Shule za Dar zifungwe kwa muda mpaka mvua zitakapokoma au kupungua

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Hali ya mvua jijini Dar si shwari kabisa, hii ni siku ya 5 sasa mvua zinanyesha nonstop. Kwa miundombinu ya hili jiji ilivyo mibovu ingekuwa busara shule zifungwe kwa muda, hasa shule za msingi, japo yale madarasa ya chini la kwanza mpaka la nne.

Hivi ninavyoandika hapa mvua imenyesha usiku kucha, na sipati picha huko mitaani hali ikoje. Watu wazima tu leo kufika kazini ni kwa mshikemshike sana, sembuse hawa watoto wadogo?

Na hii yote inasababishwa na serikali kutokuwa serious na miundombinu ya ndani ya miji, 90% ya jiji la Dar halina barabara za mitaani. Ukitoka tu kwenye barabara kuu zenye lami ukaingia mtaani basi unakutana na vijibarabara vya tope ambavyo vingi vimechongwa na wananchi wenyewe, havina hata standard ya kuitwa barabara za vumbi.





 
Uko sahihi hali wanayopitia wanafunzi kwa Sasa ni mbaya maana anafika shuleni ameloa na anarudi nyumbani ameloa madaftari yameloa nguo zimeloa hazikauki kesho anazivaa anaenda shule analoa tena
Hapa mkenda hawezi fanya lolote as anatembea kwenye gari Moja Kali sana na wake wote wako boarding schools but few months to come Hawa wote watapimwa sawa
 
Naunga mkono hoja,,nimewazuia watoto wangu kwenda shule hadi hali ikae sawa!!
 
Mzazi chukua hatua mapema ukiona hali hairidhishi mwambie mtoto alale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…