Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Kwangu hata kama nipo CCM lakini naona bado Mbowe na wale wabunge wenye msimamo wa CHADEMA wana hoja. Tena wana hoja yenye maana kubwa tu - kumbuka hata baadhi ya viongozi wa dini wanawapiga nyundo. Kwa waliosoma Kitabu cha "An Enemy of the People" najua wanajua naeleza nini.
Kwenye conclusion ya hicho Kitabu Mwandishi Isben kama sijamkosea jina anasema "The strongest man is the one who stands alone". Naamini ikitokea Mbowe kasimama pekee yake wengi watamwelewa.
Ukweli corona imeleta mtafaruku na inaonesha watu walivyo legelege kwenye msimamo. Kuna jamaa mmoja rafiki yangu aliwahi kunidokeza ukitaka kumfahamu mtu alivyo - mpe fedha ama chakula cha kutosha na kizuri. Utamjua tu tabia yake. Akina Silinde, sijui Selasie ni hamna kitu - yaani narudia tena ni hamna kitu pale. Hao wote ni wabunge maslahi tu wala hamna kudanganyana.
Kama ilivyo kwa Dk. Gwajima wabunge hawa pia njaa inawasumbua. Kumbuka pia wanaelekea kwenye uchaguzi - kwa sasa wanadunduliza njururu za kwenda kuwawezesha kwenye kampeni. Hamna hata mbunge mmoja wa CCM au wale wa upinzani wanaoendelea kwenda bungeni wanaweza kusema Bunge la kipindi hiki limejadili kitu cha maana.
HAMNA KABISA! Kama kuna mtu anaweza kunisaidia nini cha maana kimejadiliwa na bunge hili naomba atokeze mbele aniambie.
Ukweli mtupu ni hamna kitu; na pengine Bunge hili lilitakiwa lihairishwe kwa tahadhari ya corona na mijadala ingekuwa pengine ni ya Wizara ya Fedha tu kwenye Bajeti nzima ya Serikali na sio vinginevyo.
Hapa sasa tunaona jinsi wabunge maslahi wanavyobweka - corona waiogopa lakini fedha pia wazitaka. Kinawauma nini sasa kuwasema wapinzani walivyoamua kuacha bunge, nyie si mngeendelea tu bila kuwalaumu wapinzani?
Mnawalaumu kwa sababu kimoyomoyo mnaona aibu. Aibu imewajaa sana tu. Kama sio wabunge maslahi basi wekeni azimio na posho zenu zipunguzwe zikasaidie kuleta vipimo vya corona.
Tena yule mbunge Kibajaji sijui Lusinde kwa hili hata hekima tu imekuishia. Mwogopeni Mungu nyie, msiwaone wenzenu kuwa na mkakati wa kisiasa kwa uamuzi wao, ni suala la uhai. Hivi mnafikiri corona inaua kama magonjwa mengine. Ikitokea imetokea - huponi.
Selesini hivi kweli una uhakika unwatetea WanaRombo wewe? Hivi umewasemea kitu gani sasa. Umeropoka ropoka jana - na leo nahisi upo msibani!
Ili niendelee kujipumzikia huku Shinyanga kwetu - ninamwomab Mwenyezi Mungu atusamehe sana! Unafiki umetujaa!