Siasa: April 2020 imebeba ujumbe mzito!

Siasa: April 2020 imebeba ujumbe mzito!

Rais SSH ametoa kauli kuhusu udini, ukanda na ukabila
Kwa sababu unasimamia masuala ya facts. Bila kuficha chochote, unaweza kuweka mifano halisi kuonyesha, awamu ya tano namna ilivyoendeshwa kwa 1) Udini 2) Ukanda, na 3) Ukabila?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
APRIL NA YALIYOMO

Mwezi wa April umeendelea kuja na yasiyotarajiwa

Taarifa ya CAG
Taarifa imeacha maswali mengi kuliko majibu kwa kinachoitwa ''madudu'
Kiongozi wa ACT Bw Zitto amehoji Bilioni 70 zilizokuwa zinapelekwa Mwanza bila maelezo

Wapo wanaona taarifa ya CAG ni 'ya kupikwa' ina matundu mengi. CAG aliyepo aliteuliwa na Rais JPM katika mazingira tatanishi yaliyomuondoa CAG Asad

Hoja si nani ni CAG bali taarifa kama ina mashiko. wenye shaka hawana utetezi dhidi ya tuhuma.
Haitoshi tu kueleza taarifa ni mbovu, ni lazima kwenda mbali na kuthibitisha ubovu. Halijafanyika!

Kiongozi wa ACT akashambuliwa kwa kuhoji mabilioni akisema awamu ya JPM ilikithiri ufisadi kwa taarifa ya CAG. Bw Zitto akashambuliwa kwa kauli ya 'kuzikwa chato'

Kauli ya Zitto imepewa uzito na watetezi wa awamu ya tano badala ya kutetea hoja alizotoa Zitto. Kwamba, Zitto anashambuliwa na si kujibiwa. Hili litabaki kuwa tatizo, Zitto ajibiwe kwa hoja

RAIS SSH NA ROYAL TOUR
Mh Rais yupo Marekani kuzindua filamu ya Royal tour. Kuna mjadala kuhusu hili

Wapo wanaohoji gharama za Filamu na kama italeta matokeo yaliyokusudiwa
Wapo wanaohoji kwanini uzinduzi umefanyika Marekani
Wapo wanaohoji kwanini hakutafutwa nyota yoyote ili kuweka mvuto katika mitandao

Jambo moja 'common' kwa makundi yote, kwamba, Rais amefanya jambo jema.

Nchi ni kama ''bidhaa'' inahitaji kunadiwa. Nchi za dunia zina namna ya kujinadi hata kama si utalii
Kwa miaka michache Tanzania tulipoteza hata ule ushawishi wetu kwasababu hatukujinadi

Tulipoteza ushawishi na kujinadi tukiamini katika maguvu badala ya maarifa na mikakati

Utalii ni sehemu muhimu ya uchumi. Kuvutia watalii ni jambo moja, mikakati ya kushindana ni jambo jingine. Mh Rais anatakiwa apate usaidizi wa taasisi husika.

Kuna kila sababu ya kuangalia taasisi zinazohusika na utalii pamoja na Bodi ziwe za tija.
Tatizo letu ni nafasi za kitaalamu kufanywa ima za kisiasa au kupeana fadhila

Yote ya Dubhai na US hayatakuwa na maana bila uatiliaji na mikakati ya kupambana na dunia ya ushindani katika utalii. Swali la kujiuliza , je, kinachofanyika ni 'sustainable' au ni kazi za zimamoto!

Mjadala wa jinsi gani ilitakiwa iwe utaendelea na ni mzuri kwa afya ya nchi.

MAMA SALMA NA MAFAO
April haijakosa matukio ya kushangaza. Mbunge wa Mchinga na mke wa Rais wa awamu ya nne, mama Salma JK ametoa hoja ya Wake za viongozi kuandaliwa mafao kisheria wanapostaafu

Hoja ya Mb Salma imetibua nyongo katika mitandao ya jamii, wengi wakiita ubinafsi.

Hoja zitolewazo ni kwamba, awamu ya tatu ya Rais Mkapa viongozi wa juu walijitengenezea sheria ya mafao ikiwemo kuhudumiwa maisha yao yote na mshahara katika silimia 80 kama ni sahihi.

Awamu ya Tano ikatengeneza utaratibu unaohakikisha viongozi wakuu hawashtakiwi
Awamu ya Tano ikawajengea nyumba za kuishi viongozi wakuu wastaafu bila kujali walikuwa nazo

Mh Salma kwasasa ni Mbunge wa Mtama akipata masilahi yote kama mbunge mwingine

Katika mazingira hayo kuna umuhimu gani wa kutengeneza sheria za Wake wa viongozi wastaafu.

Pengine Mama Salma angejiuliza yule Mama aliyelala pale Mtama mgongo ukimuuma kwa uzito wa kuni na ndoo za maji jana yake au yule mzazi ambaye ndugu wanakimbizana kuitafuta heri yake juu ya tenga la baiskeli au yule Mwalimu wa kike aliyeinamia taa ya kandiri akitayarisha somo , wote hao wanajisikakiaje wakimsikiliza mama Salma akidai mafao yawe kisheria !

Hivi kweli Tatizo la Wananchi wa jimbo la Mchinga na pengine Wanawake wa Tanzania ni suala la mafao ya Wake za viongozi wakuu wa nchi! na hilo ni tatizo lao kubwa la kufikishwa Bungeni?

April ya 2022 imebeba mengi
 
APRIL
Mwezi huu unaendelea kuwa na matukio ya kurahisha, kuhuzunisha na mengine burudani1

ZIARA YA Mh RAIS SSH
Ziara ya uzinduzi wa Filamu ya Royal tour. Kuna ya kujadiliwa na mitandao inaendelea kurindima.

Rais aliongea na Diaspora katika Hotel karibu na ubalozi , kubwa ni Uraia pacha akisisitiza haupo bali watapewa hadhi maalumu. Uraia pacha ni ombi la Wana Diaspora washiriki ujenzi wa Taifa bila kukwazika. Rais kasema draft ya mswada (Bill) itasambazwaDiaspora waitolee maoni

Mh Raia hakuongelea yanayohusu nchi kama Katiba.
Katika hali ya kutatanisha Mh Rais alisema ameona mabango ya ''vijana'' waliokuwa nje ya ubalozi
Watanzania hao hawakuwa wengi lakini shughuli yao ilionekana pevu, Mh Rais alipitishiwa uani

Nchini Marekani uwepo wa Rais SSH unatambuliwa na serikali kuu ya Washington na ya Jimbo
Balozi wa USA Tanzania alishaitaarifu nchi yake juu ya ugeni, si suala la kubahatisha

Vyombo vya usalama vilijiridhisha Rais wa Tanzania yu salama salimini
Laiti kungalikuwa na tishio awaye angeshatiwa nguvuni, inatosha kusema hakukuwepo tishio

Vyombo vya usalama vya marekani vinashughulikia usalama wa kila mtu, anayelalamika (waandamanaji) na anayelalamikiwa awaye. Vyombo havitoi vibali vya watu kufanya shughuli zao

Vyombo vya usalama vya Marekani havipigi ramli ya matukio (taarifa za kiintelejensia) bali hufanyia kazi taarifa hizo vikikusanya ushahidi wa kutosha.

Kumpitishia Rais uani kuna maana moja, alikoseshwa fursa ya kuwasikiliza Watanzania wenye maoni tofauti na wale aliowakuta ukumbini. Makundi yote ni Raia wake na ni vema kuwasikiliza

Mh Rais alikuwa na fursa ya kupita bila kuongea nao, kuongea nao au kuwasikiliza tu akaendelea na shughuli zake. Fursa hii ingalikuwa sawa na ile aliyoitumia kukutana na Tundu Lissu nchi nzima ikazizima. Rais kukutana na TL kulimfanya awe na nguvu na kumjengea heshima sana

Kukutana na TL kulionekana kama 'udhaifu' mbele ya Wapinzani. Mh Rais akatumia 'udhaifu'( weakness) huo kuufanya nguvu (strength) mwisho wa siku akapata mileage nzuri sana kisiasa .
Nini kkilishindikana Washington , DC? hadi kupitishwa uani ! kwanini Rais atendewe haya?

Kumpitisha uani kumekuza sauti za kikundi kile kilichokuwa nje na mabango
Habari inayozungumzwa si ziara, si royal tour wala si hotuba kwa diaspora bali jinsi alivyowakwepa Raia wake na kikundi cha waandamanaji kufanikiwa 100%

Ujumbe wa kikundi cha waandamanaji umefika palipokusudiwa! ujumbe umesambaa dunia nzima kwa kupata 'kick' . Agenda za Mh Rais zikafunikwa na hoja ya Katiba! kkundi kikafanikiwa kuiweka agenda ya Katiba katika maongezi kuliko ziara ya Rais iliyosheheni mambo mengi sana.

Waliopanga au kumshauri Mh Rais hawakumtendea haki! Waliongozwa na hisia zaidi badala ya busara. Hakukuwepo sababu ya kumpitisha Rais vichochoroni! Hawakumtendea haki!
 
APRIL YAISHA NA MUUNGANO

MSEKWA ATOBOA SIRI NA KUCHOCHEA MOTO WA KATIBA

Katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haikumbukwi lini muungano haukuadhimishwa. Mwaka 2022 April limetokea hilo pengine kwa mara ya kwanza. Rais alikuwa ziarani Marekani, lakini je, ziara haikuratibiwa na kujua itaingiliana na siku hiyo muhimu?

Muungano umeadhimishwa kwa mikutano na mmoja ni ule uliofanyika Dodoma ukiwahusisha wazee wakongwe wa chama na Serikali wakiwemo Spika mstaafu P. Msekwa na Waziri mkuu mstaafu na makamu wa kwanza wa Rais Jaji J.Warioba

Katika mada zilizowasilishwa ilisemwa muungano ni imara bila ithbati ya uimara wake

Mzee Msekwa alieleza muungano ulivyoasisiwa kwa kuzingatia kuwa kulikuwepo na tishio la kurudi kwa watawala wa serikali iliyopinduliwa Zanzibar

Mzee Msekwa akasema taratibu za muungano zilifanywa kwa siri sana kuzuia kuvuja.Usiri mkubwa baina ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume .

Mzee Msekwa alisema yeye alihusika kupeleka mswada bungeni haraka na kupitishwa kisha kusainiwa haraka haraka na Rais, Nyerere akiwa Rais na Karume Makamu

Kauli ya Mzee Msekwa inaonekana nyepesi lakini imebeba mambo mazito.
Kwa wanaosema muungano haukuwahusisha wananchi wa nchi mbili, Msekwa inathibitisha hilo

Hii ina maana moja kwamba ni wakati kufanyike referendum ya kuwauliza wananchi ikiwa wanautaka muungano maana ukiundwa hawakuulizwa.

Ikiwa referendum itakuwa 'ngumu' ni wakati wa kupitia tena mambo ya muungano
Maana yake ni kuwa maoni ya Wananchi kupitia rasimu ya Warioba

Katika wakati uliopo kuna njia mbili tu zilizobaki
moja, ni referendum au pili, kuandika katiba mpya itakayoeleza muundo wa muungano

Mzee Msekwa kathibitisha wananchi hawakushirikishwa! hakuna tena mjadala bali kuwashirikisha

Wazee wengine akiwemo Mzee Warioba waliongelea faida za muungano kwa ujumla bila kutaja

Kwa kizazi cha leo kusema tu muungano unafaida bila kuzianisha si sahihi! hiki ni kizazi cha kuhoji

Mwezi huu katika mitandao kumekuwepo na nakuu ya Rais wa Zanzibar ikizungumzia ' umiliki wa aradhi ambao Mtu wa Tanzania bara anakuwa sawa na mgeni''

Katika mitandao ya tweet, Insta, JF na kwingine hilo limewaudhi sana Watanganyika
Wengi wanasema huu ni muungano gani? Kwa kuangalia umiliki wa ardhi tu!
Vipi watakapobaini gharama anazobeba Mtanganyika peke yake!!

Kwa ufupi kauli ya Rais Mwinyi imeibua mjadala mzito sana na hata kuhoji mambo mengi sana ambapo Watanganyika wanaonyesha wazi kutoridhishwa.

Kinachowakera sana Watanganyika ni ukweli kuwa wao wamebeba mzigo wa muungano asilimia 100 lakini hawasikilizwi

Kwamba kero zimekuwa ni Wazanzibar kupewa chochote wanachotaka hata kwa gharama za Watanganyika.

Makongamano ya sherehe za muungano yamefunua kidonda !

Dawa si kukifunika bali kukitafutia dawa mapema.

ikiwa viongozi wataendelea kupuuza hoja za Watanganyika ipo siku wataamka asubuhi na kukuta Watanganyika wanasema hapana! muungano utakuwa matatani

Lakini pia ipo siku wananchi watadai kura ya maoni (referendum) na itafanyika kukiwa na chuki itakayondoa busara. Muungano utakuwa matatani.

Asilimia 90% ya kizazi hiki haikuwepo wakati wa muungano, na zaidi ya 60% imezaliwa miaka ya 80 hadi leo. Ni kizazi kinachohoji kwa mantiki! Hoja zisipojibiwa kwa hoja hakuna mtutu utakoweza kulinda muungano!

Waswahili husema mchelea mwana kulia!
 
Mpaka unauliza wanajamvi kama kuna yeyote mwenye shaka juu ya Tuhuma za Udini, Ukanda na Ukabila, bado tu unataka kujitoa miongoni mwa wale wenye FURAHA sawa na wazee wa CCM?

Mbali zaidi ukahitimisha kwa kusema Hakuna Shaka kuwa awamu ya tano ilipanda mbegu mbaya nchini. Bado unadai hu miongoni mwao wakenuao meno wakati huu?

Tunajua in Upinzani+CCM Vs Magufuli. Jamii haikuwahi kuwa kinyume na Magufuli, ila ni huo muungano wa TimuMaslahi.

JIPONGEZENI, KWA MAANA MMESHINDA. Nasi tutaendelea kuomboleza na labda sauti yetu Itasikika Tena. Tumaini lipo.
Mnafaiki sana huyu jamaa...
 
....

Kwanza pole sana , pili maoni yako hayajadiliwi ni yako
Nadhani natakiwa labda nirudi kwenye SHULE ya kushiriki mijadala.

Maana ninachojua, Mjadala uanza kwa pale mada ya mjadala inapowekwa wazi kupitia kichwa cha habari ya mjadala huo.

Kisha mtoa mada hutoa ufafanuzi juu ya mjadala ama kwa kumtumia facts au maoni yake binafsi. Washiriki wa mjadala huo ujadili mada husika vile vile kwa kutumia facts ama maoni Yao huku wakitoa ushahidi wa kubeba maoni Yao. Ni kupitia maoni ya washiriki wa mjadala huo mjadala wenyewe uimarika kwa afya ya uelewa wa washiriki wote wa mjadala na wale wanaofuatilia mjadala huo.

Sasa hapa JF na hasa kwenye uzi huu ni kama tunaelekezwa tujadili facts tu bila kugusa maoni ya washiriki wa mjadala huu. Na hapa ndiyo najiuliza, ni kweli bandiko la kwanza la uzi huu limejaa facts tu kiasi ndizo zinatakiwa kujadiliwa?
 
Je, una uhakika wowote juu ya chanzo cha kutokea kwa Corona Virus?

Je, umeshawahi sikia uwepo wa virus vilivyotengenezwa maabara?
Hivi Majuzi Russia kagundua zaidi ya maabara za kibailojia 11 za viwango vya kijeshi huko Ukraine. Na moja ya vimelea hatari vya Corona vilikuwa kwenye mpango huo ulikuwa unaratubiwa kwa Karibu sana na Marekani kama alivyodhibitisha Bibi Nulad kiongozi mwandamizi wa Marekani aliyeshiriki kuipindua serikali halali na ya kidemokrasia ya Ukraine mwaka 2014.

Russia imeweka wazi ushahidi maabara hizi.
Sasa, huko Ukraine, Je. US ilikuwa inaimarisha uchumi wa Russia kwa kuanzisha Maabara za kujaribu silaha za kibailojia kwa raia wenye asili ya Russia?
 
Hivi Majuzi Russia kagundua zaidi ya maabara za kibailojia 11 za viwango vya kijeshi huko Ukraine. Na moja ya vimelea hatari vya Corona vilikuwa kwenye mpango huo ulikuwa unaratubiwa kwa Karibu sana na Marekani kama alivyodhibitisha Bibi Nulad kiongozi mwandamizi wa Marekani aliyeshiriki kuipindua serikali halali na ya kidemokrasia ya Ukraine mwaka 2014.

Russia imeweka wazi ushahidi maabara hizi.
Sasa, huko Ukraine, Je. US ilikuwa inaimarisha uchumi wa Russia kwa kuanzisha Maabara za kujaribu silaha za kibailojia kwa raia wenye asili ya Russia?
Ndio maana nilimshauri asiliongelee hili la vita ya Kiuchumi, maana hoja zake ni za kitoto mno. Ubaya zaidi si kwamba hajui Vita ya Kiuchumi ni nini. Inatia shida kidogo kuona mtu mzima wa heshima zake akijitoa ufahamu.

Leo Russia na NATO zinavutana, athari zake zimetufikia huku tulipo, na upo uweuwezekano wa sisi kuwa walengwa hasa.
Anatokea MTU kutuambia Tukwepe milindimo ya hiyo, eti wanaojiona wasomi ndio wa kwanza kumpinga. Hii nchi ngumu sana. Wasomi wetu wako brainwashed, kiasi kila kitu wanachukulia rahisirahisi.
Kuitikia Milindimo hiyo ni Kujitia kwenye mitego yao, lakini bado hatuoni.
 
a4afrika Huu uzi hausiani na mada mnazojadili, hamisheni kunakohusika tafadhali

Kama mnataka kujadili ya Mwezi April sawa, hayo mengine pelekini nyuzi husika
 
Hivi Majuzi Russia kagundua zaidi ya maabara za kibailojia 11 za viwango vya kijeshi huko Ukraine. Na moja ya vimelea hatari vya Corona vilikuwa kwenye mpango huo ulikuwa unaratubiwa kwa Karibu sana na Marekani kama alivyodhibitisha Bibi Nulad kiongozi mwandamizi wa Marekani aliyeshiriki kuipindua serikali halali na ya kidemokrasia ya Ukraine mwaka 2014.

Russia imeweka wazi ushahidi maabara hizi.
Sasa, huko Ukraine, Je. US ilikuwa inaimarisha uchumi wa Russia kwa kuanzisha Maabara za kujaribu silaha za kibailojia kwa raia wenye asili ya Russia?
Please uzi hausiani na mada unayodali, peleka kule kwenye uzi wa Mlenge (Pumzika kwa amani)!

Hapa jadili ya mwezi April. Hivi mnafanya hivi kwa bahati mbaya au kuna sababu? Msichanganye wasomaji tafadhali .
 
Hivi kweli upoje? Wewe si ndio umeleta mambo ya Corona humu, unachaguaje namna ya kujibiwa?

Wewe umeshindwa kuelewa dhana ya Vita ya Uchumi, Ndugu hapo amekuelekezea kwa mfano halisi kabisa, bado unashindwaje kuelewa?
Huu uzi ni wa matukio ya mwezi April 2022 tu! hakuna mahali covid imetajwa katika mabandiko tangulizi. Please rudisheni mjadala kwenye sehemu husika tutajadiliana

Hapa tujadiliane ya April tu kama mabandiko yanavyosema
 
Hapa tujadiliane ya April tu mabandiko yanavyosema
Ndiyo maana katika post namba 27 ya uzi huu nikaandika labda nirudi shule ya kushiriki mijadala. Baada ya kupewa sharti la kushiriki mjadala bila kujadili maoni na ushahidi unaoletwa na washiriki kuhusu mada iliyopo mezani.

Leo tumeongezewa sharti lingine la kujadili Mambo ambayo yalisemwa April tu! Sasa ukichunguza yale yaliyosemwa April tu ambayo, nguli wetu wa mijadala ndugu Nguruvi3, ni karibu mengi yanahusiania na mambo yaliyosemwa miezi iliyopita yaani kuanzia March 30, 2022 kurudi nyuma. Yaani mpaka yale ya miaka miwili nyuma. Nimejaribu kuyaanisha mambo yanayoonyesha hayakusemwa ama kutendwa April 2022 bali ni mambo ya nyuma ili niweze kuonyesha tatizo linalonikabili katika kuhusika katika mjadala huu ulio mezani kutokana na "masharti bunifu" anayoyatoa mleta mada kwenye uzi huu kadri anavyojisikia inafaa.

Ni ajabu sana mleta maada ambaye amekuwa mtu muhimu sana katika kuchochea uhuru wa kutoa maoni si katika jukwaa hili nadhani hata kwenye maeneo yake mengine ya kufanyia kazi, naye kuanza kufifisha juhudi za wananchi ama washiriki wa mijadala kutoa maoni yao na hasa mahali pale wanapooneka wanaonyesha udhaifu wa kimtazamo wa mleta mada.

Ni kweli, mleta mada ni Mwalimu wangu muhimu sana hapa JF, lakini kitendo cha kupinga yale aliyonifundisha juu ya uhuru wa kutoa maoni kimenistua sana.
=====
Ni ujumbe ulioashiria nchi haikuwa katika mstakabali mzuri miaka michache iliyopita.
Hapa unazungumizia mika michache iliyopita, hii si April 2022 tena, hivyo lazima turejee miaka michache iliyopita tuone nini kilitokea ili kuimarisha mjadala ulipo mezani.

Washiriki walimweleza Mwalimu Nyerere kadri walivyomfahamu
Lazima turejee matendo ya Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake (siyo April hiyo) ndipo tujikite vyema kwenye mjadala.

Katika kuchangia Bw Lyongo alizungumzia udini, ukabila na ukanda akisema miaka ya karibuni tumerudi nyuma. Hakuna shaka Bw Lyongo alizunguzia utawala wa JPM
Kujadili mazungumzo ya Lyongo lazima tuirejee kwenye hayo matukio ya miaka ya hivi karibu tuone nini hasa kilitokea. Hakuna cha April 2022 hapa!
Ni kwa kuelewa hivyo uchaguzi wa 2020 Mahakama kuu haikupata lalamiko, si kwasababu hayakuwepo bali ilionekana haki ya uchaguzi haitapatikana Mahakamani

Uchaguzi wa 2020 huo. Unaachaje kuyazungumzia matukio ya 2020 katika kujibu ama kutoa maoni kisa lazima tujadili ya April 2022. Kumbukumbu zipo lazima zirejewe kama kweli hatuna ajenda yenye kuficha baadhi ya mambo kisa April 2022 katika mjadala huu!

Ukichukua matukio matatu ya mwezi huu, hadhra na watu walioongelea hakuna shaka miaka awamu ya tano ilipanda mbegu mbaya nchini
Awamu ya tano kwa mujibu ya baadhi ya Watanzania ilikoma mwaka jana baada ya kumpata Mama yetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa kiongozi wetu wa nchi yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Hawamo ya tano si ya April 2022. Sasa kwa nini unatuzuia tusirejee kile kilichotokea awamu yatano ili kutoa maoni yetu na facts ili kuijenga hoja kwenye mjadala huu, wakati msingi wa mada uliyoleta inajaribu kulinganisha matukio ya wakati uliopita na sasa kwa kisingizio cha yale ya April 2022?
Mwenyekiti aliwahi kuingia matatani kwa kauli ya kutaka ''viongozi wachunguzwe kwani wapo waliokuwa na mafaili Mirembe''

Hii kauli haikutoka April 2022. Sasa tunaachaje kumjadili mtoa kauli hii na mahusiano yake na wale ambao alikuwa najaribu kuwajengea taswira ya udhalilishaji?
======
Kwa kweli, mwalimu wangu Nguruvi3 umenistaajabisha sana.
 
Wanajamvi, hakuna anaye limit mjadala kwa namna yoyote

Kinachosemwa hapa ni kuwa lazima tuwe super market na siyo dula la ''mpemba au mchaga'' unakotafuta majani ya simba kwa nusu saa.

Mabandiko yakliyopo yanahusu matukio ya April, haina maana mjadala uishie hapo, la hasha.

Mjadala unaweza kuwa extended within the perimeter of subject for discussion
Ndiyo maana kila bandiko lina kichwa.

Itashangaza kichwa kikiwa Anguko la Ndugai halafu habari na mjadala ni jinsi Harmonize alivyomsokomezea ngumi Omondi!

Wasomaji watashindwa kuelewa! tutawavuruga
 
Katika aliyofanya Rais SSH tangu achukue madaraka ni 'kuacha watu waonge' .

Rais alisema watu wakiongea viongozi wanaelewa nini kinaongelewa.
Katika kufungua uhuru wa maoni/habari uliofinyangwa miaka sita amefanya vizuri.

Kwa hatua hiyo Rais anapata faida ya ziada ya kuelewa kilichopo akilini na miyooni mwa jamii anayoisimamia kama kiongozi mkuu.
Mkuu Nguruvi3 , thanks for this
Jambo muhimu ni kuweka rekodi sawa na zisemwe wazi ili tujue ni akina nani , kwa njia gani wakifanya nini na kusaidiwa na nani walitaka taifa letu ligawanyike kwa misingi mibaya

Tusemezane
Hi ya kuanza kutafuta mchawi, au wachawi, siliafiki na siungi mkono.
P
 
Back
Top Bottom