Si tuliambiwa GSM ataishia kwenye mabango? Imekuwaje tena nembo yake iwe kwenye jezi za Simba?

Si tuliambiwa GSM ataishia kwenye mabango? Imekuwaje tena nembo yake iwe kwenye jezi za Simba?

Sasa kama team yenyewe inayotakiwa kuvaa hizo jersey hakushirikishwa katika hayo makubaliano kupitia BODI YA LIGI , inategemea kusitokee mgongano? Kama zitaishia kwenye mabango hapo ni sawa, lakini kama SIMBA SC itatakiwa kuvaa hiyo nembo basi haikuwa sahihi wao kutoshirikishwa kupitia wawakilishi wao ambao ni Bodi ya LIGI.
Kisheria bodi ya ligi/tff ndio wasimamizi wa mpira wa nchi hii, na mikataba yote hususani inayohusiana na udhamini wa ligi nzima , wao ndio wanaingia.Kwani huo udhamini wa azamu, Nbc bank, mbona hawakuhusishwa?na hata huko nyuma toka enzi za vodacom, tbl hawakuwahi kuhusishwa, na ndio maana huwa suala la logo huwa linaleta utata mala tu mdhamini anapokuwa ametangazwa?
 
Mbona simple tu MO na Vunja bei wapeleke ombi TFF la kudhamini ligi kuu.Ili Yanga nao wavae nembo original ya MO na Vunja bei.Niutani tu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo CEO angeachana na hizo mambo, hiyo sio asili yetu wala asifikirie kwamba sisi mashabiki tuna noma na hiyo logo
Safi kabisa wewe unafaa kuwa kwenye management ya makolo
 
- Klabu ya Simba imekataa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM)

- CEO wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amesema wameandika barua bodi ya ligi kuomba ufafanuzi baada ya kuambiwa kuanzia mchezo ujao wanapaswa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM)

- Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu Tanzania bara 🇹🇿, ukikataa kuvaa logo ya mdhamini unapigwa faini ya Tsh milioni 3 kwa mechi.

- Ukiendelea kukaidi, unashushwa daraja.

- Mkataba waliosaini GSM na TFF masharti yaliyopo kutoka GSM ni kuwa, logo yao inapaswa kukaa upande wa kushoto wa jezi.

- Tayari Simba SC walishapewa logo hizo na mamlaka za soka nchini wazitumie kuanzia mchezo unaofuata wa derby ya Kariakoo.
Tupia kapicha basi muzee.
 
Hayo Sasa Ni masuala ya kimkataba Baina ya hao GSM na waendeshaji wa ligi husika. Ninachopinga Ni kusema GSM Ni Yanga sc

Nani kakwambia hapa Yanga imehusishwa? Mbona wewe ndiyo unaonekana kuongozwa na mihemuko,umeona tu Simba wamepinga,ukaja na sababu zako kichwani kuwa Sababu GSM ni Yanga,tuonyeshe sehemu CEO wa Simba kaihusisha Yanga katika sababu alizozitoa
 
Hahaha...

Makolo si nao wamwambie Mudi aweke mpunga ili Utopolo nao wavae jezi zenye yale makolo ya Mudi...
 
Back
Top Bottom