Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Inaonekana wengi wamekasirishwa au kufedheheshwa sana na kitendo cha Makonda kuwaita Mbowe mwanasiasa uchwara na Zitto mshirikina. Sioni kama hili ni tatizo.
Alichofanya Makonda ni kuweka utangulizi au precedent ya aina ya mipasho ya kisiasa unayoweza kufanya kwa kiongozi wa chama cha siasa. Kwa kuwa sio tatizo kwa Makonda kufanya hivyo, sio tatizo kwa viongozi wa vyama vya upinzani kufanya hivyo hivyo kwa Magufuli kama kiongozi wa chama cha siasa.
Ila jambo moja la kukumbuka ni kwamba, Makonda amewaita Mbowe na Zitto mwanasiasa uchwara na mshirikina katika wadhifa wao wa kuwa viongozi wa vyama, jambo ambalo Magufuli pia ana wadhifa huo.
Hivyo basi vyama vya upinzani visitumie mpasho huo katika background ya Magufuli kama raisi wa nchi; yaani huwezi kusema raisi Magufuli ni mwanasiasa uchwara au mshirikina, lakini haitakuwa tatizo ukisema mwenyekiti wa CCM Magufuli ni mwanasiasa uchwara au mshirikina.
Na kama hii ni precedent isiyokubalika, basi na tuone Magufuli au Polisi au msajiri wa vyama vya siasa wakichukua hatua dhidi ya Makonda au hata kumkemea hadharani.
La sivyo ni mpasho unaokubalika kwa viongozi wa vyama vya siasa, awe Mbowe, Zitto au Magufuli. Ni mipasho ya kisiasa tunaishuhudia hata Marekani au Afrika Kusini.