Siasa za Kenya ni usanii mtupu, bora TZ yetu mara 10!

Sasa napata picha unaumri gani na Tanzania unayoijuwa wewe ni ipi. Miaka sitini mwishoni pamoja na sabini, Tanzania ilikuwa na uwezo wa kujitegemea kama Kenya ilvyo kuwa, kama ni viwanda vikikuwepo, ufugaji mwingi tuu pamoja na viwanda vya maziwa na nyama. Ukulima tulilima kama kichaa cha mwendawazimu. In short kila kitu kilikuwa kinafanya kazi kama kinavyo hitajika. Idi Amini alikuwa na yake tuu, alikuwa anataka kutujaribu, sio kwasababu ya Museveni na wengine, yeye Idi Amini alijiona amesha kuwa na kajeshi kake akaona ngonja nikachokoze ugomvi, hakuja kenya kwasababu alijuwa waingereza wamewabeba mgongoni kwa kanga kama mama na mtoto wake. Na usimcheze mama akiwa analinda mwanae.

Utajiri unausema wewe ni wa mtu mmoja mmoja amabao hauwezi kuelezea hali ya nchi. Umasikini wetu sio wa milele na wala sio wa hela, sasa hivi tunachomeka waya kila moja mahali pake, soon mtambo utawaka tuu tutaelewa mjini. Sijuwi hayo ya chakula yamekujaje, ukisoma sana bila kufanya uchungizi utaenda kuamki uwongo. Ukiniambia Kenya ina njaa ntakuelewa lakini Tanzania hiyo ni ndoto tuu.
 

Ndio hilo hilo la kusomeshwa historia ya nchi bila wewe kujifanyia kautafiti na kutafuta ukweli, na hapo ndio huwa mzungu anatupiga chini. Wewe hapo naona umewafuata wenzio kwa kuaminishwa Idi Amini kichaa kilimuingia siku moja na akaamua kuteka Kagera.

Fanya utafiti wako binafsi, soma historia, tafuta taariza zisizokua na upendeleo halafu utajua kwanini mlijikuta mnapigana naye. Hauwezi ukawawalea waasi wa nchi jirani, uwavishe na kuwapa chakula na mafunzo ya kijeshi na malazi halafu utegemee hiyo nchi jarni itacheka nawe siku zote. Huo ni uchokozi uliopitiliza, eti leo hii Kenya tulee waasi dhidi ya Tanzania, tuwape mafunzo ya kijeshi na kuwaweka wawe tayari kuivamia nchi yenu halafu Magufuli awe anatuchekea bila ugomvi. Mliwalea Yoweri Museveni na wapiganaji wake, Tito Okello na wapganaji wake, David Oyite-Ojok na wapiganaji.

Umaskini wenu sio wa milele, kama ilivyo hata kwetu pia. Tunapiga hatua, kuna tofauti kubwa sana ya tulivyokua chini ya uongozi wa chama dhalimu cha tangia uhuru na tulivyo leo ambapo demokrasia imetamalaki.
 
Kwani Idi Amini anaitaji utafiti wakati ushahidi upo, yeye alitaka kujiridhisha kama yeye ni true field Marshall, na anauwezo wachukuwa chochote atakacho, kwa kifupi alikuwa anatafuta bandari kwa nguvu. Kwa uchumi tukutate mbeleni kuko, sasa hivi tunajipanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…