PreGE2025 Siasa chafu dhidi ya Mwigulu ni woga wa 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
fumadilu = madelu , madelu=mwigulu
 
Hatuna mashaka na elimu yake. Si Ni yake bhana. Sisi hatumuelewi kwa suala moja kubwa la kutetea wabadhilifu kwa nguvu zote eti kwa sababu tu ni watu wa chama chake, alafu eti unataka mtu Kama huyo tumuamini kweli.
 
Hapa sifa zote ningezikubali kama angeweza kupaisha thamani ya pesa yetu..shilingi ya Tanzania inashuka kwa speed kubwa sana ukilinganisha na majirani zetu. Ilipanda kwa miazi miwili tukapata ahueni ila naona imerudi kulekule chini ilipokuwa...
 
Wakati mwingine wanaweza wakawa siyo wapinzani wanao-engineer move za namna hii. Uwezekano mkubwa pia ni kwamba kuna kakikundi fulani ka watu wachache ambako kanadhani kalishachukua hati miliki ya nchi hii, na ambako kana mpango wa kutawaza Rais wake; hili pia usilisahau

Kwa mtizamo wangu mimi, kikundi hicho ndiyo kilimjeruhi TL, kumchioganisha na Serikali iliyokuwa madarakani

TL hakujeruhiwa na Serikali kwa sababu ingekuwa Serikali, risasi moja tu ilikuwa inatosha na si kumjeruhi tu

TL pia hakujeruhiwa na wapinzani wenzake; kwa hiyo mpaka hapa changanya na za kwako sasa

2030 huyu mtu ni potential Candidate kwa nafasi ya Urais, pamoja na huyu Katibu Mkuu wa Chama wa sasa

Come 2030, uhakika ni kuwa mmojawapo wa wawili hawa ndiyo successor wa mama,
 
mwigulu nchemba kwa majaaliwa ya mwenyezi Mungu ndiye next president of the United republic of tanzania piga kazi waziri wangu wa fedha
 
January au Emanuel
 
Nilidhani utajibu shutuma anazotuhumiwa nazo,badala ya kumpamba.πŸ˜‚
 
Huyu aliyeshindwa kujieleza bungeni?
Hakuna mchumi hapo ni mchumia tumbo period!
Hivi niulize nani alimruhusu kuweka signature yake kwenye pesa yetu? Tutaitoa

IPO siku ipo siku hawa watalia Kilio cha kusaga meno!

Tutairudisha nchi mikononi mwa wananchi wenye nchi kutoka mikononi mwa walafi na wenye uchu wa madaraka.

Upinzani kemeeni haya mnayosikia mnayosoma kwa sauti kuu.

Kuitisha vyombo vya habari kusudi kubwa ni kuongea haya ya kupinga na kuishinikiza serikali kususpend wa chafu wezi sio kuongea petty petty issues. Sijui tunapokea waliohama sijui Sugu(mtakatishaji mwingine Huyu kupitia ex oh sorry mama mtoto) kashuka kwenye gari sijui tutawatoa madarakani.

Msiwaze vyeo wazieni watoto wenu na vizazi vijavyo.

Kuweni serious!
 
Kanda ya kati sijui mnashida gani...?!

Lazaro Nyarandu aliwahi kusema yeye ndiye chaguo la Marekani awe Raisi wa Tanzania...?!

Kwahiyo alidhani Raisi wa Tanzania anachaguliwa na Marekani au watanzania?!

Nyarandu akapotea kama upepo! Sasa bado huyu . Mwigulu Lameck Nchemba, kiukweli, huyu jamaa haaminiki, watanzania hawana imani nae hata chembe, anatuhuma nyingi sana za ufisadi, upigaji, ubinafsi, kujilimbikizia mali, dharau, jeuri, kiburi na majibu ya kuwadhihaki watanzani, aliwahi kusema asiyetaka ahamie burundi, maadamu yeye mwanae anasoma fedha ada milion saba mliobaki mtatijua wenyewe!! Huyu madilu systeme ana utafuta Uraisi kwa udi na uvumba!

Baba wa taifa alishawahi kusema "ukimuona mtu anautafuta uongozi kwa gharama yoyote basi mtu huyo ni wakumuogopa kama ukoma!"
 
Honest opinion, kati ya serikali ya mama sasa, Mwigulu ndo yupo prepared 2030 kuliko wengine.

Sioni figure ingine ya uraisi zaidi yake.

Wengine akina Makamba na Nape walikuwa na mwelekeo ila wameshapotezwa au wamejipoteza
Ila watanzania hatuko serious aisee.!!
Nape awe rais? Dah!!

Mimi nilitamani January angechukua fomu wapambane na Lissu majukwaani..!!
 
Shida ya Nyie wakina Mwigulu sijui nan? Wabinafsi sana tunaweza tukawapa kura na kuwasifia humu mnakula peke yenu embu pambana mwenyewe kujisafisha
 
Mhmm.!! Ajabu ya Bakari kujiita Beka ndio haya sasa!! 😹
 
Mwigulu hawezi kuja kuwa Rais wa Tanzania kamwe. Niko pale niite mbwa kama tutakuwa wote hai mwaka 2030.

Hana uwezo huo, labda awe Rais wa mawe
Niliitafuta hii comment, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hivi huyu Madelu bado ana uwaza Urais? Hajifunzi tyuh? Ataishia kuwa wa mawe tena.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…