Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Sasa napata picha unaumri gani na Tanzania unayoijuwa wewe ni ipi. Miaka sitini mwishoni pamoja na sabini, Tanzania ilikuwa na uwezo wa kujitegemea kama Kenya ilvyo kuwa, kama ni viwanda vikikuwepo, ufugaji mwingi tuu pamoja na viwanda vya maziwa na nyama. Ukulima tulilima kama kichaa cha mwendawazimu. In short kila kitu kilikuwa kinafanya kazi kama kinavyo hitajika. Idi Amini alikuwa na yake tuu, alikuwa anataka kutujaribu, sio kwasababu ya Museveni na wengine, yeye Idi Amini alijiona amesha kuwa na kajeshi kake akaona ngonja nikachokoze ugomvi, hakuja kenya kwasababu alijuwa waingereza wamewabeba mgongoni kwa kanga kama mama na mtoto wake. Na usimcheze mama akiwa analinda mwanae.Hapo ndio huwa mnachanganya changanya, wengi mnaijadili historia ya nchi yenu kwa kutegemea mambo ya vijiweni lakini sio kwa kuisoma ilivyo. Vita dhidi ya Id Amin viltendeka juzi sana 1978. Japo nakubali ni mojawapo wa sababu za umaskini wenu.
Tatizo mlijiingiza katika kila ugomvi Afrika, mkamchokonoa Id Amin kwa kuwalea waasi wake akina Museveni. Mzungu anasema pick your fights well, sio kuingia katika kila ugomvi na vurugu kisa uonekane mbabe. Mkaiga Mrusi eti kutunisha misuli dhidi ya Muingereza na Mumarekani ilihali leo hii hao hao Waingereza na Wamarekani ndio mnawazungushia vibakuli vya misaada.
Hauwezi ukafanya experiments za hivyo huku ukitumia watu wako maskini ilhali nchi yako hujaiboresha kiuchumi. Utaishia kuwalemaza watu wako.
Halafu hilo la umaskini huwa naona mnapenda kuimba kwamba Tanzania maskini wake wanaishi kwa raha na eti sio wengi. Tatizo huwa wengi wenu hamjui na wala hamsomi taarrifa, mnaishi kwa kujidanganya na kudanganywa na wanasiasa. Fuata vizuri takwimu, na ujue kudadavua data kisayansi, leo hii
- Tanzania ina njaa zaidi ya Kenya - hili tuliwahi kulijadili huku Mataifa majirani wa Kenya wana njaa zaidi yetu
- Tanzania ina raia wengi maskini zaidi ya Kenya, kulingana na takwimu za Benki kuu ya dunia 70% ya Watanzania ni maskini wanaoishi chini ya $2
Utajiri unausema wewe ni wa mtu mmoja mmoja amabao hauwezi kuelezea hali ya nchi. Umasikini wetu sio wa milele na wala sio wa hela, sasa hivi tunachomeka waya kila moja mahali pake, soon mtambo utawaka tuu tutaelewa mjini. Sijuwi hayo ya chakula yamekujaje, ukisoma sana bila kufanya uchungizi utaenda kuamki uwongo. Ukiniambia Kenya ina njaa ntakuelewa lakini Tanzania hiyo ni ndoto tuu.