Siasa Tanzania ni ngumu sana kwa wazalendo na wapenda maendeleo, mabadiliko ya kifikra ni muhimu sana

Siasa Tanzania ni ngumu sana kwa wazalendo na wapenda maendeleo, mabadiliko ya kifikra ni muhimu sana

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Ni ngumu sana kutetea wananchi ambao utatekwa, utateswa, utapotea au utapigwa risasi wao hawatambui mchango wako wataendelea kupiga kelele nyuma ya keyboards na story za Simba na Yanga.

Anajitokeza mtu mzalendo anaibua ufisadi na kufanya maendeleo kesho anaamka mtu anakwambia mtu yule alikuwa mbaya ,au huyu mbaya, watu wengi wanaafiki.

Nchi ambayo watu wakioneshwa pesa tu wako radhi kusifia na kufanya mambo ya ajabu haijarishi hata yatagharimu maisha ya watanzania au ndugu zake.

Hii ndio Tanzania ambayo ina hitaji mabadiliko ya kifikra kuliko nchi yoyote ile watu wathamini mali zao na za nchi, kuwe na utu, uwajibikaji na watu tudai Katiba Mpya.​
 
Nadhani siasa za Tanzania ni nyeyesi na rahisi mno ukilingasha na nchi yoyote Africa Mashariki.

Mabadiliko ya fikra yanaihitaji maudhui mbadala dhidi ya yaliopo, tena bila ya yeyote kujiona bora kuliko mwingine kitu ambacho ndio changamoto kubwa katika siasa duni na rahisi sana za Tanzania.

Uzushi, hisia na huruma vimepewa nafasi kubwa zaidi ambao mara zote unaishia mitandoni tu kwasababu sio halisi.

Kutegemea hisia na huruma kulinda na kutetea haki ni useless mbele ya vyombo hususani vya kisheria kwasababu hakuna pilato asiependa kua kwenye record za hukumu nzuri za haki zitakazotumika kama rejeo za hukumu za kesi nyingine au mifano ya hukumu nzuri za mifano ya kufundishia kwenye Taasisi za kitaaluma.

Wanaharakti wameinfluence siasa ya Tanzania na imekua tepetevu 🐒
 
Back
Top Bottom