Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Hakuna sheria inayokataza kubeba bango la kupinga kitu fulani na mimi nikuulize swali fikiria mashabiki wa simba waende misri na bango la kuunga mkono wapalastine. Humanity has no Boundary
Wewe Ukitaka kuwaelewa FIFA kuwa hawataki mpira uchanganywe na siasa, basi waambie viongozi wa serikali wamuondoe Karia madarakani.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mtu alitoa uzi juu ya maandamano ya kuwaunga mkono wapalestina, ngoja waende Misri Kama wataona hayo mabango. Wamasai wanafukizwa Loliondo hatujawahi kuona mabango.
 

Mnajitesa sana jamani, kwani hilo bango limeandika nini cha ajabu au usaidiwe tafsiri?
Kwanza nikupe tu taarifa: Palestina hawaja piga Waisrael kama propaganda zinavyoendeshwa; kilichotokea ni waasi (Hamas) ndio waliopiga Israel sasa Israel Inasaidiwa na Wamarekani kuipiga Palestina na kuua raia na watoto wasio na hatia..Shame!!!
 
Umeona game ya liver leo?
 
Huenda sheria zilishabadilishwa ndo maana game zote za La Liga pale juu kuna bendera ya Ukraine ila pia Russia kapigwa ban kushiriki mashindano yoyote ya Fifa na Uefa kwa sababu hizo hizo za kisiasa.
 
Mpumbavu udini unakusumbua kazuie namechi ya liver v everton
 
Ngassa na Dumayo je ni wa wapi ?
Singano je ?
 
Azam hata viwanda vyake anaangalia majina ya ,Hamis, Hassan ,
 
Hakuna kosa lolote hapo. Labda unaendeshwa na mapenzi binafsi tu. Kama hao jamaa kwenye bango lao wameonesha kuwa Pamoja na Palestina kitu ambacho w na watu wako hampendi, basi andika na ww bango lako kubwa uisapoti Israel, inakuwa imeisha. Hakuna haja ya maneno mengi.
 
AZAM ni wadini sana, nshasema AZAM hawana ETHICS za habari. Matangazo yao yapo kidini zaidi na sijajua kwanini Wasirivoke leseni yao ya matangazo kutoka kuwa chombo cha habari cha kijamii SECULAR na kuwa cha kidini non SECULAR.
Hata haya makasiriko yako na huyo mtoa mada pia yamejiegesha kwenye mlengo huo huo wa kidini ila hamko wazi tu. Shida yenu ji watu kuonesha kuiunga mkono Palestina. Me nashauri na wewe sema ama andika bango lako uisapoti Israrl, mbona simple tu.
 
Huko kwenye Vita vya Ukraine na Russia watu wanaandika mabango makubwa Ulaya na hadi wanaweka nenmbo za Kuisapoti Ukraine na kuilani Urusi, yanaoneshwa na Channel zote za Sports duniani, Supersport, Sky sports etc, ila mtu akiandika bango lake la khmsapoti Mparestina ndio unaona haluna weredi na mapovu kibao yanakutoka. Acheni uzwazwa. Huwezi kumpangia mtu amsapoti nani mahali penye mgogoro. Muhimu nawe kama una impact msapoti umtakaye. Azam sio wa kwanza kuonesha mabango
 
Ni kweli waliingia na Bango lakini Kilichiwakuta kutoka kwa Mashabiki Wamejuta kutaka kuutumia Mchezo wa Simba Kueneza Mambo waliyoyataka wenyewe. Walielezwa Ujumbe huo hatuutaki labda Waupeleke Israel Kuomba Msamaha maana wao ndiyo waliowachokoza. Sema Hakuna Crip hapa ila Walipigwa ile Mbayaaaa na ilikua ni aibu kubwa kwao
 
Lakini Bongo tumesema hatuutaki Ujinga wao. Ukarine Kidogo unaweza kuwatetea hawakuipiga Urusi ila walionesha dharau kwa Urusi lakini Hamasi walienda Kuwapiga Waisreal kwenye Ardhi yao. Sasa hapo Wakutetewa sahihi ni yupi kati ya Israel na Parestine. Infact: Wakutetewa na kuungwa Mkono ni Israel maana ndiye aliyeonewa lakini cha Kupingwa ni Vita inayoendelea na siyo kuungana na Mkorofi.
 
Wewe Ukitaka kuwaelewa FIFA kuwa hawataki mpira uchanganywe na siasa, basi waambie viongozi wa serikali wamuondoe Karia madarakani.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Unajadili hii mada kwa kujifungia ndani ya box ungepanua ubongo wako usingeniuliza hilo swali. Nikujibu tu kuwa aliyekua rais wa FIFA kabla ya huyu akiitwa sepp blatter aliwahi kukamatwa na serikali ya marekani kwa tuhuma za rushwa na kufunguliwa mashtaka.
 
We jamaa akili hakuna kichwani kwako kabisa,umeshindwa kutaja hizo sheria za FIFA zilizovunjwa,weka hizo sheria.

Pia inaonesha hujui kinachoendelea duniani,mfano ligi ya Hispania wao Laliga 'wanaisapoti' Ukraine [emoji1255] na wala hujawasikia hao FIFA wakinena lolote.Kwa hali ilivyo sasa huko Gaza hayo ni matukio ya kawaida.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…