Si kila anaeenda dukani anatafuta pesa, Wengine wanaenda sababu wamechoka kukaa nyumbani, auze asiuze bado atakuja na gari na kula vizuri

Mkuu ni duka classique, nguo za 50 hadi laki 3🤣
Ndio hao hao wakipewa mitaji ya milioni 10 wanaanza kuwaza biashara wanazoziona kwenye muvi na series za wakorea maana hata mtaji wamepewa tu hawajui uchungu wa kuumiza kichwa hata kupata location nzuri wao popote sawa tu

Hebu msome huyo namba mbili niliemweka
 
Ndio hao hao wakipewa mitaji ya milioni 10 wanaanza kuwaza biashara wanazoziona kwenye muvi na series za wakorea maana hata mtaji wamepewa tu hawajui uchungu/

Hebu msome huyo namba mbili niliemweka
😀😀😀😀😀
 
Ila wakt mwingine wale wanawake Ni madanga mm Niko ktk frem fln hapa ddm mwanamke huyu anafungua duka lake saa tano au sita na Ni miamala anafanya Kodi 300k
 
Watu wako wanatakatisha pesa tu,hizo biashara zao ni zuga tu!!
 
biashara zina siri nyingi sana aisee.

ndio sababu sio kila mtu anafanya[emoji28][emoji28].

unapata frem kodi 150k kwa mwezi,unajaza bidhaa za mtaji hata wa 5miln,kwa siku zinatoka bidhaa 2 za 20k@
ukitoa gharama za ulanguzi,ghalama za frem,chakula ukiwa hapo,nauli ukienda,bando na umeme unaotumia ukiwa hapo.sijui unabaki na shingapi!!lakini mtu anayo frem husika miaka unaiona tu[emoji28][emoji28].
 
Niliwahi kufanya kazi kwenye biashara ya mtu, alikua kati ya hapo watatu uliowataja hapo juu, ilikua raha sana, ni mda umepita ila bado ipo vilevile.
 
Ila sisi binadamu wa kiume tuna taabu sana. Ni sehemu chache sana unamkuta mwanamke anamsapoti au kumweka mjini mwanamume. Aisee, hizo zote ni mojawapo za tabia za ukwasi uliopitiliza kwa wanamume maana si kwa kujikamua huko kusiko na faida ili kumfurahisha mtu. Mtu ashinde dukani buree hadi jioni na bila tija! Wengine wananufaika kutokana na wenye mali/mwenye duka au mradi kutokuwa na mipango madhubuti na ufuatiliaji wa biashara. aidha, mwenye mali yupo mbali na eneo la biashara na muuzaji ni mlipwa mshahara.

Kwa huyo anayefungua duka saa nne au kufunga saa tano asubuhi, hao wote ni wagongwaji/vimada wa watu maana wanavizia watu wakiwa kazini ndo wafanye yao. huyo anayefungua saa nne hana wateja wa uhakika kwa sababu biashara yake inafanyika bila mpangilio maalum.

USHAURI: Kila wakati uzembe katika uendeshaji wa biashara au rasilimali husababishwa na wahusika kutofahamu HASARA inayoweza kuwapata na madhara yanayofuatana na hasara hiyo. Aidha, wahusika wanaweza wakawa wanafanya hivyo kwa makusudi.

KILA MTU NA AFANYE KAMA ALIVYOKUSUDIA MOYONI MWAKE MAANA ATAVUNA KWA WAKATI WAKE.
 
Kuna ndugu yangu ana duka la viatu, fremu analipa bei ghari ila ndani hata piece 100 za viatu hazifiki, na anaweza akamudu kusafiri kwa ndege kuja mkoani, kuna muda anaenda mpaka nje ya nchi eti kuchukua viatu.
 
Sasa Masters wa michezo hii ya kuzuga ni WAHINDI wa kule Kisutu, duka analouza na mali anazomiliki tofauti

Mjini mipango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…