Siasa za chuki kwa Lissu kuwa Hai hazilisaidii Taifa

Siasa za chuki kwa Lissu kuwa Hai hazilisaidii Taifa

Attachments

  • download (3).jpeg
    download (3).jpeg
    6.3 KB · Views: 2
Jamii ya Ikungi iko kwenye giza totoro yani.

Alishindwa nini kuanzisha hata scheme za umwagiliaji?. Maji Ikungi ni shida, bora Mtatiro kawasaidia wapate maji.

Umaarufu wa bure kabisa.
Anaanzisha kwa pesa kutoka wapi hizo Scheme??

Mtaturu kawasaidia?? Kasaidiaje mtu ambaye ni mtumishi wao?

Utofauti wa Jimbo la Singida Mashariki na majimbo mengine ya Singida ukoje wakati wa Lissu?
 
Hayo niyale majitu yenye roho mbaya nayayofikiri hii nchi niyao peke yao.Kumbe yatakufa yataiacha.Jitu linamchukia binadamu mwenzake kwasababu zakijinga utafikiri lenyewe nilikamilifu.Yako majitu yanamdhihaki lissu kwa hali yake utafikiri yana cha maana kumbe majinga tu.Yatabaki na chuki zao uku lissu akiendelea na maisha.
 
Hapo Chadema kuna Wengi Wamekufa japo wanavaa suti na kutembea

Kifo kina maana pana yawezekana unayedhani kafa bado anaishi na kama unabisha waulize akina Halima James Mdee na wenzake Jeuri wanaitoa wapi ilhali Mahera na Ndugai wamewekwa pembeni

Kuna tofauti kubwa Kati ya Kurudi Mavumbini na " Baba mikononi mwako naiweka roho yangu"

Wahungilage!
Hii nimeipenda
 
Ingawa tunajua kwamba chuki dhidi ya Lissu inatokana zaidi na uwezo wake wa kijasiri wa kusema kile anachokiamini dhidi ya watawala, lakini pia wapo watu wanaomchukia Lissu kwa kuwa tu yupo hai hata baada ya jaribio la kutaka kumuua kufanyika.

Kuna watu kila wakimuona Lissu anatembea na kuendeleza harakati zake za kisiasa, ghafla wanapandwa na hasira na kuchefukwa na baadhi yao huanza kuporomosha matusi na laana kwa Lissu. Unashangaa ni kwa nini watu wachukie manusura aliyopata Lissu?

Ukiweka mkatale kwamba hawa watu hawakufurahia waliposikia Lissu kashambuliwa na yupo kwenye gema (Brink) la uvuli wa mauti, itashangaza sana. Wanaochukia leo hii kwa Lissu kuwa hai, ni wale walioshangilia siku aliposhambuliwa kwa risasi.

Mpaka leo bado wanajifaragua hadharani kwamba eti Lissu hakupigwa hizo risasi zinazosemwa kapigwa na tukio zima ni maigizo tu ya kuongeza umaarufu wa kisiasa kwa Lissu na CHADEMA. Na wakati mwingine husema kwamba ni Mbowe ndiye aliyetaka kumuua Lissu kwa kuwa eti Lissu anatishia uenyekiti Mbowe CHADEMA!!

Lakini pia labda chuki yao inakuja kwa kuwa mtu wao Kafa na Lissu aliyekusudiwa kuuawa ndiye yupo mitaani anadunda. ACHENI MUNGU AITWE MUNGU!!
Mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama
 
Bwana Kilewela naona siku hizi wewe nawe umeokoka. Nakumbuka kipindi wewe uko CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 wewe na kigenge chako mlikuwa mnatembea usiku mkiwa kwenye gari aina ya Mitsubishi Pajero mnaenda kung'oa bendera za chama pinzani kwenye nyumba za watu kule Iringa. Watu wakilalamika mlikuwa mnawatishia wasitoke nje huku baadhi yenu wakiwa wamepanda hadi juu ya bati wakitoa hizo bendera.

Ashukuriwe muumba kwamba malalamiko dhidi yenu yalivyofika ofisi pendwa, wakubwa wa CCM walikataza hatua zozote zisichukuliwe dhidi yenu. Kama unamkumbuka Mama Msola, alikuwa ni moja ya wagombea waliotaka sana mchukuliwe hatua kali kwa kile kitendo cha kijambazi. Mlichokifanya kipindi kile hakina utofauti wowote na Vandalism inayofanywa na CCM Ragtag vanguard UVCCM kipindi hiki.

Nafurahi kuona kwamba umekuwa mtu mwema siku hizi na kuachana na harakati za kijambazi kama zile......
 
Lissu apunguze kujiona anajua kila kitu na kuwaona wengine hawajui siasa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa sio uongo.
Siasa sio ghiliba.
Siasa sio unafiki.
Siasa sio utapeli.
Siasa ni maisha.

Kama unataka maisha yawe mazuri, basi usiwe muongo, usiwe mnafiki, usiwe tapeli, usiwe na ghiliba.

Kuna ghiliba na utapeli na kila aina ya uovu kwenye siasa za Tanzania (hasa kwenye hii kitu inaitwa maridhiano).

Kuyaongelea hayo hadharani hakumfanyi Lissu (au Mtanzania mwingine yeyote) kuonekana ni mjuaji.

Ukweli ndio utatuweka huru,kwa nini tufiche fiche mambo kama kweli tuna nia njema ya kujenga Tanzania iliyo bora kwa watu wote!!!???

Lissu endelea kusimamia ukweli.
 
Back
Top Bottom