Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
1. Mambo ya muungano yanajulikana, na japo Tanzania bara haina serikali yake, mambo yaliyofanywa kuwa ya Zanzibar yanafanya mambo yale yale yakiwa kwenye muungano yasiwe tena ya muungano bali ya Tanzania bara.
2. Huwezi kusema mafuta yaliyoko Zanzibar ni suala la Zanzibar, na mafuta yaliyoko bara ni ya muungano. Ukishafanya mafuta yaliyoko visiwani ni ya Zanzibar, inference ni kwamba mafuta yaliyoko bara hayapaswi tena kuonwa kama ni mafuta ya muungano.
3. iwe imeandikwa kwenye katiba au la, mteule wa kugombea uraisi wa Tanzania siku zote atatoka bara, na mgombea mwenza Zanzibar, ni kutambua raisi wa Tanzania ni raisi wa Tanzania Bara, 2% ya mambo yataihusu Zanzibar, na sana sana ni mambo ya nchi za nje.
4. Katika mpangilio huu, hawakuona mbali na walisahau kusema raisi akifa makamu wa raisi hapaswi kuwa raisi kwa sababu siku zote makamu wa raisi wa kupigiwa kura atakuwa ni kutoka Tanzania bara, na akiwa raisi wa Tanzania ndio atakuwa raisi wa Tanzania bara, bila serikali ya Tanzania bara kuwapo rasmi. Raisi akifa na makamu wa Raisi toka Zanzibar akawa raisi basi awe acting president kwa maximum mwaka mmoja tu ili ndani ya muda huo uchaguzi mpya wa raisi ufanyike kisha arudie kuwa makamu wa raisi.
5. Theoretically, ukitaka kusawazisha hali iliyopo, ya Samia kuwa raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar, inabidi mtu kutoka bara aende akawe raisi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar. Tumpeleke Mwigulu akawe raisi kule, mweupe kama wao.
6. Ndio maana nikasema, kwa kuwa Samia anatoka Zanzibar kutokana na jambo lisilotazamiwa, ni busara asifanye maamuzi makubwa ya bara yenye long term lock-in effect, na kusubiri hadi raisi kutoka bara akiwa madarakani ndio afanye hayo maamuzi.
Kwanza, shukrani kwa bandiko. Nimefanya 'editing' ya points ili niweze kuzichangia nikiziwekea namba mwanzoni
Hoja #1: Waasisi wa muungano waifanya kwa 'mazoea' hawakuzingatia athari za muda mrefu.
Mambo yasiyo ya Muungano yanajulikana na inapaswa yakijadiliwa Bungeni Wazanzibar waondoke.
Ukiwaacha Wazanzibar wajadili yasiyo ya Muungano, yanakuwa ya Muungano na si ya Tanganyika tena.
Hoja# 2: Mafuta na gesi si ya Muungano, Zanzibar waliondoa. '' Disavantage' ni kwa Tanganyika kwasababu mapato yatokanayo na rasilimali kama gesi yanakwenda ZanzibarGBS. 2024/25 SMZ inapewa Bilioni takribani 500 utoka rasilimali za Tanganyika. Mambo ya Tanganyika yanakuwa ya Muungano ! ni dhulma
Hoja#3: Nyerere-Rais, Karume Makamu wa kwanza , Kawawa akawa Makamu wa pili. kwa kujua Rais wa Tanzania ni wa Tanganyika na lazima atoke Tanganyika. Katiba ya 1977 na ile ya 1984 zikavuruga, Rais wa SMZ ni mjumbe wa 'Cabinet' akjadili 98% ya mambo ya Tanganyika
Hoja#4: Nakubaliana,waliobadilisha muundo wa Rais, Makamu wa Kwanza na wa Pili walileta tatizo.
System ilikuwa kwanba Rais wa Zanzibar ni Makamu, Rais wa JMT akifariki Makamu wa pili ataendesha ya Tanganyika, Makamu wa Kwanza ataendesha ya Zanzibar wakusubiri uchaguzi wa Rais wa JMT.
Tangu Mwinyi mfumo ulikuwa Rais wa JMT atoke bara kwasababu anashughulikia 98% ya Bara.
Kwa bahati mbaya haikuwa documented ndio maana tunaye Rais wa JMT Mzanzibar , Rais wa SMZ Mzanzibar.
Hakuna Msimamizi wa mambo ya Tanganyika katika ''fairness''.
Tumeona kero zinavyomalizwa kwa kasi kwa upande mmoja kuzijadili, SSH na Mwinyi, hakuna Mwakilishi wa Tanganyika.
Hoja#5: Naafiki
Hoja#6: Kuna mantiki kubwa sana! kila anachokifanya kinakosa 'imani' kwasababu Watanganyika wanahisi hakuna msimamizi wa nchi yao au rasilimali zao. Kwa bahati mbaya sana Rais SSH ame prove mwenyewe hisia hizo kwa suala la DP kwa kuiondoa Zanzibar na mambo mengi akiitenga Zanzibar hata taasisi kama za mafuta na gesi.