuna wanaosema pamoja na kuwa Afrika ya Kusini wanahitaji walimu wa Kiswahili, lakini walimu wanatakiwa kuwa competent kwenye lugha ya Kiingereza. Na kwasababu hiyo walimu wetu wa Tanzania wana tatizo la Kiingereza ndio maana wakaachwa.
Wengine wanasema, serikali yetu imeshindwa tu kucheza na fursa hii kwa ajili ya vijana wake. Hasa Mabalozi wetu na Wizara ya mambo ya nje.
Je, mtazamo wako ni upi? (Wa kitaalaam)
Asante sana kwa mchango wako huu. Umepanua zaidi ufahamu wa hili jamboKwa maoni yangu kama Mkenya, kuna sababu kadhaa ninazohisi zimechangia, baadhi zipo kisiasa.
Kwanza kabisa serikali yenu huwa imezubaa sana kwenye masuala ya kuinadi nchi, kuwa na uhusiano mzuri baina ya mataifa haitoshi, lazima mjifunze kukaa mkao wa kimaslahi zaidi na kujituma kwenye kutafuta fursa, mnajifungia ndani eti kubana matumizi.
Mambo ya uhusiano na kuitana ndugu ni sawa ila unatumia vipi huo uhusiano, unajinadi vipi, mtoko wako vipi.
Pili, Watanzania hampo vizuri kwenye utaalam wa uandishi wa lugha ya kiswahili, kuzungumza kiswahili mtaani ni moja, ila uandishi wake kitaalam ni jambo lingine, jaribu ufanye utafiti wa mtihani wa kiswahili kidato cha nne Kenya na Tanzania, ulinganishe nina uhakika utapata jibu.
Tatu, Watanzania wengi mumeganda kwenye lugha moja ya kiswahili, hamtaki na hampendi kujiongeza, Kingereza kimewapiga wengi chenga, na badala ya kupambana kukijua huwa mnajiliwaza kwamba ni lugha ya mkoloni hivyo nyie sio watumwa...yaani sizitaki mbichi.
Ufahamu wa lugha ya kingereza hufungua fursa nyingi sana kimataifa, wewe hapo unataka ukamfunze mtu kiswahili ilhali huna jinsi ya kuwasiliana naye kwa lugha anayoifahamu kama kingereza, utatemwa tu na kukataliwa.
Mkenya yupo vizuri lugha kadhaa maana ni sera yetu kuwa wajanja wa lugha nyingi, hii imetusaidia sana kwenye kuinadi nchi. Niliona sehemu hata Kichina kitaanza kufunzwa kwenye mtaala wetu mpya.
Mwisho, ifahamike japo huwa hampendi huu ukweli mchungu kwamba Wakenya huwa tunajituma kuzidi Watanzania, hili lipo ndani ya damu yetu na tunazidi kuongeza pengo baina yetu.
Funza = Maggot
Kufundisha = teaching.
Soma kiswahili kwanza ndipo upate nafasi ya kufundisha.
Kuna makosa ya kimuundo na makosa ya kisarufi. Wewe unazungumizia yapi!?Usipokuwa makini unaweza ukawa na wewe umekosea mkuu!
Funza = Maggot
Kufundisha = teaching.
Soma kiswahili kwanza ndipo upate nafasi ya kufundisha.
Funza = Maggot
Kufundisha = teaching.
Soma kiswahili kwanza ndipo upate nafasi ya kufundisha.
Hakuna neno funza lenye kitenzi kwenye kiswahili.Nashangaa sana kuna watu wame-like hii comment yako, ungebahatika kwenda shule ungejua kuna kitu kinaitwa visawe (synonym)
funza1
KITENZI ELEKEZI~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa
- 1
fundisha, hasa mambo ya adabu na tabia.
funza2
NOMINOplural funza
- 1
mdudu mdogo kama kiroboto ambaye huingia katika miguu ya watu na wanyama.