Shule zote kufungwa Novemba 13 kutokana na tahadhari ya mvua za El Nino

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) imekuwa ikifuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Katika taarifa yake ya tarehe 18 Agosti 2026, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilitoa mwelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba – Desemba, 2026 na kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa upepo wa mvua kubwa za El Nino zinazoweza kusababisha mafuriko na athari nyingine katika baadhi ya maeneo.

Kufuatia tahadhari hiyo, tarehe 25.9.2026 WyEST ilitoa taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko ya tarehe za Upimaji na Mitihani ya Kitaifa ikiwa ni hatua muhimu ya kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na athari za mvua hizo.

Kwa kuwa madhara ya mvua za El Nino yanaweza kuathiri shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasio katika madarasa ya Upimaji na Mitihani ya Kitaifa, ni muhimu kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya usalama na ustawi wa wanafunzi wote, walimu na watumishi wengine katika shule.

Aidha, Waraka wa Elimu Namba 06 wa Mwaka 2025 kuhusu Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa Mwaka wa Masomo 2026 na Waraka wa Elimu Namba 01 wa Mwaka 2026 kuhusu Kalenda ya Mihula kwa Kidato cha Tano na Sita kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 zinaelekeza kufunga Shule tarehe 04/12/2026 kwa muhula wa masomo unaoishia Desemba 2026.

Hivyo, kwa kuzingatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Nino na athari zake, Kamishna wa Elimu anaelekeza kwamba, Shule zote zifungwe tarehe 13 Novemba 2026 kwa muhula unaoishia Desemba, 2026 badala ya tarehe 04/12/2026 kama ilivyokuwa imeelekezwa awali katika nyaraka za Elimu zilizo bainishwa katika Aya ya 5 ya Waraka huu.

Hatua hii inalenga kulinda usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine katika shule.

Waraka huu utaanza kutumika rasmi tarehe 1 Oktoba, 2026.

Soma Pia: TMA: October kuna mvua za El Nino zinakuja

Ninakushukuru kwa ushirikiano.

Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa
KAMISHNA WA ELIMU

#KaziNaUtu#TunasongaMbele#TabasamuLaUtu.webp
#KaziNaUtu#TunasongaMbele#TabasamuLaUtu-1.webp
 
Ni vizuri maana kuna sehemu bila kuvuka mito haufiki shuleni.

Ila kama mvua zilitarajiwa kuanza September mpaka sasa October karibu dunia nzima bado hazija ripotiwa yaweza kuwa zitakuwa kinyume na inavyo tahadharishwa haswa huku Tanzania
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) imekuwa ikifuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Katika taarifa yake ya tarehe 18 Agosti 2026, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilitoa mwelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba – Desemba, 2026 na kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa upepo wa mvua kubwa za El Nino zinazoweza kusababisha mafuriko na athari nyingine katika baadhi ya maeneo.

Kufuatia tahadhari hiyo, tarehe 25.9.2026 WyEST ilitoa taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko ya tarehe za Upimaji na Mitihani ya Kitaifa ikiwa ni hatua muhimu ya kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na athari za mvua hizo.

Kwa kuwa madhara ya mvua za El Nino yanaweza kuathiri shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasio katika madarasa ya Upimaji na Mitihani ya Kitaifa, ni muhimu kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya usalama na ustawi wa wanafunzi wote, walimu na watumishi wengine katika shule.

Aidha, Waraka wa Elimu Namba 06 wa Mwaka 2025 kuhusu Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa Mwaka wa Masomo 2026 na Waraka wa Elimu Namba 01 wa Mwaka 2026 kuhusu Kalenda ya Mihula kwa Kidato cha Tano na Sita kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 zinaelekeza kufunga Shule tarehe 04/12/2026 kwa muhula wa masomo unaoishia Desemba 2026.

Hivyo, kwa kuzingatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Nino na athari zake, Kamishna wa Elimu anaelekeza kwamba, Shule zote zifungwe tarehe 13 Novemba 2026 kwa muhula unaoishia Desemba, 2026 badala ya tarehe 04/12/2026 kama ilivyokuwa imeelekezwa awali katika nyaraka za Elimu zilizo bainishwa katika Aya ya 5 ya Waraka huu.

Hatua hii inalenga kulinda usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine katika shule.

Waraka huu utaanza kutumika rasmi tarehe 1 Oktoba, 2026.

Soma Pia: TMA: October kuna mvua za El Nino zinakuja

Ninakushukuru kwa ushirikiano.

Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa
KAMISHNA WA ELIMU

View attachment 3682662View attachment 3682661
Mbona ni maeneo machache yatakayofikiwa na hizo mvua za el nino?

Na kama ni kujali usalama wa madenti, vipi kuhusu vyuo vya kati (madenti ni kama wa sekondari tu) na vyuo vya elimu ya juu?
 
Hizi mvua mbona zinapewa promo ya kipekee sana! Isije ikawa ni kichaka cha kupigia hela za wananchi mazombi! Naona hela heka zimekuwa nyingi kupitiliza.

Ni tahadhari tu kweli?
 
Back
Top Bottom