Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

k̫u̫n̫a̫ u̫w̫e̫z̫e̫k̫a̫n̫o̫ w̫a̫t̫a̫k̫a̫o̫a̫n̫d̫a̫m̫a̫n̫a̫ n̫i̫ p̫o̫l̫i̫s̫i̫.....w̫a̫m̫e̫j̫i̫p̫a̫n̫g̫a̫ k̫w̫e̫l̫i̫ k̫w̫e̫l̫i̫.
 
The greatest fear is when you fear the unknown.
Akihutubia hiyo tarehe 31 basi ujue anawaogopa ye awaache tu aone kama wataandamana.
Ila pia polisi wamechoka mwezi mzima mazoezi ya kumkabili usiemjua inasikitisha sana!!!
Huku toka asubuhi wanafyatua mabomu ya machoz sijui ndo mazoez yenyewe, hii hali inanikumbusha enzi za mtikila, wakati anabebwa na walala hoi huku serikali haitaki abebwe mpaka nyerere alipoingilia kati na akasema mwacheni anayetaka kubebwa kama jeneza na abebwe, hapo polosi wakaacha kumzingira cha ajabu baada ya hapo hakuna aliyejitokeza kumbeba mtikila mpaka umaarufu wake ukapotea hadi mauti yanamkuta hakuwa na umaaru wa kutishia serikali.
 
Sasa ninyi UKAWA si huwa mnajifananisha na yaliyotokea uarabuni? Andamaneni sasa maana huko Misri waliandamana mbela ya vifaru vya jeshi! Sasa itakuwa aibu yenu mkikimbia defenda za polisi!
 
Nasikia CHADEMA wamepanga kuairisha kimya kimya ili police wahenye kutafuta hewa
 
Habari nilizopata kutoka jikoni zinasema kuwa siku ya August 31 mwaka huu, siku moja kabla ya UKUTA rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kutangaza mambo mazito kwa watanzania.

Inasemekana kuwa rais anatarajiwa kuliweka jeshi la polisi katika tahadhari kubwa huku kukiwa na mazuio kadhaa yatakayo ambatana na tahadhari hiyo kwa jeshi la polisi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kunatarajiwa kuwa na operesheni nzito ya jeshi la polisi na huenda kukatumika nguvu kubwa zaidi katika kukabiliana na Chadema nchi nzima.

Aidha nimedokezwa kuwa ofisi zote za Chadema nchini zinatarajiwa kuzingirwa na jeshi la polisi siku hiyo ya september moja.

#UKUTA for Democracy!
Kuna solution moja pekee katika sintofahamu ya sasa hivi ni kwa Mkuu mwenyewe wa nchi kurealize kuwa siku alipotangaza kuwapa 'likizo' ya lazima vyama vya siasa vya upinzani hadi mwaka 2020, akiri kuwa ulimi uliteleza na aviruhusu vyama vyote vya siasa vifanye shughuli zao za siasa kwa mujibu wa Katiba ya nchi na Sheria ya vyama vya siasa.

Kinyume cha hapo kama siku hiyo atakuja na 'story' zake kuwa yeye hajaribiwi....... Na akaamua kupiga mikwara kuwa ataviamuru vyombo vyake vya dola 'anavyovimiliki' kuwashughulikia raia wema anaowaita kuwa wanaleta fyoko fyoko.........

Hakika atakuwa ameamua kuitumbukiza nchi hii kwenye machafuko........
 
Uongo mwingine wa dikteta uchwara huu hapa.

Odinga afichua aliyoteta na JPM





Raila Odinga

Na Ratifa Baranyikwa,

MWANASIASA maarufu nchini Kenya, Raila Odinga, amesema amemuuliza Rais John Magufuli kuhusu hatua yake ya kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Odinga ambaye anaongoza muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (CORD), alisema tofauti na maelezo anayoyasikia nje, katika mazungumzo yao Rais Magufuli alimwambia hajapiga marufuku mikutano ya kisiasa ikiwemo ile ya wanasiasa au viongozi wa juu wa kitaifa wa vyama vya siasa wasio na majimbo.

Alisema badala yake alimwambia amepiga marufuku mikutano ya kubeba watu kwenye mabasi kutoka eneo moja kwenda jingine kwa madhumuni ya kufanya vurugu.


Odinga aliyekuwa nchini kwa shughuli binafsi, yeye na familia yake, aliyasema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika Hoteli ya Hyat Dar es Salaam na wahariri wa magazeti ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.

Katika mahojiano hayo yaliyoanza kuchapishwa wiki hii na gazeti dada la MTANZANIA JUMAPILI la RAI, Odinga pia alizungumzia mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hatua ya wabunge wa upinzani kususia vikao vyake, lakini pia uamuzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kujiunga upinzani na kisha kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Odinga anayetambulika kama baba wa demokrasia katika siasa za Afrika Mashariki, alilazimika kufichua siri ya mazungumzo baina yake na Rais Magufuli baada ya wahariri kutaka kujua kama alikutana na rafiki yake huyo na kuzungumzia joto la siasa za hapa nchini.

Katika majibu yake kuhusiana na swali hilo, Waziri Mkuu huyo wa zamani nchini Kenya, alikiri kukutana na Rais Magufuli Jumapili ya Agosti 14 mwaka huu Ikulu, Dar es Salaam na kula naye chakula cha jioni kisha kuzungumza mambo yao ya kirafiki na yale ya kisiasa lakini yasiyohusu urais.

“Jana mimi nimeongea na Rais yeye ameniclaim tofauti okey…amesema hajawanyamazisha wasiongee, anasema wanataka kufanya maandamano katika jimbo zile zingine ambazo hawana watu na kutaka kubeba watu kwa mabasi yeye alisema wakitaka hivyo wafanye kwao na si kubeba watu kutoka eneo hili kwenda eneo lingine, sasa sijui ukweli mimi maana mimi si Mtanzania.

“Anasema hajawakataza kama wakifanya eneo lao wanaweza kufanya lakini kubeba watu kutoka jimbo hili kwenda jimbo hili na mabasi kwenda kuleta vurugu ndio anasema amekataa,” alisema.

Alipoulizwa kama pengine Rais Magufuli amemweleza msimamo wake wa kupiga marufuku siasa za ushindani hadi mwaka 2020 pia ulilenga kuwazuia viongozi wakiwemo wale wa juu wa kitaifa wa vyama vya upinzani wasio na majimbo, Odinga alisema huku akimalizia na kicheko;

“Anasema hajakataa.”


Akisisitiza kile alichoelezwa na Rais Magufuli ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi, Odinga alizungumzia uhuru wa kutoa maoni akisema wapinzani kazi yao ni kupinga na si kushangilia na kwamba hiyo ndiyo demokrasia.

Alisema kutokana na kile alichomweleza Rais Magufuli, hadhani kama alikuwa na madhumuni ya kuwanyamazisha wapinzani.

Awali wakati akijibu swali hilo, Odinga ambaye miezi mitatu iliyopita alikuja nchini na kukutana na Rais Magufuli nyumbani kwake Chato, ziara ambayo ilizua gumzo hapa nchini na Kenya, alianza kwa kusifu kazi iliyofanywa na kiongozi huyo ya kusafisha hekalu lake pindi tu alipoingia madarakani Novemba mwaka jana.

“Kwanza nimshukuru sana Rais Magufuli kwa yale aliyofanya, tangu ashike hatamu ya utawala Tanzania kuna maendeleo mengi ambayo yamefanyika kwa mfano ile vita dhidi ya ufisadi, uzembe na kuleta nidhamu kwa upande wa kutoa huduma kwa wananchi.

“Sasa waliolala usiwaamshe (kicheko), lakini mimi sioni kama kuna shida kubwa, kama upande huo wapinzani wanatafuta relevance sasa kwa hivyo nilikuwa sitaki kujiingiza katika mambo ya ndani ya Tanzania,” alisema.

Wakati haya yakitokea sasa kwa takribani miezi mitano kumekuwa na vita baridi ya kisiasa kati ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Msingi wa vita yenyewe ni madai yanayotolewa na Ukawa, hususani Chadema kwamba Taifa limeporwa haki na demokrasia na Serikali inayotawala.

Kutokana na hilo hivi karibuni Chadema walitangaza kufanya mikutano na maandamano nchi nzima ifikapo Septemba mosi mwaka huu kupitia operesheni waliyoibatiza jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Hatua hiyo ya Chadema ilionekana wazi kumkera Rais Magufuli ambaye akiwa katika ziara ya chama chake mkoani Singida takribani wiki mbili zilizopita alikaririwa akisema yeye si mtu wa kujaribiwa na kwamba mwanasiasa atakayeandamana kinyume na maagizo yake atakiona cha mtema kuni.

Rais Magufuli alisema mtu pekee anayeweza kupita kila mahali ni yeye peke yake kwa sababu ni rais huku pia akiruhusu mikutano kwa wabunge wenye majimbo tu.

Juni mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kupiga marufuku mikutano ya siasa za ushindani hadi mwaka 2020, akiwataka watu kufanya kazi.

Odinga afichua aliyoteta na JPM

SOURCE: Mtanzania
 
Kwa hiyo tarehe hiyo ndiyo tutaanza kujua kama huyu ni malaika au shetani
 
Mi.i naogopa hapa kusije kukawa na mchezo wa paka na na panya ikawa jeshi na serekali wanajiandaa akafu na hawa wengine wanaahirisha wanapeleka mbele halafu tukawa kwenye tension kwa muda mrefu .na tukashi dwa kufanya kazi
 
Habari nilizopata kutoka jikoni zinasema kuwa siku ya August 31 mwaka huu, siku moja kabla ya UKUTA rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kutangaza mambo mazito kwa watanzania.

Inasemekana kuwa rais anatarajiwa kuliweka jeshi la polisi katika tahadhari kubwa huku kukiwa na mazuio kadhaa yatakayo ambatana na tahadhari hiyo kwa jeshi la polisi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kunatarajiwa kuwa na operesheni nzito ya jeshi la polisi na huenda kukatumika nguvu kubwa zaidi katika kukabiliana na Chadema nchi nzima.

Aidha nimedokezwa kuwa ofisi zote za Chadema nchini zinatarajiwa kuzingirwa na jeshi la polisi siku hiyo ya september moja.

#UKUTA for Democracy!
Hivi Chadema wana ofisi kweli za kuzingirwa na polisi? Pale Ufipa polisi wawili tu wanatosha ofisi ina vyumba vitatu.
 
Magufuli might be getting the UKUTA thing wrong. Simply let them go ahead. Whatever the support CDM will get, there is no doubt the numbers will keep dwindling every time they organize UKUTA sessions. By 2020, it will have become irrelevant!
 
Hatari sana ingekuwa Mzee Mwinyi ndio Rais angesema ndugu zanguni andamaneni ni ruksa hii nchi yetu sote ....ila JPM Wallah atawaumiza though hawa jamaa wabishi...
 
The greatest fear is when you fear the unknown.
Akihutubia hiyo tarehe 31 basi ujue anawaogopa ye awaache tu aone kama wataandamana.
Ila pia polisi wamechoka mwezi mzima mazoezi ya kumkabili usiemjua inasikitisha sana!!!
halafu watu hawajui tu.....mazingira kama haya yule adui wa tatu (eg Al Shabab) ndimo anamoweza kujipenyeza na kufanya vitu vyake.

ningekuwa mimi niko karibu na JPM ningemshauri asi-gamble na "unknown".

yeye angeacha maandamano yafanyike ila patakapofanyika fujo aweke kibano... huku kuminyanaminyana huku nina wasiwasi mambo kama ya Nigeria au Middle East yanaweza kutokea huku pia.
 
Hili linahitaji busara zaidi mkulu si vinginevyo! Onyesha utu wako ruhusu mikutano ya kisiasa iendelee, TUTAPONA!
Si mrahisi kiivyo. Kwanza mahojiano hawezi. Na anaona akiwaruhusu atakuwa kama kashindwa vile.. Criminal minded
 
Back
Top Bottom