Uchaguzi 2020 Si Magufuli, si Humphrey Polepole waliojaribu hata ku-tweet kushukuru wapiga kura au kusherehekea ushindi mpaka sasa

Uchaguzi 2020 Si Magufuli, si Humphrey Polepole waliojaribu hata ku-tweet kushukuru wapiga kura au kusherehekea ushindi mpaka sasa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kama nilivyosema katika uzi wangu wa asubuhi ya leo,mpaka muda huu viongozi hawa wako kimya kabisa licha ya Magufuli kutangazwa mshindi wa kitu cha urais.

Inawezekana chama kinajiandaa kutoa tamko rasmi wakati wowote ule, ila bado nilitarajia kutokana na furaha ya ushindi, mmoja wa viongozi hawa angeshasema lolote kupitia mitandao na hasa mtandao wa Twitter kuhusu ushindi huu wa asilimia zaidi ya 80 ila cha ajabu wako kimya kabisa.

Ni vijana wao wa mitandaoni tu wakiwemo kina Pascal Mayalla ndio wanaojikakamua kusherekea na kusifu na kukejeli wapinzani ila wenye chama mpaka sasa kimya utadhani wao ndio wametangazwa kushindwa.

Anyway,labda nao wao hawana access na internet ndio maana wako kimya.

All in all, hii ni dalili kuwa hata wenyewe hawana raha na matokeo haya na huenda hawakutarajia mambo yangeenda yalivyoenda.

Tunawasubiri mjikaze kutoa taarifa ya ushindi na kupongezana.Nasubiri tweet ya Mwenyekiti (Mgombea)na Polepole.
 
Hii ni tweet ya account rasmi ya CCM. Account ambayo ipo verified. Au mwenzetu una makengeza?

Screenshot_20201031_144143.jpg


 
Kwani hujui kuwa mitandao imefugwa? Subiri kesho baada ya kukabidhiwa rasmi cheti cha ushindi na NEC.
 
Wataweza kweli,.kushindana nasi..
Polepole ameonyesha ujemedar wa Hali ya juu katika nafasi yake ya ukatibu mwenezi..
Kuunga mkono juhudi ndio kumeiangusha cdm na cuf
 
Labda na wao hawana VPN, maana inaneti imezimwa kwa muda wa zaido ya siku 3 sasa
 
Back
Top Bottom