NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Ushahidi unaendelea kukusanywa ili mhusika atupwe nje ya ulingo mwakani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani unatuambia sisi tumezingua? Sasa ngoja tukutafute utuambie vizuri uso kwa uso.wamezingua. basi bora angevaa kininja tusione sura yake.
Hakuna mwenye uhakika huyo alikuwa ni mwanaume na mlinzi WA RaisiLakini Kuna andiko linakataza mwanaume kuswali na wanawake!?
Bandari baadaye. Kwanza jee mlinzi wa rais alikuwa sawa kuingia upande wa wanawake kuswali!??Tutapambania bandari, hilo sio suala la kidini 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Umewajibu shura hivyo!Msikiini si kila anayeingia huulizwa yeye nani
Huyo MTU aliingia kama wanawake wengine kuswali sio mlinzi WA Raisi na Raisi mwenyewe hamjui
Shura ya maimamu iko straight forward, hawajiumiumi, Kama umekosea wanakuambia.Asante sana kwa ufafanuzi.
Naomba kuuliza shura ya imam na bakwata wana kauli moja ama kila mmoja ana kuwa na kauli yake haswa kwa maswala tata kama haya.
Tuseme alikuwa mwanaume. Jee kiimani anakatazwa kuswali upande wa wanawake!?Hakuna mwenye uhakika huyo alikuwa ni mwanaume na mlinzi WA Raisi
Msingi wa kukosea unajengwa juu ya nini!?Shura ya maimamu iko straight forward, hawajiumiumi, Kama umekosea wanakuambia.
Bismillahir Rahmanir Rahiim
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
KAMATI YA MAADILI
WARAKA WA WAZI KWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI
JUNI 18, 2024.
‘MLINZI MWANAMUME WA RAIS KUVAA HIJABU NA KUINGIA MSIKITINI’
Shura ya Maimamu imeona malumbano yanayoendelea katika Mitandao ya Kijamii kuhusiana na picha inayomuonesha mtu anayekisiwa kuwa ni mwanamume akiwa amevaa mavazi ya kike ya Kiislamu.
Picha hiyo inamuonesha mtu huyo akiwa pamoja na wanawake wa Kiislamu akiwa nyuma ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Msikitini
Picha hiyo inasemekana ilichukuliwa katika Swala ya Idd Adh-Ha iliyo swaliwa juamatatu Juni 17, 2024, katika Msikiti wa Mikocheni (kwa Warioba), jijini Dar es Salaam.
Katika malumbano hayo inaelezwa kuwa mtu huyo ni miongoni mwa timu ya walinzi wa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na alikuwa Msikitini hapo kikazi.
MAKOSA MAKUBWA
Shura ya Maimamu imo katika juhudi ya kupata hakika ya mtu huyo kama ni sehemu ya ulinzi wa Rais Samia Suluhu Hassan au laa. Hata hivyo ikiwa tukio kama hilo litaihusisha serikali yoyote ile tunasema ifuatavyo:
Ifahamike kuwa Wanawake wa Kiislamu huvaa mavazi ya stara kusitiri aura zao mbele ya wanaume wasio waume zao.
Lakini wanapokuwa sehemu ya wanawake Msikitini huwa huru kupunguza stara zao kwa kuamini kuwa hakuna mwanamume atakaye waumbua.
Kwa hiyo mwanamume kuingia sehemu hiyo tena kwa kificho, ni kudhamiria kuwaona utupu wanawake hao wachamungu wenye tabia ya kujistiri. Na hiicho ni kitendo kibaya cha kuwadhalilisha na kuwafedhehesha wanawake wachamungu.
Vilevile Wanawake wa Kiislamu wanapo swali hujipanga katika safu peke yao mbali na wanamume. Kitendo cha kumuweka mwanamume miongoni mwao kisha wakagusana tena ndani ya swala kinaharibu swala zao.
Pia ni kutendo cha kukiuka sheria zinazolinda uhuru wao wa kuabudu. Kitendo hicho pia kinavunja utukufu na heshma ya nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu, Msikiti.
Turejee kusema iwapo mwanamume atajitanda kwa mavazi ya wanawake kisha akaingia Msikitini upande wa wanawake basi hicho ni kitendo kibaya kabisa kinachofedhehesha dini na hata usalama wa taifa.
Shura ya Maimamu inakemea vikali kitendo hicho kisifanywe na ikiwa kimefanywa mfanyaji, na walioidhinisha wanapaswa kuwaomba radhi Waislamu.
Iwapo wahusika hao ni Waislam, wanapaswa kutubu kwa Allah (SW) kwa kutothamini dini yao.
WITO KWA SERIKALI
Shura ya Maimamu inatoa wito kwa vyombo husika vya Dola Tanzania kutoa ufafanuzi iwapo ni kweli kwamba msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan ulijumuisha mlinzi mwanamume aliyeingia Msikitini sehemu ya wanawake na kwamba alifanya hivyo akiwa amefichama kwa kuvaa hijab, vazi la stara la wanawake wa Kiislamu.
Shura inasisitiza kuwa ufafanuzi huo ni muhimu sana kupatikana kwa haraka kwa sababu zifuatazo:
1. Kuondoa taharuki miongoni mwa jamii, na hususan wanawake wa Kiislamu.
2. Ikiwa serika ya Tanzania imehusika, ni muhimu Umma ufahamishwe tukio hilo ni la mara ya kwanza au ndio utaratibu wa kiulinzi toka Rais mwanamke alipokuwa Makamu wa Rais na sasa Rais.
3. Umma ufahamishwe iwapo mlinzi huyo ni yeye pekee au wapo wengine wanaume wanaoingia na Rais Msikitini upande wa wanawake wakiwa wamevaa hijabu.
4. Umma ufahamu mlinzi huyo kuvaa hijabu na kuingia kwa kificho Msikitini kwa wanawake ni utashi wake au ni utaratibu wa kazi aliopangiwa.
5. Wananchi wana haki ya kupata ufafanuzi kwa serikali yao pindi linapotokea jambo lenye kutatiza katika jamii.
Katika kuhitimisha, Shura ya Maimamu inarejea wito wake kwa kuhimiza vyombo husika kitoa ufafanuzi wa suala hili kwa muktadha wa nukta tulizoainishwa hapo juu .
Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2024.
USTADHI MUSTAFA M. ABEID
KATIBU KAMATI YA MAADILI
Kabisa...Kwa utaratibu huu wa wanaume kuvaa mavazi ya kike msikitini, usalama wa Rais uko hatarini na vyombo vya dola visijidanganye kuwa vinaimarisha ulinzi wa Rais!
Baadhi ya misikiti hairuhusu wanaume na wanawake kuchanganyika wanaposali lakini misikiti mingine huruhusuTuseme alikuwa mwanaume. Jee kiimani anakatazwa kuswali upande wa wanawake!?
Hakika wapo straight mno, kwa kweli maswali hoja zao zinapaswa kujibiwa kwa ufasaha na wahusika, sambamba na kuomba radhi.Shura ya maimamu iko straight forward, hawajiumiumi, Kama umekosea wanakuambia.
Wapi huko na msikiti upi?Baadhi ya misikiti hairuhusu wNaume na wanawake kuchanganyika wanaposali lakini misikiti mingine huruhusu
Kwa hili Rais anahusika kwa 100%, hawezi akajitetea kuwa hakufahamu!Waislamu wamkatae kiongozi anayedharau dini Kwa kuingia na wanaume sehemu ya wanawake!!