Siasa na michezo

Siasa na michezo

DMmasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
561
Reaction score
900
Salaam waungwana,

Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wenye mamlaka kuingilia michezo mbalimbali.

Sote tutakubaliana tangu 2015 tunayo aina ya viongozi ambao katika kila jambo wanaelekeza sifa na shukrani kwa raiya namba moja.

Juzi wakati nasikiliza michezo waziri aliyepo kwenye hii wizara alikuwa anamwaga sifa zote kwa raiya namba moja yakwamba kwa juhudi zake tumepeleka timu mbili robo fainali nikasema hii ni mulemule sifia ubakie.

Sasa jana katibu wa CHANETA kasikika akilalama serikali haiwasapoti na kuna kipindi walitakiwa kwenda kwenye mashindano maswala ya shekeli yakaleta shida. Wakati huu tena wanapaswa kwenda South Africa kwenye mashindano shekeli ni tabu tena.

Kwa kuyatamka hayo katibu wa CHANETA ameonekana tope kwenye airforce nyeupe ya bishoo, kaonekana Yuda mbele ya wakristo, kaonekana jiwe kwenye tonge la wali.

Naam ameshushiwa robota la dhambi na amepaswa kuwajibika kaitwa kamati ya nidhamu na waziri anasema kunapesa zilikuwa zimeelekezwa kwenye netball zisitishwe.

Moja kwa moja niliyoyabeba ni yapi

1. Ukitaka kubaki mwenyewe simama kwenye ukweli (hii ameimba ata Luck dube ) wakati huu kila mtu ameonekana yuko upande wa waziri ata watangazaji walifanya namna kusakafia katibu haonekane kutu kwenye chuma.

2. Cha muhimu sana nikusifia siyo kukosoa au kusema ukweli

3. Waziri alionekana kuvurugwa sana na hili swala. Kwanini? na alisema "niwaambieni ukweli zile pesa za hamasa azikutumika ata kwenye Afcon"

Karibu kwetu
Jisikie uko kwenu
 
Back
Top Bottom