Si kila Mchungaji, Nabii au Mtume anayetumia Biblia kufundisha ni Mkristo, wengine ni matapeli

Si kila Mchungaji, Nabii au Mtume anayetumia Biblia kufundisha ni Mkristo, wengine ni matapeli

Na si kila mchungaji/nabiii/mtumishi wa Mungu anaesema Kaenda Mbinguni Ni Tapeli/Mwizi

Kuna mindset nimeanza kuiona shetani anai iingiza kwa watu "indirect way" yani sasa hivi mtumishi

wa Mungu akisema kaongea na YESU katka MAONO watu wanaguna kimya kimya,akisema Ameonyeshwa Mbingu na yanayofanyika huko '"watu wanaguna kimya kimya"

Shetani ameshaanza kufanikiwa kuondoa TRUST ya wanadamu kwa watumishi wa MUNGU wa kweli,na katika hili shetani alitumia akili nyingi sana ili ku win hii game.

Aliingiza Manabiii FEKI,watumishi FEKI akawapa PROMO wakajulikana halafu akaanza wafanya wafanye vituko,kwasababu tumeshawajua ina maana chochote watachofanya tutakiona,wanafanya ujinga wa wazi na makusudi kabisa.. hiii ni TARGET ya shetani kukuondolea TRUST kwa watumishi halisi wa MUNGU.

Dunia ya sasa,sema tu Umeenda mbinguni uone watu watavyojikataaa,wataona ndio wale wale ila ukweli ni kwamba.

Si kila anaesema KAENDA MBINGUNI ni tapeli,Si kila anaesema Kaongea na MUNGU ni nabii wa uongo,Tupo katika DUNIA CHAFU iliyoharibika lakini bado MUNGU anawatu anawatumia,bado Mungu ana mawakili wake hapa duniani tena anao ongea nao DIRECT.

SODOMA NA GHOMORAH pamoja na uchafu wao wote lakni alikuepo LUTU, hata leo pamoja na maasi kuongezzeka kama ya SODOMA wapo vipanga wa MUNGU anao waaminia.

so tuache kubeza watumishi wa MUNGU.
 
Uko sahihi

WAEFESO 4:11-13
Naye alitoa wengine kuwa
mitume,
na wengine kuwa manabii;
na wengine kuwa wainjilisti
na wengine kuwa wachungaji
na waalimu;
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Mungu hana mipaka
Walio wa kweli tunawajua kwa sura na matendo yao!
Ila wengi ni matapeli na wahuni
 
Rudi kajifunze Ubatizo na maana yake
Halafu ujue pia Yesu hakufa, aliyekufa ni Kristo
Ukiuelewa ukristo utaelewa

Yesu ni Mungu
kwahiyo kulikuwa na Yesu na Kristo?
Kwa andiko lipi
Aliitwa Yesu Kristo ndo ninavyojua
 
Kwa kifupi tu ni kwamba dini zote ni Utapeli mtupu, ila Walokole ndio wamepotea zaidi.
Usiseme dini zote,ukisema dini zote utakua unakosea,ila changamoto zamaisha ndio zinachangia,tatizo hili limekua kubwa mno na waathirika wakubwa ni watu walioumia na kuchoka mioyo hususani wanawake.MUNGU ATUSAIDIE KWAKWELI
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaojiita Mitume, Manabii au Wachungaji ambao wamekuwa wakiwakonfyuzi watu hasa wale ambao si waumini wa Dini ya Kikristo.

Kitu kibaya zaidi hao Viongozi wa madhehebu hayo wamekuwa wakitumia Biblia kama njia ya kufanya huo utapeli wao ukaonekana ni ukweli, Watanzania wengi wamejikuta wananaswa kwenye mtego huo kwakuwa kama tujuavyo Watanzania na kusoma vitabu ni kama paka na panya.

Watu wengi kutokusoma Biblia ndiyo imekuwa mtaji mkubwa wa hao matapeli kwasababu wanafahamu hao wanaojiita Wakristo hawaielewi Biblia kwa ufasaha.

Biblia ni kitabu kilicho wazi kabisa kwa wafuasi wa Kristo na hakina mambo mengi kama watu wanavyodhani. Kwakuwa wafuasi wengi wanaojiita "Wakristo" hawapendi kuisoma ndipo hao matapeli wamejipatia huo mwanya wa kuwadanganya.

Neno "Wakristo" lilipatikana kwa mara ya kwanza pale kwenye Mji wa Antiokia, na hii ni baada ya wafuasi wa Yesu kukutana huko kwa muda wa mwaka mmoja na kuungana katika mambo ya kufundishana yale yote ambayo Yesu Kristo aliwafundisha kabla hajapaa.

Hii utaipata katika kitabu cha Matendo ya Mitume 11 : 26

Hivyo neno "Wakristo" kwa kifupi ni watu wanao muamini Yesu Kristo, kuiamini imani yake na yale aliyoyafundisha.

Maswali amabayo Nabii, Mtume au Mchungaji hawezi yajibu;

1. Ni wapi katika Biblia imesema watu wafunge hadi wafe ili waende mbinguni?

2. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka gari uende ukaombewe?

Msingi wa kupata gari ni kufanya kazi, na maandiko yako wazi. "Fanya kazi siku sita na siku ya saba pumzika. Mungu ataibariki kazi ya mikono yako."

3. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mchumba (mume/mke) upakwe maji au mafuta ya upako?

4. Ni wapi katika Biblia imesema ukiumwa UKIMWI uende kanisani uombewe UKIMWI uondoke?

Kupata UKIMWI ni matokeo ya dhambi, hivyo Mungu kwa uaminifu kabisa anaweza kukusamehe dhambi ila UKIMWI ukaendelea kuishi nao hadi unakuingiza kaburini.

Msipoielewa Biblia hakika mtafia dhambini.

5. Ni wapi katika Biblia imesema biashara yako ikiyumba ukachukue mafuta na maji ya upako uweke kwenye biashara yako?

Fanya biashara kwa uaminifu, fuata taratibu zote za kibiashara, mfanye Mungu awe wa kwanza katika biashara zako hakika utafanikiwa tu. Achaneni na hao matapeli watawaumiza sana tu.

6. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kumuona Mtume au Nabii ni lazima ulipe fedha?

7. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kuombewa na mtumishi wa Mungu ulipe fedha?

8. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mtoto ukapewe mafuta na maji ya upako utumie ili uzae?

Wakristo ni watu wa maandiko (scriptures), ukiona unaingia mkenge kwa hao wapiga ramli wanaojiita Manabii na Mitume tambua wewe si Mkristo bali ni muunga tela la wapagani.

Mtaibiwa na kutapeliwa sana, kibaya zaidi mtakoseshwa na uzima wa milele kwa madanganyo ya matapeli hao.
  • Kuhani Musa
  • Nabii Mashimo
  • Nabii Tito
  • Geor Davie
Hawa ni matapeli persay
 
Mtafute professor Lumumba wa Kenya U-tube kuhusu Bible, ilitumika katika kugandamiza Waafrika. "Ukristu ni ukoloni"
 
Mko bize na wachungaji na manabii ila Waganga na washirika wao mnawaruka .
Hawa ndio wanafanya uharibu Grade one Kila Kona na hamuwazingatii.
Hao Waganga Na Washirikina Ndiyo Siku Wamegeuka Manabii Na Mitume.

Pia Kuwa Makini Lisemwalo lipo.
 
Jamani kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake waacheni watu wale.....Wasipokuwepo waumini watafunga huduma zao lakini wanao wengi na kila siku wanaongezeka
Watu wengi hawataki kazi wala kufuata utaratibu wanataka miujiza
Mtu anapaka mafuta ya nabii sehemu za siri ili atakayemuingilia amuoe jamani....

INSTAGRAM @dollrubii_decors
Hatariii
 
Uko sahihi

WAEFESO 4:11-13
Naye alitoa wengine kuwa
mitume,
na wengine kuwa manabii;
na wengine kuwa wainjilisti
na wengine kuwa wachungaji
na waalimu;
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Mungu hana mipaka
Naam

Mathayo 24:11
Na watatokea manabii wengi wa uongo ambapo watapotosha watu.

Tuweni makini
 
Naam

Mathayo 24:11
Na watatokea manabii wengi wa uongo ambapo watapotosha watu.

Tuweni makini

Tumefundishwa jinsi ya kuwatambua

MATHAYO 7:15-20
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

Kumbukumbu La Torati 13:1-4

1. “Akitokea nabii au mtabiri wa ndoto miongoni mwenu, akawaahidi na kuwapa ishara au maajabu fulani,

2. halafu ishara au maajabu hayo yatokee, kisha aseme: ‘Tufuate miungu mingine na kuitumikia, (miungu ambayo hamjapata kuijua)’,

3. msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

4. Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
 
Barikiwa Sana.
 
Back
Top Bottom