Mkuu
The Boss,
Ni kweli serikali ya China walimiliki njia kuu za uchumi na kupanga sera zote za uchumi kutoka serikalini (central Planning)
Lakini wachina walinza kurekebisha uchumi wao rasmi mwaka 1978 na wakati huo Tanzania sera za Azimio la Arusha zimeyumba sana.
Mabadiliko ya uchumi wa China yaliitwa Reform and Opening Up na yalibuniwa na Deng Xiaoping akiongoza wanamabadiliko wengine ndani ya chama cha kikomunisti cha China CCP.
Mabadiliko ya uchumi wa China yalikuwa ni mabadiliko kwelikweli kuanzia ndani ya China yenyewe yaani uwekezaji binafsi, ubunifu na ujasiriamali, na ukuzaji uchumi kwa ajili ya soko la ndani. Baada ya hatua hiyo Wachina wakaingia kwenye kuhakikisha waongeza umri wa kustaafu kazi, kudhibiti watu waso na kazi (unemployment) kwa kuhakikisha watu waenda kufanya kazi viwandani, kuhudumia walohitaji huduma za afya na mwisho kufanya mabadiliko katika makampuni na mashirika ya umma katika kuyaendesha na usimamizi wake.
Mwaka 1989 kukawa na matatizo ambayo yalipelekea kukawa na yale maandamano maarufu pale Tiananmen Square na kuna watu walizuia vifaru vya jeshi na watu wengi walikufa.
Maandamani yalee yalitokana na hali ngumu ya uchumi kwani ukianza kufanya mabadiliko ya uchumi ili uuweke sawa ni lazima kuna asilimia kubwa ya watu wataathirika na vyuma vitaanza kubana, na hapo Wachina walijiandaa kwa hilo.
Baada ya haya mambo ya maandamano kuisha mwaka 1992 bwana Deng Xiaoping akafanya ziara kubwa sana kusini mwa China kwenye miji ya Zhuhai, Ghuangzou, Shenzhen na Shanghai na hotuba yake ilikuwa ndo kiini cha miji hiyo kuwa ilivyo leo hii na Ghuangzou ukiwa kitovu cha biashara cha kimataifa.
Hotuba ya Xiaoping ilikuwa ni ya kusisimua na yenye kutia hamasa akasema, ataka mji wa Ghuangzou ufanane na nchi nne ziloitwa Four Asian Tigers ndani ya miaka 20.
Naam, mwaka 2014 China ilikuwa imeipita Japan na kuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani.
Hivyo, chama cha CCP walifanya na mambo makuu kwa hatua mbili kama yafuatayo:
Hatua ya kwanza
1. Kwa miaka 10 (1970 hadi 1980) kurekebisha njia zitumikazo kwa kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa zaidi ili kupata mazao mengi kulisha nchi, kuweka akiba na kuuza nje.
2. Kufungua nchi kwa ajili ya mitaji ya moja kwamoja yaani Direct Investiment.
3. Kuruhusu wajasiriamali kufanya biashara bila woga na kuondoa urasimu.
4. Pamoja na hayo yote mashirika na makampuni ya umma yaliendelea kuwa chini ya serikali.
Hatua ya pili 1980- 1990
1. Kubinafsisha mashirika na makampuni ya umma au serikali kwa watu binafsi/makampuni binafsi ili wayaendeshe chini ya usimamizi mkali.
2. Kuingia mikataba na watu/ makampuni binafsi kuendesha makampuni na mashirika ya umma.
3. Kuondoa udhibiti wa bei na masoko.
4. Kuondoa sera na sheria ngumu zinodhibiti ukuaji wa biashara na mitaji yake.
5. Pamoja ya yote hapo juu bado njia kuu za uchumi kama mabenki, bandari, mashirika kama ya mafuta na rasilimali zingine yalibaki kuwa chini ya serikali.
Mambo haya niloeleza , ndiyo yaliifanya sekta binafsi nchini China kukuwa sana na GDP kufikia asilimia mwaka 2005 na wakti huo bwana Hu Jintao na baadae bwana Wen Jiabao wakiwa mawaziri wakuu waliendeleza libeneke na kuanzia hapo China ikawa tishio kwa Marekani.
CCM imekuwa madarakani tangia ilipoasisiwa kutoka TANU na imeshindwa kuiweka Tanzania katika moja ya mataifa bora kiuchumi katika eneo la maziwa makuu na ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Hatua alozichukua Hayati Mwalimu ni kweli alitaka kuiga Wachina, lakini alikosa watu wa kumsaidia kuangalia ni wapi afanye aloyataka au wapi aache kubana. Pia hata alipokuja mzee Mwinyi nae alishauriwa vibaya juu ya utandawazi na marekebisho ya Uchumi.
Alipokuja hayati Mkapa ndio akaharibu kabisa kwa kuachia njia kuu za uchumi kama benki ya NBC kwenda kwa wageni ambao walimiliki asilimia zaidi ya 60 nq hata yeye mwenye kujigawia sehemu ya rasilimali za taifa.
Mzee Kikwete yeye alitaka tu kufanya kitu chaitwa Checks and Balances (nafikiri wale mazee watanielewa hapa) na mwisho wake uchumi haujulikani umesimama wapi na nani audhibiti.
Alipokuja hayati JPM alijikuta amechelewa na sanasana akaamua kufanya aloyafanya na yalikuja kuleta athari kubwa maana hakujipanga sawasawa.
Wachina walijipanga kwa kila kitu kuanzia chama chenyewe cha CCP na hakukuwa na maombi popote pale ni kazi tu.
Unapofuata sera za Glasnost (uwazi) na Perestroika |(marekebisho) watakiwa kuwa mkweli na si mjanja kama Mikhail Gorbachev ambae kumbe kwa pembeni alikuwa aiuza USSR mpaka ikaanguka.
Lakini Wachina wamefuata kiukweli sera za Glasnost na Perestroika na le hii China ni nchi yenye uchumi mkubwa duniani.