Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Lakini Kuna andiko linakataza mwanaume kuswali na wanawake!?
Hakuna,Ila Quran inaaguza kutogusana jinsia tofauti baada ya kutia udhu,swala ya kiislam kwenye safu nyayo hugusana,japo Aya hiyo Kuna tafsiri pia kwamba kugusa hapo maana yake kugonga Kama Maryam alivyosema kwenye Aya nyingine 'nitapataje mtoto ilhali sijaguswa na mwanaume',so ili uwe salama baada ya udhu usigusane na jinsia tofauti
 
Shura ya maimamu ni miongoni mwa taasisi ambazo waislam waliunda kujikomboa toka bakwata,baada ya mwinyi kuambiwa na mufti hemed bin jumaa 'inaelekea Nyerere hakukwambia bakwata ni nini'.. mwinyi akawaasa waislam waunde taasisi nje ya bakwata,ndiyo likaundwa 'baraza kuu' na taasisi nyingine chini yake ikiwemo shura
Asante kwa kutufahamisha mkuu, kwa hio kwa ujumla wake wanaweza wasiive chungu kimoja, maana msimamo wao huu naamini kabisa bakwata wangekuja vinginevyo.
 
Maana bila andiko (surah) wakija BAKWATA wakasema PSU walikuwa sahihi kuingiza mwanaume msikitini, hapo utazuka utata.

Ili kusiwe na utata ni lazima mtizamo wa kuunga mkono ama kupinga ujengwe juu ya Quran tukufu ama hadithi inayokubalika kwa wote.
Mwisho wa siku watafungwa na hoja ulazima wa huyo mlinzi wa rais kuvaa mavazi ya kike, kama ilikua ni lazima kuingia sehemu hio huyo mlinzi kwa nini hadaa imetumika ya kuvaa mavazi ya kike?
 
Mwisho wa siku watafungwa na hoja ulazima wa huyo mlinzi wa rais kuvaa mavazi ya kike, kama ilikua ni lazima kuingia sehemu hio huyo mlinzi kwa nini hadaa imetumika ya kuvaa mavazi ya kike?
Inawezekana hapo ni mambo ya kiufundi.

Ila PSU wameonesha udhaifu katika kujipanga kwao.
 
Watu wengine mna haiba ya kitumwa mpaka inashangaza. Mnaishi wapi wakati dunia imepiga hatua kubwa kabisa na watu wanajitambua? Watu wa usalama ni Malaika? Hawaulizwi? Wana turufu ya kufanya chochote? NB: kwenye hayo ya malumbano ya sijui dume kuingia msikitini siko kwa sababu inawezekana siyo mwanamke. Nimechangia kwa sababu nimeshangaa unavyojidhalilisha kama wewe siyo binadamu mwenye utu.
Ebu nenda pale Lugalo kawaulize mwenyewe
 
Lakini Sheikh Ponda si ndie aliyekuwa anasema leo kwamba maisha yamekuwa magumu sana Awamu ya Sita?
Sasa,baada ya maisha kuwa magumu Shekh Ponda hadhanii kwamba anaweza kuwepo mwanamke anataka 'kumfua' Mheshimiwa rais?
Wakishindwa kuelewana kuhusu hili swala,tutarudi kwenye siasa za Mwembechai.
Na watashindwa kuelewana; kwa sababu watajadiliana,halafu watawauliza Al- Azhar University,Cairo,watauliza Msikiti Mkuu,Makka,halafu unadhani watajibiwa nini?
Kwa hiyo busara itumike,tatizo dogo lisilete fujo kubwa.
 
Maana bila andiko (surah) wakija BAKWATA wakasema PSU walikuwa sahihi kuingiza mwanaume msikitini, hapo utazuka utata.

Ili kusiwe na utata ni lazima mtizamo wa kuunga mkono ama kupinga ujengwe juu ya Quran tukufu ama hadithi inayokubalika kwa wote.
Kuna somo linaitwa Fiqh! Fiqh ni kujua kitu kwa undani. Fiqh ni mjumuisho wa Qur'an na Sunna ambazo zinatoa kanuni na mwongozo. Kwa ujumla Fiqh ni sheria/sharia.

Sunna ni kauli na matendo ya Mtume Muhammad s.a.w: Haikuthibiti kwa mwanamke na mwanaume kuswali kwa kuchanganyika kwa swafu (kupanga mstari) moja. Bali wanaume watajikusanya kivyao kuswali na wanawake watajikusanya kivyao kuswali huku wakiongozwa na mwendesha ibada mmoja (imam).
 
Back
Top Bottom