T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
- Thread starter
- #21
Kuna ndugu yangu ni afisa wa halmashauri moja ya vijijini alienda kwenye kikao cha wazazi shuleni. Ugomvi ulikuwa ni wazazi kugoma kutoa mchango wa mahindi na maharage ili watoto wao wale shuleni. Wananchi walipangana na kupeana hoja, na kuwapanga wale wazee wanaojua kuongea sana. Walipinga kuchangia chakula eti hawana uwezo na walimu watauza mahindi.Sio kila mtanzania ana uwezo wa kumpeleka mwanae shule za gharama ila kwa wale wenye uwezo huo wafanye hivyo. Shule za kata zina msaada mkubwa sana kwa wazazi walio na kipato kidogo na ndio zilizobeba idadi kubwa ya wanafunzi.
Jambo la msingi ni sisi wazazi tushirikiane na walimu kuwasimamia watoto wetu wasome kwa bidii. Jitihada zikifanyika kwa pamoja vijana watafanya vizuri katika mitihani yao.
Mwalimu mkuu haamini wananchi wanakosaje vibaba vya mahindi. Wananchi wakamwambia mbona walimu wake wana madeni kwenye maduka ya mangi, kama wana uwezo mbona wanakopa. Mjadala ukaisha wanafunzi watashinda njaa sababu elimu ni bure. Hiyo shule ilikuwa inafelisha, umbali wa kwenda shule wengine ni mkubwa, kijiji hakina umeme. Mipango ikaja ni walimu kufundisha bure muda wa ziada ila wanafunzi watakuwa na njaa hivyo wale shuleni. Wazazi wakagoma kuchanga mahindi elimu ni bure (hapo waliishagoma kuchangia hela ya masomo ya ziada jioni).
Sasa unategemea kufaulu hapo?
Ukiwa mzazi unaishi sehemu ina ugumu usifanye mambo mengi, wewe pambana wanao wasome sehemu zina unafuu. Unategemea miujiza shule kama Mburahati au Mbagala?
Hiyo Mbagala kwanza pembeni kuna danguro, wanafunzi zaidi ya 200 wanagonga sifuri kwenye NECTA, walimu hawatoshi watoto kibao.
Nazungumzia kwa anayeweza. Ambaye hawezi sawa ila akae akijua.