PreGE2025 Siasa chafu dhidi ya Mwigulu ni woga wa 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hakika Dr.Mwigulu L.Nchemba ni mtu na nusu!
Kwa tunaomjua huyu ni Bingwa wa Uchumi na hesabu!
Uliza mtu yeyote aliyesoma Ilboru - Arusha na Mazengo High School- Dodoma.
Mtafuteni Professor Osoro au Dr. Ndashau pale University of Dar es Salaam wawambie nini Dr.Mwigulu alifanya pale UDSM.
Huyo ndiye Overall Best Student wa Mwaka wake katika kozi ya Uchumi.
Mwigulu ni mwadilifu,mnyenyekevu na hana makuu Kijana kutoka jamii ya kifugaji.
Dr.Mwigulu is one of the Best Economics brain we have as the Country at the moment.
fumadilu = madelu , madelu=mwigulu
 
Hatuna mashaka na elimu yake. Si Ni yake bhana. Sisi hatumuelewi kwa suala moja kubwa la kutetea wabadhilifu kwa nguvu zote eti kwa sababu tu ni watu wa chama chake, alafu eti unataka mtu Kama huyo tumuamini kweli.
 
Hakika Dr.Mwigulu L.Nchemba ni mtu na nusu!
Kwa tunaomjua huyu ni Bingwa wa Uchumi na hesabu!
Uliza mtu yeyote aliyesoma Ilboru - Arusha na Mazengo High School- Dodoma.
Mtafuteni Professor Osoro au Dr. Ndashau pale University of Dar es Salaam wawambie nini Dr.Mwigulu alifanya pale UDSM.
Huyo ndiye Overall Best Student wa Mwaka wake katika kozi ya Uchumi.
Mwigulu ni mwadilifu,mnyenyekevu na hana makuu Kijana kutoka jamii ya kifugaji.
Dr.Mwigulu is one of the Best Economics brain we have as the Country at the moment.
Hapa sifa zote ningezikubali kama angeweza kupaisha thamani ya pesa yetu..shilingi ya Tanzania inashuka kwa speed kubwa sana ukilinganisha na majirani zetu. Ilipanda kwa miazi miwili tukapata ahueni ila naona imerudi kulekule chini ilipokuwa...
 
Katika kila zama za siasa, kuna wanasiasa wachache wenye dira, msimamo, na rekodi safi ambao wanapopata umaarufu na kuwa tishio kwa wapinzani wao, huanza kushambuliwa kwa propaganda chafu, uvumi na hila ili kuwaharibia taswira yao kwa umma. Leo hii, Tanzania inashuhudia smear campaign ya wazi dhidi ya Dkt. Mwigulu Nchemba, Mwanasiasa mwenye rekodi safi, mwenye mchango mkubwa kwa nchi katika ujenzi wa kiuchumi na kiutawala, na ambaye bila shaka anaonekana kuwa endapo atatiania 2030 atakuwa tishio kubwa sana kwa maadui zake.

Kampeni hii inayofadhiliwa na genge la wapinzani wake wa ndani na nje ya chama chake, wakitumia mitandao ya kijamii na gazeti la mtandaoni lililoanzishwa kwa lengo moja tu – kumchafua. Wanatumia kila njia kumhusisha na ufisadi, pasipo hata punje moja ya ushahidi, huku wakipuuzia ripoti rasmi za CAG, Kamati ya PAC na LAAC ambazo hazijawahi kumtaja katika kashfa yoyote ya kifisadi.

Mwigulu ni kijana aliekuzwa vyema na Chama, kuanzia kuwa Rais wa Wachumi Vyuo Vikuu vinavyofundisha uchumi nchini, Mbaraza wa UVCCM, Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa, Mchumi wa CCM Taifa, Naibu wa Fedha, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Katiba, na sasa Waziri wa Fedha. Uzoefu huu unawatisha wapinzani wake, kwani wanajua wazi kuwa amejengwa na Chama kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Taifa siku za usoni.

Huu sio mchezo mpya katika siasa – ni mbinu iliyotumiwa kwa miaka mingi duniani kote dhidi ya viongozi waadilifu wenye nafasi kubwa ya kushinda madaraka.

Haya yanayomkumba Dkt. Mwigulu Nchemba sio ya kipekee kwa Tanzania pekee, bali ni mkakati wa kawaida wa siasa chafu duniani kote.

✅ Nelson Mandela (Afrika Kusini)

Kabla ya kuwa Rais, wapinzani wake walimtengenezea tuhuma kuwa ni gaidi na hatari kwa taifa. Walitaka wananchi waogope kumchagua, lakini historia ilimhukumu kwa haki, na leo anaheshimika duniani.

✅ Barack Obama (Marekani)

Wakati akiwania Urais, wapinzani wake walieneza uongo kwamba hakuwa Mmarekani halisi, na alikuwa Mwislamu wa itikadi kali. Lengo lilikuwa kumfanya Wamarekani wamuogope na kumpinga. Hata hivyo, ukweli ulisimama, na akawa Rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

✅ Uhuru Kenyatta (Kenya)

Kabla ya uchaguzi wa 2013, wapinzani wake walimhusisha na kesi ya ICC kwa madai ya kupanga vurugu za 2007/08, lakini baadaye ushahidi haukupatikana. Lengo lilikuwa kumzuia asiwe Rais wa Kenya.

Mbinu zote hizi zinatumika sasa dhidi ya Dkt. Mwigulu Nchemba – kwa sababu ni mwanasiasa anayewatia hofu wapinzani wake, ndani na nje ya chama chake.

KWA NINI WANAMCHAFUA DKT. MWIGULU NCHEMBA?

Ripoti zote za CAG, PAC, na LAAC hazijawahi kumtaja kwenye ufisadi.

Hana skendo yoyote ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Hajawahi kufutwa kazi kwa utovu wa nidhamu.

Kwa kuwa hawana chochote cha kweli cha kumshambulia, wameamua kutengeneza uongo kwa lengo moja tu – kumfanya aonekane mchafu kwa wananchi na chama chake.

Dkt. Mwigulu amekuwa Waziri wa Fedha aliyefanikisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha juu.

Ametekeleza nia ya Rais Samia Suluhu ya kuongeza mapato ya serikali, kudhibiti mfumuko wa bei, ambavyo vimeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Ni msomi mwenye PhD ya Uchumi, mwenye uwezo wa kuchambua sera za fedha na kuhakikisha taifa linakuwa imara kiuchumi.

Kwa wapinzani wake, ukweli huu ni tishio kubwa – hivyo wameamua kutumia mbinu za propaganda na siasa chafu.

Historia imetufundisha kuwa wanasiasa wa kweli wanaweza kuchafuliwa kwa muda mfupi, lakini ukweli huibuka hatimaye. Leo hii, Dkt. Mwigulu Nchemba anashambuliwa kwa sababu moja tu , Kiongozi Jasiri na tishio kwa wapinzani

➡ Hatuwezi kuruhusu siasa chafu kuficha ukweli wa utendaji wake bora.
➡ Tutaendelea kusimama na viongozi waadilifu wanaoleta maendeleo kwa Taifa letu.
➡ Tanzania inahitaji uongozi thabiti, si siasa za uongo na hila.
Wakati mwingine wanaweza wakawa siyo wapinzani wanao-engineer move za namna hii. Uwezekano mkubwa pia ni kwamba kuna kakikundi fulani ka watu wachache ambako kanadhani kalishachukua hati miliki ya nchi hii, na ambako kana mpango wa kutawaza Rais wake; hili pia usilisahau

Kwa mtizamo wangu mimi, kikundi hicho ndiyo kilimjeruhi TL, kumchioganisha na Serikali iliyokuwa madarakani

TL hakujeruhiwa na Serikali kwa sababu ingekuwa Serikali, risasi moja tu ilikuwa inatosha na si kumjeruhi tu

TL pia hakujeruhiwa na wapinzani wenzake; kwa hiyo mpaka hapa changanya na za kwako sasa

2030 huyu mtu ni potential Candidate kwa nafasi ya Urais, pamoja na huyu Katibu Mkuu wa Chama wa sasa

Come 2030, uhakika ni kuwa mmojawapo wa wawili hawa ndiyo successor wa mama,
 
mwigulu nchemba kwa majaaliwa ya mwenyezi Mungu ndiye next president of the United republic of tanzania piga kazi waziri wangu wa fedha
 
Wakati mwingine wanaweza wakawa siyo wapinzani wanao-engineer move za namna hii. Uwezekano mkubwa pia ni kwamba kuna kakikundi fulani ka watu wachache ambako kanadhani kalishachukua hati miliki ya nchi hii, na ambako kana mpango wa kutawaza Rais wake; hili pia usilisahau

Kwa mtizamo wangu mimi, kikundi hicho ndiyo kilimjeruhi TL, kumchioganisha na Serikali iliyokuwa madarakani

TL hakujeruhiwa na Serikali kwa sababu ingekuwa Serikali, risasi moja tu ilikuwa inatosha na si kumjeruhi tu

TL pia hakujeruhiwa na wapinzani wenzake; kwa hiyo mpaka hapa changanya na za kwako sasa

2030 huyu mtu ni potential Candidate kwa nafasi ya Urais, pamoja na huyu Katibu Mkuu wa Chama wa sasa

Come 2030, uhakika ni kuwa mmojawapo wa wawili hawa ndiyo successor wa mama,
January au Emanuel
 
Katika kila zama za siasa, kuna wanasiasa wachache wenye dira, msimamo, na rekodi safi ambao wanapopata umaarufu na kuwa tishio kwa wapinzani wao, huanza kushambuliwa kwa propaganda chafu, uvumi na hila ili kuwaharibia taswira yao kwa umma. Leo hii, Tanzania inashuhudia smear campaign ya wazi dhidi ya Dkt. Mwigulu Nchemba, Mwanasiasa mwenye rekodi safi, mwenye mchango mkubwa kwa nchi katika ujenzi wa kiuchumi na kiutawala, na ambaye bila shaka anaonekana kuwa endapo atatiania 2030 atakuwa tishio kubwa sana kwa maadui zake.

Kampeni hii inayofadhiliwa na genge la wapinzani wake wa ndani na nje ya chama chake, wakitumia mitandao ya kijamii na gazeti la mtandaoni lililoanzishwa kwa lengo moja tu – kumchafua. Wanatumia kila njia kumhusisha na ufisadi, pasipo hata punje moja ya ushahidi, huku wakipuuzia ripoti rasmi za CAG, Kamati ya PAC na LAAC ambazo hazijawahi kumtaja katika kashfa yoyote ya kifisadi.

Mwigulu ni kijana aliekuzwa vyema na Chama, kuanzia kuwa Rais wa Wachumi Vyuo Vikuu vinavyofundisha uchumi nchini, Mbaraza wa UVCCM, Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa, Mchumi wa CCM Taifa, Naibu wa Fedha, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Katiba, na sasa Waziri wa Fedha. Uzoefu huu unawatisha wapinzani wake, kwani wanajua wazi kuwa amejengwa na Chama kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Taifa siku za usoni.

Huu sio mchezo mpya katika siasa – ni mbinu iliyotumiwa kwa miaka mingi duniani kote dhidi ya viongozi waadilifu wenye nafasi kubwa ya kushinda madaraka.

Haya yanayomkumba Dkt. Mwigulu Nchemba sio ya kipekee kwa Tanzania pekee, bali ni mkakati wa kawaida wa siasa chafu duniani kote.

✅ Nelson Mandela (Afrika Kusini)

Kabla ya kuwa Rais, wapinzani wake walimtengenezea tuhuma kuwa ni gaidi na hatari kwa taifa. Walitaka wananchi waogope kumchagua, lakini historia ilimhukumu kwa haki, na leo anaheshimika duniani.

✅ Barack Obama (Marekani)

Wakati akiwania Urais, wapinzani wake walieneza uongo kwamba hakuwa Mmarekani halisi, na alikuwa Mwislamu wa itikadi kali. Lengo lilikuwa kumfanya Wamarekani wamuogope na kumpinga. Hata hivyo, ukweli ulisimama, na akawa Rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

✅ Uhuru Kenyatta (Kenya)

Kabla ya uchaguzi wa 2013, wapinzani wake walimhusisha na kesi ya ICC kwa madai ya kupanga vurugu za 2007/08, lakini baadaye ushahidi haukupatikana. Lengo lilikuwa kumzuia asiwe Rais wa Kenya.

Mbinu zote hizi zinatumika sasa dhidi ya Dkt. Mwigulu Nchemba – kwa sababu ni mwanasiasa anayewatia hofu wapinzani wake, ndani na nje ya chama chake.

KWA NINI WANAMCHAFUA DKT. MWIGULU NCHEMBA?

Ripoti zote za CAG, PAC, na LAAC hazijawahi kumtaja kwenye ufisadi.

Hana skendo yoyote ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Hajawahi kufutwa kazi kwa utovu wa nidhamu.

Kwa kuwa hawana chochote cha kweli cha kumshambulia, wameamua kutengeneza uongo kwa lengo moja tu – kumfanya aonekane mchafu kwa wananchi na chama chake.

Dkt. Mwigulu amekuwa Waziri wa Fedha aliyefanikisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha juu.

Ametekeleza nia ya Rais Samia Suluhu ya kuongeza mapato ya serikali, kudhibiti mfumuko wa bei, ambavyo vimeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Ni msomi mwenye PhD ya Uchumi, mwenye uwezo wa kuchambua sera za fedha na kuhakikisha taifa linakuwa imara kiuchumi.

Kwa wapinzani wake, ukweli huu ni tishio kubwa – hivyo wameamua kutumia mbinu za propaganda na siasa chafu.

Historia imetufundisha kuwa wanasiasa wa kweli wanaweza kuchafuliwa kwa muda mfupi, lakini ukweli huibuka hatimaye. Leo hii, Dkt. Mwigulu Nchemba anashambuliwa kwa sababu moja tu , Kiongozi Jasiri na tishio kwa wapinzani

➡ Hatuwezi kuruhusu siasa chafu kuficha ukweli wa utendaji wake bora.
➡ Tutaendelea kusimama na viongozi waadilifu wanaoleta maendeleo kwa Taifa letu.
➡ Tanzania inahitaji uongozi thabiti, si siasa za uongo na hila.
Nilidhani utajibu shutuma anazotuhumiwa nazo,badala ya kumpamba.😂
 
Hakika Dr.Mwigulu L.Nchemba ni mtu na nusu!
Kwa tunaomjua huyu ni Bingwa wa Uchumi na hesabu!
Uliza mtu yeyote aliyesoma Ilboru - Arusha na Mazengo High School- Dodoma.
Mtafuteni Professor Osoro au Dr. Ndashau pale University of Dar es Salaam wawambie nini Dr.Mwigulu alifanya pale UDSM.
Huyo ndiye Overall Best Student wa Mwaka wake katika kozi ya Uchumi.
Mwigulu ni mwadilifu,mnyenyekevu na hana makuu Kijana kutoka jamii ya kifugaji.
Dr.Mwigulu is one of the Best Economics brain we have as the Country at the moment.
Huyu aliyeshindwa kujieleza bungeni?
Hakuna mchumi hapo ni mchumia tumbo period!
Hivi niulize nani alimruhusu kuweka signature yake kwenye pesa yetu? Tutaitoa

IPO siku ipo siku hawa watalia Kilio cha kusaga meno!

Tutairudisha nchi mikononi mwa wananchi wenye nchi kutoka mikononi mwa walafi na wenye uchu wa madaraka.

Upinzani kemeeni haya mnayosikia mnayosoma kwa sauti kuu.

Kuitisha vyombo vya habari kusudi kubwa ni kuongea haya ya kupinga na kuishinikiza serikali kususpend wa chafu wezi sio kuongea petty petty issues. Sijui tunapokea waliohama sijui Sugu(mtakatishaji mwingine Huyu kupitia ex oh sorry mama mtoto) kashuka kwenye gari sijui tutawatoa madarakani.

Msiwaze vyeo wazieni watoto wenu na vizazi vijavyo.

Kuweni serious!
 
Kanda ya kati sijui mnashida gani...?!

Lazaro Nyarandu aliwahi kusema yeye ndiye chaguo la Marekani awe Raisi wa Tanzania...?!

Kwahiyo alidhani Raisi wa Tanzania anachaguliwa na Marekani au watanzania?!

Nyarandu akapotea kama upepo! Sasa bado huyu . Mwigulu Lameck Nchemba, kiukweli, huyu jamaa haaminiki, watanzania hawana imani nae hata chembe, anatuhuma nyingi sana za ufisadi, upigaji, ubinafsi, kujilimbikizia mali, dharau, jeuri, kiburi na majibu ya kuwadhihaki watanzani, aliwahi kusema asiyetaka ahamie burundi, maadamu yeye mwanae anasoma fedha ada milion saba mliobaki mtatijua wenyewe!! Huyu madilu systeme ana utafuta Uraisi kwa udi na uvumba!

Baba wa taifa alishawahi kusema "ukimuona mtu anautafuta uongozi kwa gharama yoyote basi mtu huyo ni wakumuogopa kama ukoma!"
 
Honest opinion, kati ya serikali ya mama sasa, Mwigulu ndo yupo prepared 2030 kuliko wengine.

Sioni figure ingine ya uraisi zaidi yake.

Wengine akina Makamba na Nape walikuwa na mwelekeo ila wameshapotezwa au wamejipoteza
Ila watanzania hatuko serious aisee.!!
Nape awe rais? Dah!!

Mimi nilitamani January angechukua fomu wapambane na Lissu majukwaani..!!
 
Shida ya Nyie wakina Mwigulu sijui nan? Wabinafsi sana tunaweza tukawapa kura na kuwasifia humu mnakula peke yenu embu pambana mwenyewe kujisafisha
 
Hakika Dr.Mwigulu L.Nchemba ni mtu na nusu!
Kwa tunaomjua huyu ni Bingwa wa Uchumi na hesabu!
Uliza mtu yeyote aliyesoma Ilboru - Arusha na Mazengo High School- Dodoma.
Mtafuteni Professor Osoro au Dr. Ndashau pale University of Dar es Salaam wawambie nini Dr.Mwigulu alifanya pale UDSM.
Huyo ndiye Overall Best Student wa Mwaka wake katika kozi ya Uchumi.
Mwigulu ni mwadilifu,mnyenyekevu na hana makuu Kijana kutoka jamii ya kifugaji.
Dr.Mwigulu is one of the Best Economics brain we have as the Country at the moment.
Mhmm.!! Ajabu ya Bakari kujiita Beka ndio haya sasa!! 😹
 
Mwigulu hawezi kuja kuwa Rais wa Tanzania kamwe. Niko pale niite mbwa kama tutakuwa wote hai mwaka 2030.

Hana uwezo huo, labda awe Rais wa mawe
Niliitafuta hii comment, 😂😂😂😂
 
Hivi huyu Madelu bado ana uwaza Urais? Hajifunzi tyuh? Ataishia kuwa wa mawe tena.
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom