Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Ukishindwa kutumia busara katika kunadi sera zako wakati kampeni basi tumia utimamu kuangalia maneno unayozungumza. Ni hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa wakiingia katika kiwango cha ujinga na upumbavu kwa kutumia maneno ya dhihaka dhidi ya imani za kidini, hasa Ukristo, ili kumfurahisha mgombea Urais au kuonekana waaminifu kwa upande fulani wa kisiasa.
Kitendo hiki si tu kwamba ni cha upuuzi, bali pia kinadhalilisha misingi ya heshima na mshikamano wa kijamii. Na kinaonesha uwezo mdogo wa fikra ya uongozi haswa kwa chama kama CCM.
Kwa nini mwanasiasa aone ni busara kubeza imani ya wakristo? Je, kuna faida ipi ya kisiasa inayoweza kuzidi maumivu ya kisaikolojia na kiroho anayoyasababisha kwa waumini hao? Ukweli ni kwamba hakuna faida yoyote. Badala yake, anajijengea picha ya kiongozi asiyeheshimu watu na asiye na busara wala utimamu wa akili. Katika jamii yenye mchanganyiko wa kidini kama Tanzania, kutumia imani kama chombo cha kejeli ni sawa na kuchezea kaa la moto.
Kanisa, kama taasisi yenye nafasi kubwa katika malezi ya maadili ya kitaifa, halipaswi kukaa kimya. Ni wajibu wa viongozi wa dini kuzungumza kwa uwazi na kukemea matamshi ya aina hii, bila kuogopa majina au vyeo vya wanasiasa husika. Ukimya wao unaweza kutafsiriwa kama ridhaa, na kwamba wameunga mkono kauli za kijinga namna hii.
Aidha, ni lazima tuweke mipaka kati ya siasa na dini. Imani ni kitu kitakatifu, ni chombo cha kujenga utu na mshikamano sio dhihaka na uchawa wa kipumbavu. Siasa ni medani ya ushindani wa fikra na sera na kama hauna sera baki nyumbani na wajukuu uwalee. Kuchanganya viwili hivi kwa matusi na dhihaka ni kuvunja heshima ya taifa.
Kwa mtazamo wangu, hata kama mtu sio Mkristo, ni wajibu wa kila raia kukataa dhihaka dhidi ya imani yoyote. Taifa linalodharau dini ni taifa linalojipeleka shimoni. Wanasiasa waelewe: kura hupatikana kwa heshima, si kwa kejeli.
THIS IS A VERY BIG NO 👎