Nadhani mtoa mada hajaspecify kuwa iyo sheria niya nchi gani.
Hiyo ni Sheria ya Marekani, na kwa international flights, yaani ukitaka au kuingia US, hutakiwi kuingia na kiwango kinachozidi USD 10K, na ukitaka kufanya hivyo, kuna fomu maalumu unatakiwa kujaza fomu ( FinCEN Form 105).
Hata hivyo, kiwango kama hicho kimekuwa adopted na nchi nyingi duniani, including Tanzania.
NB: Kwa ndani hakuna limit lakini ukienda benki (Tanzania) na kutaka kuchukua pesa nyingi, sheria butu inakutaka utoe taarifa polisi ili upewe escort(unalipia) !
Sina hakika kama kiwango kimebadilishwa manake kwa muda mrefu kilikuwa ni kiwango kilichowekwa enzi za Nyerere ambacho, kwa mujibu wa kiwango kile, basi 99.9% ya wananchi wanaoenda benki walitakiwa kwenda na polisi!
ANGALIZO: Kwa wafanyakazi wa serikali kama vile Cashiers na wale wa Bank, kama vile Supervisor or Bank Tellers wanatakiwa kuizingatia sana hiyo sheria.
Ikitokea government officials umeenda benki na kuchukua mpunga, kisha ukaporwa na majambazi, uchunguzi utaanza kwa kuangalia ikiwa ulienda benki na police escort!
Aidha, aliye-authorize cheque pale benki pamoja na Bank Teller aliyelipa, wanaweza kujikuta matatani kama walilipa cheque bila kuwa endorsed na police kuonesha kwamba kuna escort!