Si kila Mchungaji, Nabii au Mtume anayetumia Biblia kufundisha ni Mkristo, wengine ni matapeli

Na si kila mchungaji/nabiii/mtumishi wa Mungu anaesema Kaenda Mbinguni Ni Tapeli/Mwizi

Kuna mindset nimeanza kuiona shetani anai iingiza kwa watu "indirect way" yani sasa hivi mtumishi

wa Mungu akisema kaongea na YESU katka MAONO watu wanaguna kimya kimya,akisema Ameonyeshwa Mbingu na yanayofanyika huko '"watu wanaguna kimya kimya"

Shetani ameshaanza kufanikiwa kuondoa TRUST ya wanadamu kwa watumishi wa MUNGU wa kweli,na katika hili shetani alitumia akili nyingi sana ili ku win hii game.

Aliingiza Manabiii FEKI,watumishi FEKI akawapa PROMO wakajulikana halafu akaanza wafanya wafanye vituko,kwasababu tumeshawajua ina maana chochote watachofanya tutakiona,wanafanya ujinga wa wazi na makusudi kabisa.. hiii ni TARGET ya shetani kukuondolea TRUST kwa watumishi halisi wa MUNGU.

Dunia ya sasa,sema tu Umeenda mbinguni uone watu watavyojikataaa,wataona ndio wale wale ila ukweli ni kwamba.

Si kila anaesema KAENDA MBINGUNI ni tapeli,Si kila anaesema Kaongea na MUNGU ni nabii wa uongo,Tupo katika DUNIA CHAFU iliyoharibika lakini bado MUNGU anawatu anawatumia,bado Mungu ana mawakili wake hapa duniani tena anao ongea nao DIRECT.

SODOMA NA GHOMORAH pamoja na uchafu wao wote lakni alikuepo LUTU, hata leo pamoja na maasi kuongezzeka kama ya SODOMA wapo vipanga wa MUNGU anao waaminia.

so tuache kubeza watumishi wa MUNGU.
 
Walio wa kweli tunawajua kwa sura na matendo yao!
Ila wengi ni matapeli na wahuni
 
Rudi kajifunze Ubatizo na maana yake
Halafu ujue pia Yesu hakufa, aliyekufa ni Kristo
Ukiuelewa ukristo utaelewa


Yesu ni Mungu
kwahiyo kulikuwa na Yesu na Kristo?
Kwa andiko lipi
Aliitwa Yesu Kristo ndo ninavyojua
 
Kwa kifupi tu ni kwamba dini zote ni Utapeli mtupu, ila Walokole ndio wamepotea zaidi.
Usiseme dini zote,ukisema dini zote utakua unakosea,ila changamoto zamaisha ndio zinachangia,tatizo hili limekua kubwa mno na waathirika wakubwa ni watu walioumia na kuchoka mioyo hususani wanawake.MUNGU ATUSAIDIE KWAKWELI
 
  • Kuhani Musa
  • Nabii Mashimo
  • Nabii Tito
  • Geor Davie
Hawa ni matapeli persay
 
Mtafute professor Lumumba wa Kenya U-tube kuhusu Bible, ilitumika katika kugandamiza Waafrika. "Ukristu ni ukoloni"
 
Mko bize na wachungaji na manabii ila Waganga na washirika wao mnawaruka .
Hawa ndio wanafanya uharibu Grade one Kila Kona na hamuwazingatii.
Hao Waganga Na Washirikina Ndiyo Siku Wamegeuka Manabii Na Mitume.

Pia Kuwa Makini Lisemwalo lipo.
 
Hatariii
 
Naam


Mathayo 24:11
Na watatokea manabii wengi wa uongo ambapo watapotosha watu.



Tuweni makini
 
Naam


Mathayo 24:11
Na watatokea manabii wengi wa uongo ambapo watapotosha watu.



Tuweni makini

Tumefundishwa jinsi ya kuwatambua

MATHAYO 7:15-20
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.


Kumbukumbu La Torati 13:1-4

1. “Akitokea nabii au mtabiri wa ndoto miongoni mwenu, akawaahidi na kuwapa ishara au maajabu fulani,

2. halafu ishara au maajabu hayo yatokee, kisha aseme: ‘Tufuate miungu mingine na kuitumikia, (miungu ambayo hamjapata kuijua)’,

3. msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

4. Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
 
Barikiwa Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…