Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Naye si angenyoa hizo ndevu zake...!
Ila kwakuwa hakuna Aya inayo kataza wanawake kuswali peke yao basi shura ya Maimamu haikustahili kukosoa hilo jambo.
 
Mkuu Angalia (Dili) na Waumin wengine wadogo, Wadogo. Mambo ya Serikali na Safu ya Ulinzi wa Rais n siri nzito. Pia kumbuka serikali Haina Dini
Pamoja na kwamba serikali haina dini, huheshimu dini za raia wake.

Haya mambo naona kama ni kumtega Rais, kuchafua serikali na kuigombanisha na raia kupitia dini kwa makusudi.

Inashindikana vipi kudhibiti kusanyiko la wanawake lilopangwa mpaka mwanaume ajivalishe hijab?

Kama kulikuwa na viashiria vya hatari, Rais mwanamke angewakilishwa na mwanaume.

Pili, shura ya maimamu inatakiwa ifanye uchunguzi wake, ikemee na itoe ushauri namna ya kuhakikisha usalama wa Rais katika matukio kama hayo ikishirikiana na vyombo vya dola.

Isisubiri kuomba radhi, maji yakimwagika hayazoleki.
 
Kwani Papa aliporuhusu mashoga kubarikiwa vatican aliweka andiko?
Unachanganya mada.
Wewe hujui kua wanawake hawachanganyiki na wanaume kwenye misikiti?
Najua. Lakini ni utamaduni tu ama ni sharia ya dini!?
Kwahiyo hao watu wa ulinzi wameingia kwa wanawake coz hawajui hilo andiko?
Inawezekana...
Ingekua hawajui kua wanawake hawachanganyiki na wanaume,wasingejificha kwa kuvaa hijabu.
Hawakujificha ila mazingira yaliwataka iwe hivyo.

Rais ameingia sehemu wapo wanawake peke yao. Unataka na mtu wa PSU aingie kama mwanaume?

Hivi wangeingia kikawaida si ndiyo ingezua taharuki siku ile ile!!??
 
Nimetafuta kama kuna andiko limewekwa linalokataza wanaume kuswali na wanawake sijaona.

Wangeweka hilo andiko bila ya shaka lingeongezea uzito wa habari yenyewe
Wenzetu huwa kwao utaratibu wa dini ndio muhimu zaidi kuliko andiko la Mungu. Kwao mungu = dini
 
Unachanganya mada.

Najua. Lakini ni utamaduni tu ama ni sharia ya dini!?

Inawezekana...

Hawakujificha ila mazingira yaliwataka iwe hivyo.

Rais ameingia sehemu wapo wanawake peke yao. Unataka na mtu wa PSU aingie kama mwanaume?

Hivi wangeingia kikawaida si ndiyo ingezua taharuki siku ile ile!!??
Mtu kama wewe hata kukujibu ni kazi bure tu,maswali yako ya kijinga yanaashiria kua uwezo wako wa uelewa na kuchanganua mambo ni mdogo sana,najua kua unateswa na udini,

Rudia tena kusoma hilo tamko aliloweka mleta mada,majibu yamo humo tayari.
 
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

KAMATI YA MAADILI

WARAKA WA WAZI KWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

JUNI 18, 2024.

‘MLINZI MWANAMUME WA RAIS KUVAA HIJABU NA KUINGIA MSIKITINI’

Shura ya Maimamu imeona malumbano yanayoendelea katika Mitandao ya Kijamii kuhusiana na picha inayomuonesha mtu anayekisiwa kuwa ni mwanamume akiwa amevaa mavazi ya kike ya Kiislamu.

Picha hiyo inamuonesha mtu huyo akiwa pamoja na wanawake wa Kiislamu akiwa nyuma ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Msikitini

Picha hiyo inasemekana ilichukuliwa katika Swala ya Idd Adh-Ha iliyo swaliwa juamatatu Juni 17, 2024, katika Msikiti wa Mikocheni (kwa Warioba), jijini Dar es Salaam.

Katika malumbano hayo inaelezwa kuwa mtu huyo ni miongoni mwa timu ya walinzi wa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na alikuwa Msikitini hapo kikazi.

MAKOSA MAKUBWA

Shura ya Maimamu imo katika juhudi ya kupata hakika ya mtu huyo kama ni sehemu ya ulinzi wa Rais Samia Suluhu Hassan au laa. Hata hivyo ikiwa tukio kama hilo litaihusisha serikali yoyote ile tunasema ifuatavyo:

Ifahamike kuwa Wanawake wa Kiislamu huvaa mavazi ya stara kusitiri aura zao mbele ya wanaume wasio waume zao.
Lakini wanapokuwa sehemu ya wanawake Msikitini huwa huru kupunguza stara zao kwa kuamini kuwa hakuna mwanamume atakaye waumbua.

Kwa hiyo mwanamume kuingia sehemu hiyo tena kwa kificho, ni kudhamiria kuwaona utupu wanawake hao wachamungu wenye tabia ya kujistiri. Na hiicho ni kitendo kibaya cha kuwadhalilisha na kuwafedhehesha wanawake wachamungu.

Vilevile Wanawake wa Kiislamu wanapo swali hujipanga katika safu peke yao mbali na wanamume. Kitendo cha kumuweka mwanamume miongoni mwao kisha wakagusana tena ndani ya swala kinaharibu swala zao.
Pia ni kutendo cha kukiuka sheria zinazolinda uhuru wao wa kuabudu. Kitendo hicho pia kinavunja utukufu na heshma ya nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu, Msikiti.

Turejee kusema iwapo mwanamume atajitanda kwa mavazi ya wanawake kisha akaingia Msikitini upande wa wanawake basi hicho ni kitendo kibaya kabisa kinachofedhehesha dini na hata usalama wa taifa.

Shura ya Maimamu inakemea vikali kitendo hicho kisifanywe na ikiwa kimefanywa mfanyaji, na walioidhinisha wanapaswa kuwaomba radhi Waislamu.

Iwapo wahusika hao ni Waislam, wanapaswa kutubu kwa Allah (SW) kwa kutothamini dini yao.

WITO KWA SERIKALI

Shura ya Maimamu inatoa wito kwa vyombo husika vya Dola Tanzania kutoa ufafanuzi iwapo ni kweli kwamba msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan ulijumuisha mlinzi mwanamume aliyeingia Msikitini sehemu ya wanawake na kwamba alifanya hivyo akiwa amefichama kwa kuvaa hijab, vazi la stara la wanawake wa Kiislamu.

Shura inasisitiza kuwa ufafanuzi huo ni muhimu sana kupatikana kwa haraka kwa sababu zifuatazo:

1. Kuondoa taharuki miongoni mwa jamii, na hususan wanawake wa Kiislamu.

2. Ikiwa serika ya Tanzania imehusika, ni muhimu Umma ufahamishwe tukio hilo ni la mara ya kwanza au ndio utaratibu wa kiulinzi toka Rais mwanamke alipokuwa Makamu wa Rais na sasa Rais.

3. Umma ufahamishwe iwapo mlinzi huyo ni yeye pekee au wapo wengine wanaume wanaoingia na Rais Msikitini upande wa wanawake wakiwa wamevaa hijabu.

4. Umma ufahamu mlinzi huyo kuvaa hijabu na kuingia kwa kificho Msikitini kwa wanawake ni utashi wake au ni utaratibu wa kazi aliopangiwa.

5. Wananchi wana haki ya kupata ufafanuzi kwa serikali yao pindi linapotokea jambo lenye kutatiza katika jamii.

Katika kuhitimisha, Shura ya Maimamu inarejea wito wake kwa kuhimiza vyombo husika kitoa ufafanuzi wa suala hili kwa muktadha wa nukta tulizoainishwa hapo juu .

Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2024.

USTADHI MUSTAFA M. ABEID
KATIBU KAMATI YA MAADILI
Mkichunguza mkajiridhisha kuwa alikuwa mwanaume then mtuambie nani huyo aliachana na kuswali akabakia kupiga picha ya wanaoswali.
 
Asante sana kwa ufafanuzi.
Naomba kuuliza shura ya imam na bakwata wana kauli moja ama kila mmoja ana kuwa na kauli yake haswa kwa maswala tata kama haya.
Wameshakwambi ni shura ya maimam meaning watu wasiofata sheria za mwenyezi mungu bali za dini tu
 
Back
Top Bottom