Sijui kwanini watanzania tunapenda ku-invest emotions kwa watu tusiowajua at personal level. Huu ndio msingi unakuta unampenda mtu au unamchikia mtu ambae yeye hakujui kabisa.
Binafsi nilikuwa namkubali sana Magufuli not necessary at personal level, isipokuwa kwenye nidhamu, maendeleo na values zake Tanzania ni nchi ya wote kila mtu apate haki.
Lakini sikuwahi kuwa na personal issues na hao mapoyoyo wawili (wawepo wasiwepo serikalini sikosi usingizi) zaidi ya kuwaona wajinga tu kudhani kumnanga Magufuli kunamjengea bi-tozo.
Watanzania hasa wakipato cha chini kikubwa kwao kwa Magufuli nchi ilikuwa ya haki na mizinguo ya rushwa ukienda ofisi za serikali kupata huduma ilipungua sana.
Sasa kumtoa Makamba na Nape hakubadilishi tabia mbaya iliyorudi baada ya Magufuli na sidhani kama wananchi wengi wasioshinda mitandaoni wanajali hao watu wawe mawaziri au la, wanachotaka ni yao yaende kama umeme wa uhakika, maji, kutowekewa mitozo kila kukicha.
Hao wametumbuliwa kwa sababu za raisi mwenyewe sio kwa sababu ya kufurahisha kundi.
Huyo Mombo Selemani na Emmanuel Nchimbi washafanya kazi pamoja Brazil. Chances are bwana Selemani kuikwaa hiyo post ya DG wa labda kuna influence ya Nchimbi kutaka kujua nani hatari kwa Samia, feedback ya haraka haraka imekuja na hao watu wawili.