Siasa za Afrika zinaharibiwa na watawala walioko madarakani

Siasa za Afrika zinaharibiwa na watawala walioko madarakani

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
16,583
Reaction score
42,992
Siasa za Kiafrika zimejaa hila uhuni mauwaji jinai utekaji hujuma wizi na kila aina ya uovu.

Yaliyotokea Tanzania ndio yanatokea Uganda kwa Museveni.

Somo la historia tunalofundishwa kuwalaani wazungu na ukoloni wao kwetu inabidi tubadili mtaala wake kwasababu viongozi wa Afrika wa sasa ni wabaya kuliko wazungu. Wanapenda ku overstay kwenye madaraka at any cost hata ikibidi kuua.

Haiumi sana ukatili ukifanyiwa na mtu baki ila akikufanyia ndugu wa damu inauma zaidi.

Kuchapwa viboko hamsa vya mkoloni na kufungwa minyororo na hata kukatwa vidole walikofanyiwa babu zetu hakuumi sana kama Risa anazokupiga ndugu yako ili abaki madarakani.

Uganda mwandishi kachapwa risasi mchana kisa yupo kambi ya Bobi Wine. Afrika who Bewitched you?
 
Siasa za Tanzania zimeharibiwa na jiwe.

Nasema uwongo ndugu zangu?
 
Siasa za Tanzania zimeharibiwa na jiwe.

Nasema uwongo ndugu zangu?
Wakati wa utawala wa rais Kikwete, nchi yetu ilipiga hatua kubwa sana kwenye suala la demokrasia na utawala bora

Pamoja na madhaifu yake, rais Kikwete alikuza sana demokrasia nchini...

Ni kweli kulikuwa na matukio ya kutekana na mauaji ,lakini huwezi kulinganisha na awamu ya tano...

Tangu kuanza kwa awam ya tano, siasa za chuki zimezidi mno...

Ukijifanya kumkosoa bwana mkubwa,...unakiona cha mtema kuni.....

Kiufupi siasa za nchi hii zimeharibika sana kwa sababu ya jiwe.
 
Back
Top Bottom