Si tuliambiwa GSM ataishia kwenye mabango? Imekuwaje tena nembo yake iwe kwenye jezi za Simba?

Si tuliambiwa GSM ataishia kwenye mabango? Imekuwaje tena nembo yake iwe kwenye jezi za Simba?

Hahaha...

Makolo si nao wamwambie Mudi aweke mpunga ili Utopolo nao wavae jezi zenye yale makolo ya Mudi...
Shida MO amepiga hela kisha ameitelekeza timu.Ilitakiwa moto kwa moto watoe hela nao kudhani ligi kuu .Ili Yanga nao wavae nembo ya MO na Vunja bei
 
Hahaha...

Makolo si nao wamwambie Mudi aweke mpunga ili Utopolo nao wavae jezi zenye yale makolo ya Mudi...
Hakuna haja, kuweka mpunga huko ni kunufaisha wengine bila sababu. Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Simba wavae tu wala hakuna shida
 
Shida MO amepiga hela kisha ameitelekeza timu.Ilitakiwa moto kwa moto watoe hela nao kudhani ligi kuu .Ili Yanga nao wavae nembo ya MO na Vunja bei

Hahah...

Tena jezi ya Utopolo inakuwa na logo ya Mo Xtra kwenye makalio kama majezi ya timu za uarabuni
 
Kisheria bodi ya ligi/tff ndio wasimamizi wa mpira wa nchi hii, na mikataba yote hususani inayohusiana na udhamini wa ligi nzima , wao ndio wanaingia.Kwani huo udhamini wa azamu, Nbc bank, mbona hawakuhusishwa?na hata huko nyuma toka enzi za vodacom, tbl hawakuwahi kuhusishwa, na ndio maana huwa suala la logo huwa linaleta utata mala tu mdhamini anapokuwa ametangazwa?
Na kisheria na kikanuni nembo ya mdhamini mkuu ndio inayokaa ktk jezi ya timu ,na ndio maana ilitakiwa kama kanuni au sheria imebadilishwa kuwa kwamba ata mdhamini mwenza akae ktk jezi basi ilitakiwa wadau na vilabu washirikishwe ,hii ni sawa sawa bunge kupitisha sheria pasipo kushirikisha wabunge wenyewe
 
Mbona simple tu MO na Vunja bei wapeleke ombi TFF la kudhamini ligi kuu.Ili Yanga nao wavae nembo original ya MO na Vunja bei.Niutani tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Wakifanya hivyo watakua wametatua tatizo?
 
Nani kakwambia hapa Yanga imehusishwa? Mbona wewe ndiyo unaonekana kuongozwa na mihemuko,umepna tu Simba wamepinga,ukaja na sababu zako kichwani kuwa Sababu GSM ni Yanga,tuonyeshe sehemu CEO wa Simba kaihusisha Yanga katika sababu alizozitoa
Umesoma barua ile lakini? Yanga imetajwa mara ngapi mle?
 
Kisheria bodi ya ligi/tff ndio wasimamizi wa mpira wa nchi hii, na mikataba yote hususani inayohusiana na udhamini wa ligi nzima , wao ndio wanaingia.Kwani huo udhamini wa azamu, Nbc bank, mbona hawakuhusishwa?na hata huko nyuma toka enzi za vodacom, tbl hawakuwahi kuhusishwa, na ndio maana huwa suala la logo huwa linaleta utata mala tu mdhamini anapokuwa ametangazwa?

Na kanuni ile ya nembo itakayovaliwa itakuwa ya mdhamini mkuu peke yake kwa mujibu wa kanuni ya 16 ya TFF unalitolea ufafanuzi upi hapa?
 
Hatuvai na hizo fine zao za mil. 2 tutalipa, sisi hatuna shida na pesa
 
Back
Top Bottom