Siamini kama naelekea kuondoka kwenye Ardhi ya laana

Mambo yakitiki sidhani kama nitarudi kwenye hii ardhi iliyolaaniwa inayonuka damu! Nitakua natoa tuu pole nikiwa huko ughaibuni nawaangalia tu mnavyopimwa shaba.
Kwani huna ndugu, jamaa au marafiki huku bongo?...Au hao hawakuhusu?... anyway kila laheri.
 
Wewe mbona haurudi bongo?
Suala si kurudi au kutorudi Bongo.

Suala ni jinsi ulivyoandika.

Kwanza umelimbuka, lakini ulimbukeni si tatizo.

Tatizo ni ile hali ya kuwa huoni raha mpaka uwatambie wengine, Kiingereza inaitwa "to lord it over them".

Njoo tu ujue moto wa ughaibuni kuna wengine waliomba poo wakarudi Bongo wenyewe.
 
Utapatamani urudi we ufanye ukabaji wizi halafu uachwe nenda hata leo una faida gani kwenye hii nchi hata mtaani kwako hujulikani
 
Kwa hili lililotokea na yanayoendelea kutokea ni wazi kuwa wengi wataondoka kulinda usalama wao.

Ukiwaza vifo vilivyotokea kwa wengi waliokuwa wametulia zao tu nyumbani inaumiza na inahatarisha sana maisha. Bado kuna kamata kamata ya vijana, tumeshakuwa wakimbizi kwenye nchi yetu wenyewe.
 
Minakuja naamini huo moto nitauvumilia kama wewe ulivyovumilia mpaka leo umejichimbia mambele, ulimbukeni kawaida maana sijawahi kukanyaga UGHAIBUNI, ni kama tu miaka ile mtu wa mkoani ukiahidiwa kusafiri kwenda dar lazima upagawe.
 
Kama wale watoto wapo wanasali wameshika biblia mtu kaingia kampiga mamayao ya kichwa unafikiri wataitamani bongo wale, wakipata upenyo wakiondoka hawarudi tena
 
Minakuja naamini huo moto nitauvumilia kama wewe ulivyovumilia mpaka leo umejichimbia mambele, ulimbukeni kawaida maana sijawahi kukanyaga UGHAIBUNI, ni kama tu miaka ile mtu wa mkoani ukiahidiwa kusafiri kwenda dar lazima upagawe.
Ukimbukeni si tatizo kwani ni aina ya ujinga na mjinga hachekwi anaelimishwa tu.

Ila, punguza shobo za kucharaza wenzako fimbo sana kwa sababu unakwenda ughaibuni tu, bado upo dunia hii hii ughaibuni si mbinguni kihivyo.

Fikiria kuna wengi hawatakuwa na uwezo wa kuondoka kama wewe na ku lors it over them like that is just so selfish and ignorant.

Buju Banton katika "Untold Stories" aliimba.

"Who can afford to run will run
But what about those who can't they will have to stay"


View: https://youtu.be/Kb-0Eo0Yk0o?si=WCOkGNyVtnxMLjeo
 
Mkuu unajiskiaje unaondoka unaacha ndugu na jamaa zako kwenye moto,huko ulaya utaishi kwa amani ya moyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…