Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Mimi binafsi siyo muislam ila niseme tu kuwa ikiwa kitendo hicho kimefanyika basi ni makosa makubwa mno yaliyofanywa na waliompangia kazi huyo jamaa na hata kumshauri avae nguo za kike.

Huo ni udhalilishaji kwa akina mama wachaMungu walioingia Msikitini kusali.

Kitendo hiko kitapotezewa kwa kuwa tu Rais ni Muislam ila angekuwa Mkristo, sipati picha ingekuaje.

Ikiwa ni kweli basi serikali iwaombe radhi waislamu wote na watu wachukue tahadhari ili watu wasiendelee kujificha kwa mavazi hayo ambayo hayamtambulisha mtu.
Na inaonekana siyo mara ya kwanza kitendo kama hicho kufanyika.
 
Mimi nadhani wahusika walifafanue hili swala vizuri tu kisije kikaonekana kama kitendo cha makusudi cha kuunajisi Msikiti,Tafsiri yake katika medani za kisiasa huko mbeleni inaweza kuleta athari hasi wakati ni jambo tu linahitaji ufafanuzi.
 
MAKOSA MAKUBWA
Shura ya Maimamu imo katika juhudi ya kupata hakika ya mtu huyo kama ni sehemu ya ulinzi wa Rais Samia Suluhu Hassan au laa. Hata hivyo ikiwa tukio kama hilo litaihusisha serikali yoyote ile tunasema ifuatavyo:
Yaani hawa jamaa sijui vipi? Mwanaume, asiyekuwa mlinzi, kukaa jirani na Rais, atakuwa nani huyo?!!
 
Nikikuwa nasubiri tamko lako. Mpaka hapa unaonesha undumilakuwili waziwazi! Uko tayari kunajisi imani yako kisa UCHAWA!
Mtu kumjua kama ni Mwanaume au Mwanamke lazima uione eneo lake la Siri kama la kike au kiume.

Huo ndio ushahidi wa uhakika

Huwezi kokodolea tu macho mtu ukasema yule ni Mwanamke au mwanaume

Mwenye huo ushahidi kwenye hiyo shura ya maimamu aweke
 
Hivi upo ndani ya nyumba ya ibada, halafu unataka ulinzi gani tena? Kama ulinzi ni muhimu ndani ya nyumba ya ibada basi haya mambo ya kuabudu tumetengeneza!!!
Anapokuwa ndani ya nyumba ya Mungu na kiti chake huwa hamuoni?
 
Back
Top Bottom