Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Watu wengi wamekuwa wakivitazama vyama vya upinzani katika mtazamo wa kuwa mbadala wa CCM katika uongozi, na wengi wanasema kwamba bado havijakomaa kuongoza nchi, jambo ambalo siku zote nasema, tulipopata uhuru TANU haikuwa imekomaa kuongoza nchi.
Sasa mimi naona kama imefikia mahali jeshi la Polisi halijui wajibu wao na wamefikia mahali wanakubali kuendeshwa na wanasiasa wa CCM kama ng'ombe anaevutwa kwa kutumia pete ya puani. Nadhani ni wakati muafaka kwa Watanzania kudhamiria kuwaondoa CCM madarakani, si kwa sababu labda chama fulani cha siasa ni mbadala mzuri, bali kwa ajili ya "to teach the Police force and other security organs in the country a lesson" katika kutambua wajibu wao na kuutekeleza nje ya ulingo wa kisiasa.
Na itafurahisha sana kama CCM wakielewa kwamba walitolewa madarakani kwa sababu za kulifanya jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kama watumishi wao binafsi, na sio watumshi wa umma wa Watanzania