Siasa za awamu ya 5 na ya 6 zinaelekea kudidimiza umoja wa Taifa letu

Siasa za awamu ya 5 na ya 6 zinaelekea kudidimiza umoja wa Taifa letu

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Chama changu Tawala hujinadi kukuza umoja wa Kitaifa lakini kwa awamu hizi mbili ninaona umoja huo unazidi kudidimia. Chama change kinajuhami kupita kiasi hata kwa kuumiza wengine. Hivi ni kweli kabisa tunajaribu kuwaaminisha watu kuwa Mbowe ni Gaidi! INAUMIZA SANA, pamoja na UCCM wangu.
Hivi hofu yote ya nini? Mbona JK na Mkapa waliongoza bila stress ya hoja za upinzani? Hwa watu walijibu hoja. Kumbuka Mkapa kipindi wanadai kahongwa dhahabu - alikuja kwenye media na akajibu vizuri na wala hakugombana au kukamata wapinzani na hata vyombo vya ahabari vilivyoandika alivihoji kwa umaridadi wao wa uandishi kwa kushindwa kufuatilia kwa kina habari hiyo.
CCM kwa sasa tunatumia ubabe na vyombo vya ulinzi kutisha tisha tu. Ukweli hata mimi hata kama sipo kwenye siasa active lakini kinachoendelea kunyanyasa upinzani ninatoka CCM. Wanangu wananihoji maswali amabayo ninashindwa kuyajibu? Mfano jana kanihoji kwa nini Mbowe kakamatwa? Ukweli ninashindwa kuelezea?
Hii chuki inayojengwa dhidi ya upinzani imekithiri kiasi kwamba hata mjinga tu anaweza kuelewa upinzani unafanyziwa kwa sasa. Washauri na wasaidiizi wa Rais huyu ninaamini wengi ni wale waliotoka awamu ya tano ambayo ilikuwa always inajihami kwa kuumiza upinzani. Hawa wanamharibia sana sana sana sana sana sana sana sana sana sana sana sana Rais SSH. Kwa hili wanamtega nalo! Mpaka sasa SSH hajatamka neon lolote kuhusu kukamtwa kwa Mbowe! Lawama zote zitakuja kumwelekea kwake siku za usoni. Mbowe sio GAIDI. Mbowe ameonewa sana huyu Mbowe. Dodoma akina Silinde na Lijualikali walimtumia vijana wakampige then CCM tukasingizia alikuwa amelewa!
Ikiwa bado ni mapema sana - ninazidi kumwomba Rais SSH aangalie washauri wake na wasaidizi wake katika masuala ya siasa - aache kukubaliana na ushauri wenye dalili za kuvuruga umoja wa KiTaifa - historia inaona na yeye ana watoto na wajukuu pia. Watakuja kuumizwa na matendo yake mabaya na kama ilivyo karma inaweza ikaja kuwarudia uzao wake hata kama sio yeye. Tukuze umoja na upendo wetu - tuache kubomoa umoja wa kiTaifa. Sisi wote - CCM na hata wapinzani tu wazalendo wa nchi yetu na ndiyo maana tunashindana kwa kupitia siasa za vyama vingi tukiwa hapahapa nchini. Tuache woga MBOWE sio GAIDI!
SSH tafadhali sema neon Mbowe aachiwe afanye siasa ili uzao wake, ndugu na wafuasi wake wasijenge chuki ya kimapinduzi dhidi ya CCM. Mbowe sio GAIDI!
 
Mtu yoyote anaetaka kuandaa maandamano yasio na kikomo nchi nzima ili kufanya nchi isitawalike ni sawa na gaid tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Somalia wana Utawala. Ishu sio kutawala, watawala wanatenda Raia wanavyotaka, wote tunaishi kwenye nchi moja?, huyu analipwa laki 3 anakatwa kodi..huyu analipwa zaidi ya 10 mil halipi kodi.
 
Hata Somalia wana Utawala. Ishu sio kutawala, watawala wanatenda Raia wanavyotaka, wote tunaishi kwenye nchi moja?, huyu analipwa laki 3 anakatwa kodi..huyu analipwa zaidi ya 10 mil halipi kodi.
Well said!
 
unajua Kwa nini chama kuu kimekuwa oga kiasi hicho??
Fikirini! Katika miaka 60 ya utawala huu Tanzania, ni asilimia 1.1% tu ya familia zenye baba (yaani Mkuu wa Nyumba) aliyehitimu shahada ya kwanza!! Kwa muda wa miaka 60!! Huu ni utafiti wa Benki ya Dunia!! watu milioni 60 gawanya kwa tano (ambayo ni idadi ya watu katika kaya moja) unapata kaya 12 milioni. Kaya ambazo baba ana shahada ni kaya milioni moja (1) tu!!! Kwa miaka 60!! Nyingi next zote ni chini ya hapo!! Isitoshe wakati wa Mwalimu Nyerere Literacy rate ilikuwa kama asili mia 90%. Utafiti huu wa 2018 unaonyesha asili Mia 35% hawawezi kusoma na kuandika!! Yaani tunarudi nyuma!!
Hivyo maendeleo ya mtu binafsi yanakuwa chini sana kwa kuwa wakuu wa kaya siyo wasomi!!
Hivyo chama kuu lazima kiogope wapinzani! Kwani their days are numbered!!

Siku hizi wenye vitambi barabarani ni wao tu wengine wote wamekondeana ama wanadhoofu kiakili kwa kukosa maisha bora!!

Shame on them!!
 
Hili nalo neon!
 
Back
Top Bottom