Siamini Shilingi ya Somali na Gourde ya Haiti ina thamani kuliko shilingi ya Tanzania

Madini 🤝
 
Somalia's agricultural sector is the backbone of the economy, contributing to over 70 percent of total GDP, 80 percent of its employment, and about 50 percent of its exports.

Wanalima muda gani huku wanapigana muda wote ?
Gomba
 
Somalia's agricultural sector is the backbone of the economy, contributing to over 70 percent of total GDP, 80 percent of its employment, and about 50 percent of its exports.

Wanalima muda gani huku wanapigana muda wote ?
Somalia 🇸🇴 wanaexport animals Quality products kama vile hornes,skin,hide,hoof na products zingine za mifugo kama fresh carcases kuliko tanzania


NB; vita kila siku ipo wanapigana! Hapa ndy utaelewa kwann wabongo ni bongolala.
 
Kuna Mtu alisema waandishi wa Habari Tanzania hawajui kuandika Namba na wewe inaonekana ni Mwandishi.

132,38 badala ya 13,238.

Hata hivyo kwa hesabu zako Thamani ya Tanzania dhidi ya Dola ni kubwa kuzidi hizo za Haiti na Somali
 
Nadhani umefananisha GDP na hali ya kupanda thamani ya Usd. GDP yetu ni kubwa kama mara tatu hivi ya hao Somalia.

Ila kuhusu thamani Usd kuna mambo kadhaa hupandisha kwenye nchi, hata suala kukosekana utulivu wa kisiasa.

Lakini demand ya Usd huchochea sana inunuliwe kwa bei kubwa katika nchi. Kama vile sukari watu wakiitaka sana, inapanda bei.

Mahitaji ya dola yanapoongezeka ndivyo thamani yake inavyoongezeka. Mahitaji yakipungua, ndiyo thamani inapungua.

Pia, mfumuko wa bei wa ndani ya nchi nao hupandisha dollar, unakuta bidhaa imejazwa tozo hadi inapanda, basi inaamsha dola.

Hata trade deficits, yaani uagizaji bidhaa za nje ya nchi kuwa mkubwa kuliko bidhaa za ndani kuuzwa nje nayo inapandisha dola.

Maana mtahitaji kununua dollar nyingi ili muagize bidhaa huko nje, huku ninyi mkizipata chache kwa mauzo yenu madogo nje. Hiyo inaleta demand ya dollar, ni lazima ipande.

Ova
 
Haloo , Haloo Wariaa.....
Mbrrrrrrrrrrrr

 
Gdp per capital zao je? Kupima uchumi wa nchi kwa uimara wa sarafu tu ni ujinga.
 
Kwahiyo unataka mama aendelee kukopa ili thamani ya pesa yetu ipande?
Usiwe na haraka subiri DP World waanze kazi mapato yataongezeka na TSH itapanda thamani!
 
Tofautisha exchange rate na thamani ya sarafu. Exchange rate inategemea sana uongozi na usimamizi wa mzunguko wa pesa. Iwapo nchi inaingiza pesa kwenye mzunguko kiholelea kama Tanzania inavyofanya sasa, basi exchange rate ya sarafu yake itapungua. Somalia na Haiti hazina pesa nyingi kwenye mzunguko wake kwa hiyo exchange rate ya pesa yake ni strong.
 
Haina mashiko kulinganisha.

Nikuulize hili na kisha tafakari.

South korea won 1= 1.92Tsh

Je tunapimana misuli na wakorea kiuchumi kisa thamani za ela zetu zinakaribiana?
 
Hapa lazima uchanganyikiwe, je ni kweli shilingi ya kenya Ina nguvu kuliko Yen ya Japan?
1 USD = 161.03 Japanese Yen
1 USD = 128.25 Kenyan Shs
 
Ungesema pia hela yetu imeipita ya Iran na nchi kibao
 
Kuna Mtu alisema waandishi wa Habari Tanzania hawajui kuandika Namba na wewe inaonekana ni Mwandishi.

132,38 badala ya 13,238.

Hata hivyo kwa hesabu zako Thamani ya Tanzania dhidi ya Dola ni kubwa kuzidi hizo za Haiti na Somali
Sio kweli
 
Kwahiyo unataka na sisi tubadilishe mfumo wa uandishi kwa ajili yako sio?
 
Hata Tanzania hela yetu ina thamani kuliko Indonesian rupiah lakini Indonesia imetuacha mbali kimaendeleo
 
Mtoa mada hata kama kakosea kuweka alama lakini swali lake lina mantiki
Mfano mshangae Italy hela yake ya Lira iko chini sana dhidi ya shillingi ya Tanzania lakini ni nchi iliyopiga hatua kubwa mno kimaendeleo kwa viwanda na ni moja ya G7.
Marekani pamoja na dola yake kutumika sana duniani lakin haifui dafu kwa nchi ya kuwait
Japan ina maendeleo makubwa tungetegemea hela yake iwe juu kuliko marekan lakini hali sio hivyo

Wanauchumi tunaomba msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…