Siasa inalipa!! Angalia unaodaiwa kuwa utajiri wa Baraza la Mawaziri Kenya!

Asante kwa taarifa, vipi hapa kwetu? Lakini Kama siasa Hakuna pesa kwa nini matajiri wanahonga ili wawe wanasiasa?
Mkuu nikusaidie kidogo ,kenya hakuna anaeenda kwenye siasa akiwa maskini,makamu wa rais kenya yule ni tajiri kama bakhresa ile nchi ya kibepali kuwa tajiri ni kigezo pia kukupa kura
 
Bado hujaeleweka mkuu. Hao uliowataja wameteuliwa kuwa mawaziri kwa sababu ni mabilionea au wamepata mabilionea baada ya kuwa mawaziri?

Ninachokijua mimi, Kenya huteuwa mawaziri wake nje ya wabunge. Sasa tueleze kuna kapuku gani ameteuliwa kuwa waziri na kisha kujitajirisha na mali za wananchi wa Kenya. Au unaongelea bongo lala
 
Ushawahi kujiuliza wanasiasa mfano mawaziri wana utajiri kiasi gani? Je unajiuliza kwanini matajiri wakubwa duniani wanaingia kwenye siasa? Siyo nchi za kiafrika tu, hata Ulaya?Fuatana nami nikupe uhondo!

Hivi majuzi Rais wa Kenya William Ruto aliteua majina ya mawaziri wateule, hii ni baada ya kuvunja baraza la mawaziri kufuatia maandamano ya GEN Z mwezi uliopita.

Katika utaratibu wa kawaida, wateule hufanyiwa usaili, ambapo pamoja na mambo mengine walihojiwa juu ya utajiri wao!

Angalia hapa
1.Dr Andrew muhuia Ksh 214 Milioni, hii ni zaidi ya bilioni 4.28 za kitanzania
2.Aden Duale Ksh 980 Milioni zaidi ya shilingi Bilioni 19.6 za Kitanzania
3.John Mbadi Ksh 380 Milioni zaidi ya Shilingi za kitanzania 7.6 Bilioni
5.Davis Chirchir Ksh 509 Milioni zaidi ya Shilingi za kitanzania 10.14 Bilioni
6.Joho Ksh 2.5 billion, hii ni zaidi ya Bilioni 50 za kitanzania

Ukiangalia baraza hilo la mawaziri mwenye pesa kidogo kuliko wote anaitwa Eric Muga utajiri wa Ksh 31 Million zaidi ya Shilingi za kitanzania Milioni 620.

Hii inakupa picha gani? Je tuanzishe utaratibu huu hapa Tanzania kuhojii mali za viongozi ?

MWANAO MTAFUTIE KADI YA VYAMA VYA SIASA 😀😀KUNA PESA NDEFU!
Kwani ile tume ya maadili ya viongozi wa umma hawana hizo taarifa ama ndio sirikali?
 
Asante kwa taarifa, vipi hapa kwetu? Lakini Kama siasa Hakuna pesa kwa nini matajiri wanahonga ili wawe wanasiasa?
Mkuu siasa ina toa
1.kupata taarifa za ndani za serikali ikiwemo wapi vitajengwa vyuo ,wawekezaji wataweka wapi miradi hivo fasta unawahi viwanja
2.Power: matajiri nje ya siasa ni watu wa kawaida .ila akiwa senator hata akosee anatendewa kwa heshima .pià anapata nguvu ya kutumia dola kwa maslahi yake
3.tender :akiwa ndani ni rahisi kuzipata kuliko akiwa nje itabidi atoe rushwa kubwa
4.umaarufu.tajiri bila umaarufu ni kama mke bila mtoto.kuna raha ya kutokea mahali watu wengi wanakujua ,sasa mfano arusha kuna mitajiri ya kutisha ya madini na haijasoma ,huwa hata wakimuona dullyskes wanamshangaa yaan ile hali kaja baa watu wote wanamfata huwa heshima kuu.
5.connection ; ukikalia ofisi ya umma unaweza msogelea na kujuana na mkuu yeyote sasa mtu kama nape nauye na ukapuku wake fikilia ameshawahi kaa meza moja na elon musk .waza mbowe bila siasa angesalimiana lini na marais mbalimbali
 
Umeandika vizuri mkuu! Nimependa 1,2,3 na 5 wanasiasa wanaishi maisha Fulani ya hadhi ya juu ukilinganisha na wafanyabiashara wa kawaida
 
Kwani ile tume ya maadili ya viongozi wa umma hawana hizo taarifa ama ndio sirikali?
Yani unaipa serikali kazi ya kuichunguza 😄😄😄Tume ikipata majibu inaripoti kwa nani? Je ataweza kuchukua hatua dhidi ya aliyemteua?
 
Bado hujaeleweka mkuu. Hao uliowataja wameteuliwa kuwa mawaziri kwa sababu ni mabilionea au wamepata mabilionea baada ya kuwa mawaziri?

Ninachokijua mimi, Kenya huteuwa mawaziri wake nje ya wabunge. Sasa tueleze kuna kapuku gani ameteuliwa kuwa waziri na kisha kujitajirisha na mali za wananchi wa Kenya. Au unaongelea bongo lala
Nimekwambia kwenye baraza la mawaziri Kenya mwenye utajiri mdogo ana Milioni 620,kwa kuwa hata hapa kwetu ni majirani huoni kwamba siasa inalipa mkuu?
 
Umeandika vizuri mkuu! Nimependa 1,2,3 na 5 wanasiasa wanaishi maisha Fulani ya hadhi ya juu ukilinganisha na wafanyabiashara wa kawaida
So kutajirika ni jambo moja ,kuulinda ni topic nyingine ,usione wanasiasa wanatoa sadaka kanisani ,ni kwamba kuwa na hela kwa siri ni mateso ,askari watakuwinda daily na kukuchomoa hela ,dawa ni unatafuta ukaribu na wakubwa wao mfano unajenga kituo cha polisi unakabidhi jeshi na hotuba juu wote wanakuona kwa tv unacheka na IGP.Unadhani kuna kapolisi ka kukugusa?

kuna baa ilikuwa Inashindwa kodishwa sababu aliemiliki alikuwa anagawa sana hela polisi .
Mm nkapachukua na kupakarabati siku ya uzinduzi nkaalika rpc na rso .baada ya wiki wakaja usiku kukagua vibali na kusumbua nkawa nshatoa maagizo warekodiwe ,nkaitisha kikao kwa mkuu wa mkoa na kuweka ila footage wakiomb rushwa.
Hawakuwahi sogea ila mm kwa hiali nkawaambia gari ya patrol kila siku ichukue elfu 30 kaunta ijumaa hadi jumapili=90k ,na rpc nkawa nampa 500 kila mwisho wa mwezi nilipiga hela miaka 7 .so kaka inamaana ngetaka yote yaishe ni kugombea udiwani tu ,rpc akileta zake napendekeza ahamishwe vikao vya ccm mkoa anaufyata
 
Mkuu uko vizuri! Kusema kweli pesa si kitu mbele ya power! Kulinda utajiri ni kazi kuliko kuutafuta. Ukikosana na Serikali unaweza kushushwa siku chache tu, mfano mzuri Mh Manji
 
Kumbe kumiliki gari na nyumba ni matokeo ya siasa kulipa?
Mawazo ya kimaskini sana haya!
Mkuu, kuna watu wako UVCCM hawana ramani ya kueleweka ila akishalamba uteuzi utamsahau ndani ya miaka 5
 
Back
Top Bottom