Si hata Rais Mstaafu Mwinyi walisema anauza nchi? Kiko wapi?

Umeongea kweli tupu. Tuliokuwepo tunajua hali ilivyokuwa. Bahati mbaya sana, wengi wa wanaojifanya wachambuzi wa utawala walikuwa vijijini tena habari pekee enzi hizo ni RTD hivyo hawakuwa wakijua kilichokuwa kinaendelea mijini hasa Darisalaama. Rais Mwinyi ndiye muanzishi wa uchumi tunaouona leo. Ila kuna watu tayari wana maradhi mioyoni mwao, hawatataka kuelewa.
 
Utasemaje aliuza Loliondo wakati vibali vya uindaji vinatolewa na kufutwa na Rais yeyote?
Mkapa kwanini hakufuta? Kikwete? Magufuli??hao wote wasifute vibali ??
Au hajui ardhi yote Tanzania iko chini ya Rais??anaweza futa hati yeyote??
Kufuta mikataba holela ndio magufuli amesababisha ndege zinakamatwa huko nje.
 
Mie sitasahau kipindi cha JK

Kila petrol station mpya inayojengwa walikuwa wanasema ya Ridhiwani. Baada ya Mzee Kikwete kutoka madarakani yale maneno yote yalipotea alafu watu wakajikausha kama sio wao
 
Mie sitasahau kipindi cha JK

Kila petrol station mpya inayojengwa walikuwa wanasema ya Ridhiwani. Baada ya Mzee Kikwete kutoka madarakani yale maneno yote yalipotea alafu watu wakajikausha kama sio wao
Mimi nakumbuka ule uzushi wa Riziwan kukamatwa China...huwa nacheka Sana ukiona mtu msomi anaongea vitu vya vijiwe vya bodaboda
 
Sawa endeleeni na yenu bana simshasaini tabu iko wapi. Msituchoshe
 
Mzee Mwinyi alikuwa na wazo hilo zuri na kutokana na washauri wake aliona ajaribu kurekebisha uchumi kupitia ushauri pia wa IMF na WB.

Usisahau kwamba hata hayati Nyerere sera zake ziliingiliwa na mipango mipya ya IMF na WB ambayo ilisisitiza kuwepo marekebisho ya uchumi (restructuring) na hiyo ilitokana na hali mbaya ilotokana na athari za vita ya Uganda.

China hawakuwa na ushauri wowote wa IMF wala WB na walianza kazi moja kwa moja.

Hivyo tukiongelea sera za uchumi za Tanzania tusisahau mikopo na kamba za masharti kutokea IMF na WB.

Je, wafahamu pia kuwa China haikuwa mwanachama wa WTO hadi mwaka 2001 ilipojiunga rasmi na walikuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Sababu kubwa ni kwamba uchumi wa China wafuata modeli tofauti kabisa na kanuni au framework ya WTO hivyo China hawakutaka hiyo framework ya WTO ambayo nchi nyingi duniani zimebanwa nayo.

Hivyo ni kweli mzee Mwinyi alianzisha mambo hayo ya Trade Liberalization lakini alihitaji mipango thabiti khasa hali ya uchumi wa ndani, kiwango cha watu wasoajiriwa na masuala mengine "domestically" kabla ya kwenda kuingiza kila kitu ndani ya nchi kutoka nje.
 
We jamaa unachokitetea sijui ni nini
 
Asante sana Mkuu umenikumbusha mbali sana 1983 nauza dawa za mbu za vipande na mimi nilikuwa kataka kundi la watu wanaoitwa walanguzi kipindi hicho maisha yalikuwa magumu usipime

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mzee Mwinyi: Mambo yaliyotushinda sisi Marais Watatu kwa miaka 30 Shujaa Magufuli ameyafanya kwa miaka 3
Mzee Mjanja yule

alijua kupata cha kwny uvungu wa Mjinga we mpe misifa tu

mwanae sasa hivi anatembelea ving'ora kutokana na ile misifa

Mwinyi na Familia yake wanakula Matunda ya Uhuru, Muungano na Mapinduzi matukufu kuliko familia yeyote ile japo hakushiriki harakati za uhuru, Mapinduzi wala Muungano
 
Asante sana Mkuu umenikumbusha mbali sana 1983 nauza dawa za mbu za vipande na mimi nilikuwa kataka kundi la watu wanaoitwa walanguzi kipindi hicho maisha yalikuwa magumu usipime

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Zile dawa hovyo, maana zawalevya mbu kisha mbu hao baadae huamka na kurudi kwenye eneo la tukio (kwenye ngozi za watu) kuendelea na kazi.

Baada ya wiki mbili mtu na homa ya malaria.
 
Akili ni nywele

Hakuna binadamu asiyependa Sifa!
 
Jiridhishe na fact zako mkuu. China alitamani awe founding member wa GATT/WTO lakini attempts zake ziliwekewa ngumu na US, EU, Japan na si kwamba mwenyewe hakuwa akitaka. Yes, sababu kubwa yakukataliwa kujiunga ni kutakiwa kutekeleza sera za uchumi wa Soko.

Kumbuka China kukua kwake kiuchumi kulichangiwa sana na Marekani ambapo mbali ya mikopo aliyopewa lakini pia alipewa "most favoured nation" status na US. Hii ni kwasababu China alikuwa na makubaliano maalum ya kununua industrial goods kutoka US na kuuza pamba yake US akibadilishana na mattekta kabla hajafanya u-turn.

Alipopunguziwa favor za kufaidika na masoko ya EU na US, huku mpango wake wa "modernization program" ulipofanikiwa, hakuwa na namna zaidi ya kukubali masharti ya uchumi wa Soko na hivyo kuwa mwanachama wa WTO.
 
Mbona unachanganya limao na machungwa,kwa kila kipindi Dunia huwa inapitia kwenye hatua fulani au njia fulani za kiuchumi.By that time Nyerere ana opt Sera za kijamaa-ndicho kipindi ambacho Sera hiyo ilikuwa inasambaa duniani kote huku kinara wake akiwa U.S.S.R.

USA na west countries ziliogopa kukua kwa Sera hiyo kwenye Nchi za Ulaya mashariki,Asia na Afrika.Ndipo wakaja na mkakati maalumu wa kuudhofisha Sera hiyo na kupropaganda Sera ya ubepari.

Mwinyi kuruhusu biashara huria hakuwa chaguo but ilikuwa ni lazima kutokana na hali halisi ya mazingira ya kiuchumi yalivyokuwa Tanzani na duniani.
 
Mimi nakumbuka ule uzushi wa Riziwan kukamatwa China...huwa nacheka Sana ukiona mtu msomi anaongea vitu vya vijiwe vya bodaboda
Nchi ina watu wapuuzi sana hii. Yale majengo ya makambi ya majeshi yaliyokuwa yanajengwa Msata ati ya Rizwan. Barabara ya Bypass kutoka Tanga kupitia Msoga kama unaenda Morogoro ulipingwa pia at Rizwan ndo kaamrisha.. Barabara ya Bagamoyo Msata ilipingwa kwamba anajipndelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…