Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake


Kwanza, shukrani kwa bandiko. Nimefanya 'editing' ya points ili niweze kuzichangia nikiziwekea namba mwanzoni

Hoja #1: Waasisi wa muungano waifanya kwa 'mazoea' hawakuzingatia athari za muda mrefu.
Mambo yasiyo ya Muungano yanajulikana na inapaswa yakijadiliwa Bungeni Wazanzibar waondoke.
Ukiwaacha Wazanzibar wajadili yasiyo ya Muungano, yanakuwa ya Muungano na si ya Tanganyika tena.

Hoja# 2: Mafuta na gesi si ya Muungano, Zanzibar waliondoa. '' Disavantage' ni kwa Tanganyika kwasababu mapato yatokanayo na rasilimali kama gesi yanakwenda ZanzibarGBS. 2024/25 SMZ inapewa Bilioni takribani 500 utoka rasilimali za Tanganyika. Mambo ya Tanganyika yanakuwa ya Muungano ! ni dhulma

Hoja#3: Nyerere-Rais, Karume Makamu wa kwanza , Kawawa akawa Makamu wa pili. kwa kujua Rais wa Tanzania ni wa Tanganyika na lazima atoke Tanganyika. Katiba ya 1977 na ile ya 1984 zikavuruga, Rais wa SMZ ni mjumbe wa 'Cabinet' akjadili 98% ya mambo ya Tanganyika

Hoja#4: Nakubaliana,waliobadilisha muundo wa Rais, Makamu wa Kwanza na wa Pili walileta tatizo.
System ilikuwa kwanba Rais wa Zanzibar ni Makamu, Rais wa JMT akifariki Makamu wa pili ataendesha ya Tanganyika, Makamu wa Kwanza ataendesha ya Zanzibar wakusubiri uchaguzi wa Rais wa JMT.

Tangu Mwinyi mfumo ulikuwa Rais wa JMT atoke bara kwasababu anashughulikia 98% ya Bara.
Kwa bahati mbaya haikuwa documented ndio maana tunaye Rais wa JMT Mzanzibar , Rais wa SMZ Mzanzibar.
Hakuna Msimamizi wa mambo ya Tanganyika katika ''fairness''.
Tumeona kero zinavyomalizwa kwa kasi kwa upande mmoja kuzijadili, SSH na Mwinyi, hakuna Mwakilishi wa Tanganyika.

Hoja#5: Naafiki

Hoja#6: Kuna mantiki kubwa sana! kila anachokifanya kinakosa 'imani' kwasababu Watanganyika wanahisi hakuna msimamizi wa nchi yao au rasilimali zao. Kwa bahati mbaya sana Rais SSH ame prove mwenyewe hisia hizo kwa suala la DP kwa kuiondoa Zanzibar na mambo mengi akiitenga Zanzibar hata taasisi kama za mafuta na gesi.
 
Mlolongo mrefuuuuuuu wa malalamiko, si muiache tu Zanzibar? Kwanini mnain'gang'ania sasa?

Oooohhh mlidhani mtawanyonya? Sasa wanakunyonyeni nyie sasa ndio mjue hawataki jimuungano lenu, warudishieni inchi yao
Full stop
 
Hivi haya mambo hao walioko huko juu hawayaoni?
 
Mlolongo mrefuuuuuuu wa malalamiko, si muiache tu Zanzibar? Kwanini mnain'gang'ania sasa?

Oooohhh mlidhani mtawanyonya? Sasa wanakunyonyeni nyie sasa ndio mjue hawataki jimuungano lenu, warudishieni inchi yao
Full stop
Utanyonya nini kutoka kwenye jiwe?
 
Hivi haya mambo hao walioko huko juu hawayaoni?
Mambo haya wanayaona na wanayajua sana tena wengine wakiyatekeleza

Makamu wa Rais si ndiye anaongoza vikao vya kero za Wazanzibar!

Waziri Mkuu si ndiye msimamizi wa shughuli za serikali bungeni! ulisikia chochote wakati Wazanzibar wanaukana Utanzania. PM alikuwa kimyaaa ! angesEMA Mbowe sasa!!!

Spika , Wazanzibar wakiukana Utanzania alikuwepo! ulimsikia akisema jambo. Mbowe angesema sasa!

Waziri wa Fedha , ndiye anagawa pesa na mafungu ya kumaliza kero za Zanzibar

Waziri wa Muungano, yeye anashughulikia kumaliza kero za Zanzibar

Orodha inaendelea, wanaogopa vyeo vyao kuliko Mama Tanganyika! Ipo siku tutarudisha rekodi
 
Mlolongo mrefuuuuuuu wa malalamiko, si muiache tu Zanzibar? Kwanini mnain'gang'ania sasa?
Hakuna malalamiko, kuna facts. Hakuna anayeishikilia isipokuwa CCM
Ukitaka kujua hakuna anayeishikilia Zanzibar, jibu swali hili. Bila Zanzibar, Tanganyika ina kipi cha kupoteza?
Oooohhh mlidhani mtawanyonya? Sasa wanakunyonyeni nyie sasa ndio mjue hawataki jimuungano lenu, warudishieni inchi yao
Full stop
Wao warudishe nchi yao
1. SMZ ipeleke mswada BLW kama ule uliobadilisha katiba. Wajadili halafu wabadili katiba , hakuna wa kuwazuia.
2010 hawakuzuiliwa, sidhani kama kuna atakayewazuia

2. Wabunge wa Zanzibar watumie 2/3 kupeleka mswanda Dodoma. Tena sasa ni rahisi zaidi Rais ni Mzanzibar

3. Wakishindwa yote mawili, kuna njia nyingine. Wabunge kutoka Zanzibar wasije Dodoma. Mawaziri na Watendaji kutoka Zanzibar waondoke Tanganyika. Wazanzibar wawaunge mkono warudi kuijenga Zanzibar, muungano utakuwa umefika hatma.

Mtanganyika hawezi kufanya lolote , hana chombo chochote! hana Serikali wala Bunge la Tanganyika
 
Wakati watu wanalilia katiba, nyie mlikuwa mnacheza amapiano. Katiba inamruhusu, ningepata nafasi namimi, ningemega sehemu ndogo niuze
 
Mbali na kuwa katiba imempa mamlaka makubwa mtawala, kufanya maamuzi ambayo anafanya ni jambo ambalo linaashiria upeo mdg wa akili.
 
Mbali na kuwa katiba imempa mamlaka makubwa mtawala, kufanya maamuzi ambayo anafanya ni jambo ambalo linaashiria upeo mdg wa akili.
Tunapaswa kuiona nafasi ya uraisi kama nafasi ambayo imetangazwa kwa ajili ya watu ku-apply wakiwa na qualifications kujaza nafasi hiyo, kama ambavyo tungetangaza nafasi ya kazi ya Director General wa kampuni fulani. Sifa au umaarufu au ushabiki tu wa kisiasa, mara nyingine bila hata elimu ya mambo ya uongozi, sheria au uchumi, zitaendelea kutupa maraisi wasio na uwezo katika nafasi hii na kututia katika janga la maamuzi yasiyofaa, yakiwa na athari za muda mrefu kwa taifa hili.
 
Jamaa wana mafuta na gesi ya kufa mtu,
Wapeni tu uhuru wao muone kama hamtasaidiwa na wao
Story ya mafuta Zanzibar ni ya muda mrefu sana. Kama tayari wameshayatoa mafuta kwenye muungano, kwa nini hadi leo hatusikii wakiyachimba? Si wawaite wajomba zao wawachimbie, badala ya kuwaita wajomba zao kuja bara kutuharibia rasilimali zetu.
 
Uongo mkubwa sana huu.

Suluhisho sahihi ni kupatikana kwa Katiba ya nchi ambayo ni nzuri. Katiba itakayoweka misingi imara ya kuwepo kwa Serikali moja ya kidemokrasia ambayo inawajibika kwa Wananchi, na wala siyo vinginevyo.
Sijui kwanini watanganyika wengi hawataki serekali yao wapo tu kuishikilia zanzibar
 
Sijui kwanini watanganyika wengi hawataki serekali yao wapo tu kuishikilia zanzibar
Tatizo lililopo Tanzania wala siyo suala la idadi ya Serikali tunazopaswa kuwa nazo, bali tatizo lililopo ni kwamba Serikali zote kabisa zilizopo:-
1. Ni Serikali za Kidikteta, Siyo Serikali za Kidemokrasia.
2. Serikali zilizopo Haziwajibiki kwa Wananchi wa nchi husika.

Hivyo basi, hata Tanzania iwe na Serikali zipatazo tatu, nne au zaidi ya hizo lakini kama Serikali hizo zitakosa sifa hizi mbili nilizotaja hapa juu ni sawa na kazi bure(work done equal to zero).
 
Naombeni site ya kudownload full movie free za makampuni ya movie kama universal pictures
 
Je hiyo moja kwa mawazo yako wewe ndio itakuwa na usawa au kuzidisha udikteta kwa upande wa zanzibar kufuta utambulisho wao kutimiza lengo lilowekwa
 
Story ya mafuta Zanzibar ni ya muda mrefu sana. Kama tayari wameshayatoa mafuta kwenye muungano, kwa nini hadi leo hatusikii wakiyachimba? Si wawaite wajomba zao wawachimbie, badala ya kuwaita wajomba zao kuja bara kutuharibia rasilimali zetu.
Bado hamjawaruhusu.
Hakuna kitu kama uhuru na uamuzi
Narudia tena kwa mara ya mwisho waacheni inchi yao
 
Hakuna malalamiko, kuna facts. Hakuna anayeishikilia isipokuwa CCM
Ukitaka kujua hakuna anayeishikilia Zanzibar, jibu swali hili. Bila Zanzibar, Tanganyika ina kipi cha kupoteza
Kwa hiyo ccm ipo kenya, kama haina cha kupoteza kwanini mawalazimishia muungano? Sasa ya nini mlolongo wooote huo

Si ni Tanganyika tu wawaachoe inchi yao?
Kwanini mnalazimisha?
Kwani ccm ipo kenya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…