Siamini naanza kuacha uhuni, umalaya, ubazazi na ubaradhuli. Huyu mtoto nimemuibua humu humu JamiiForums

Siamini naanza kuacha uhuni, umalaya, ubazazi na ubaradhuli. Huyu mtoto nimemuibua humu humu JamiiForums

asikwambie mtu ukisikia "kupatwa kwa gudume ndo huku" hii huwa inatoka mara moja kila baada ya miaka 1,000. waswahili wanasema "aisifuye mvua imemnyeshea" moyo wangu umepapatika kwa miaka mingi sana na hatimaye umefika kwenye kilindi cha bahari na kutulia tuli kama maji ya mtungini.

Duuh! Hatimaye kaka GuDume umepatwa lol. Sababu sio kwa sifa hizi ulizozimwaga.

Kila la kheri kaka! Ila sio kwa misemo hiyo leo sababu usingeitumia , nadhani uzi wako ungekuwa mrefu hatari.
 
shukrani ndugu yangu... ni upenzi tu wa lugha hii adhimu ambayo haishi hamu na utamu.
Mkuu Leo umetumia vitendawili nahau misemo mithali na tanakali sauti nyingi mno
Hongera ndugu yangu.


Nami naingia chimbo niibuke na mke
 
mkimuibukia ana screen shoot ananitumia... na tayari ameshanitumia wote waliomtaka humu nawafaham ntakuja tu kuwapa onyo muda si mrefu.

Kwa kuwa na sisi tunatafuta humu humu, ni vizuri ungemtaja kama alivyofanya Mshana Jr ili tusije tukajikuta tunamuibukia shemeji yetu pm kwa kutojua[emoji41] [emoji41] [emoji41]
 
hizo ni zako mimi yangu "jasiri haachi asili" yako wewe iandike utakavyo ... hiyo ya ukambaa ni typing error tu.

Umejitahidi na methali, ila umekosea tu kdg. "Jahili aachi asili" na sio"jasiri"...... Ukuukuu wa pamba, si upya ukambaa. Not mkambaa..!
 
ha ha ha.. mwenye moyo mgumu lakini laini, mwenye macho makali ya kuona ndani lakini mapole kwa kuona nje... mwenye uzuri wa waridi. aliyeogea maji ya majani ya mkaratusi.. mwenye uzuri wa tausi..... sauti ya chiriku.... mwendo wa maringo kama twiga atembeapo kati kati ya msitu... amejawa maneno matamu ya kumtoa nyoka pangoni. hana makuu mwenye moyo wa huruma na upendo wa asili....
Ni mwanamke gan anaweza kumteka gudume
 
ndugu zanguni (leo hata namna ya kuwa address imebadilika) nashukuruni sana kwa kweli... mtoto kaumbika... mashavu yake yote yanaonekana kuwa na mvuto,sura ya yai,lips za mfuto na macho ya goroli. rangi yake ya chungwa lilioiva ... akiongea ni kama hataki maana anaweka vituo vyote kwa usahihi kabisa. kwa kweli... "mla mla leo ,mla jana kala nini?" nami nimejipatia mtoto mantashallah... allahamdullilah "kimfaacho mtu chake" maana msije waswahili mkaanza kusema oohh.. sijui ni na nini... gudume amekutana na maneno ya wahenga ya kuwa "subra yavuta kheri"
SAFI SANA
 
Back
Top Bottom