Shunie kuanzia leo jiite rasmi Mrs. GENTAMYCINE kwani umeuteka moyo wangu kunakotukuka

Shunie kuanzia leo jiite rasmi Mrs. GENTAMYCINE kwani umeuteka moyo wangu kunakotukuka

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Uwe labda umeshawahi sijui Kutongozwa humu au huko barabarani au hata kuwa na Mahusiano na Watu wenye Idadi kama Mabehewa yote ya Treni ya Bara au hata kama una mapungufu yako yoyote au hata kama Wewe ni mchawi / kigagula ila leo nikuambie tu rasmi kuwa katika Members wa JamiiForums ambao natamani sana siku moja Mimi na Yeye tusimame Madhabahuni tukiwa tunafunga Ndoa yetu ni Wewe uitwae Shunie.

Nina sifa moja kubwa kama pia si zawadi niliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kujua sana kuchagua vitu vizuri, sahihi na makini na kamwe sijawahi kukosea hivyo nakuomba popote pale ulipo kuanzia sasa tena ikibidi ringa na tamba kabisa huku ukijiita Mrs. GENTAMYCINE kwani Moyo wangu Kwako umeshakufa Kitambo hivyo Kazi Kwako Wewe tu Kuuzika.

Bahati nzuri sijawahi Kumtongoza Mwanamke yoyote humu Jamvini tokea nijiunge rasmi hivyo asikutishe ' Kinyankera ' yoyote kuwa sijui nimeshawahi kumtokea au kumbandua / kumbaioloji ila Wewe ndiyo wa Kwanza hivyo jiamini huku ukitembea kifua mbele kuwa Wewe sasa ndiyo Mrs. Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer.

I love you so much Shunie mwaaaaaaaahhhhhhhhhh.....pokea rasmi hilo busu langu la thamani kubwa lililojaa ' mahaba ' ya Kimataifa.

Penzi ni Kikohozi na kulificha siwezi.

Nawasilisha.
 
Shunie Hongera kwa kuuteka moyo wa kiumbe cha Mwenyez Mungu.

Huyo Mwanamke nampenda sijapata kuona na haijawahi kutokea. Ila hata yeye pia huko alipo au salamu hizi zikimfikia itabidi afurahi kwani amepata dhahabu halisi kabisa hivyo Kazi Kwake tu kuitunza na kuhakikisha kwamba haitamaniwi na wengine ambao usiku na mchana walikuwa wanaota Kupendwa na GENTAMYCINE ila bahati mbaya sana moyo wangu haukuwaona kama ambavyo kila uchao ulikuwa ukimwona tu Shunie.
 
Kumbe kunawanaoota eenhee ?😱 si mchezo
 
Back
Top Bottom