Siasa za Kenya ni za kushangaza sana

Siasa za Kenya ni za kushangaza sana

Tuajaribu kutofautisha wapiga debe ambao mara nyingi ndio hao wenye elimu ya wastani na wanasiasa kwa ajili ya mikakati ,hawa wanamikakati ndio wanaojenga chama ,na wapige debe ndio wanaotangaza chama.

Mkuu kuna tofauti kubwa hapa ,chama ni lazima kiwe na wanasiasa wapanga mikakati(strategists) ,wanasiasa ambao kazi yako kubwa ni uenezi ndio hao ambao hawaitaji kuwa na elimu kubwa kwa maana wanapokea maelezo ya nini kifanyike kwa maelekezo wa wanamikakati.Huwezi kuwa mwanamikatiti mzuri kama huna elimu dunia mkuu.
Wewe ulikuwa unamjua Shujaa Ally Mohamed Kibao?

Unamjua Mzee Nyaucho?

Wana mikakati huwa hawatajwi hovyo bwashee 😄
 
Tuajaribu kutofautisha wapiga debe ambao mara nyingi ndio hao wenye elimu ya wastani na wanasiasa kwa ajili ya mikakati ,hawa wanamikakati ndio wanaojenga chama ,na wapige debe ndio wanaotangaza chama.

Mkuu kuna tofauti kubwa hapa ,chama ni lazima kiwe na wanasiasa wapanga mikakati(strategists) ,wanasiasa ambao kazi yako kubwa ni uenezi ndio hao ambao hawaitaji kuwa na elimu kubwa kwa maana wanapokea maelezo ya nini kifanyike kwa maelekezo wa wanamikakati.Huwezi kuwa mwanamikatiti mzuri kama huna elimu dunia mkuu.
Hapo nimekupata vizuri ni kweli ni muhimu sana kwenye

kusuka mikakati na mipango nadhani kipindi kile
cha akina Wakili Masumbuko Lamwai, Wakili Mabere
Marando, Dr. Wilbroad Slaa na Prof Mwesiga Baregu
walisaidia sana upinzani kwenye mikakati.
 
Riggy G is gone.
Kitendo cha yeye Kum-acknowledge Kenyata kwamba ni undisputed King of Mount Kenya, Kitendo cha yeye kukiri kwamba Odinga was far way better than Ruto, tena kwenye recorded media, huko nyuma ya pazia inamaana kuna mengi yanaendelea.

Iyo motion ya kumuondoa Gachagua imeandaliwa na Ruto, na kuna uwezekano mkubwa sana ikafanikiwa, na itapofanikiwa, hiyo ndio ticket ya Ruto kutoka Ikulu 2027, maana waluo na wakikuyu wakicombine forces, hata afanyaje, hatoboi. Ruto anaamini 2027 atapata backup ya Raila, ila laila keshachokwa na waluo, na kwa kukubali hiyo post ya AU, waluo tayari washamuona miyeyusho.

Siasa ya Kenya iko wazi sana, predictable.
Ahaaa haaa alitamka hadharini kwamba Kenyatta ni Kingpin wa

watu mlima 😅😅🤣. Nadhani ile Limuru 3 ndio ilimueka Riggy G karibu na
Kenyatta na viongozi wengine wa Mount Kenya.

Riggy G kijana wa Nyeri kakalia kuti kavu 🤣🤣. Umechambua

Vizuri siasa za Kenya mkuu hongera sana.
 
Bora hizo watu wanapeana makavu na nchi yao ina songa ,huko hakuna uchawa si unaona makamu anamzingua rais wake na fresh . Sasa njoo Stanza uone chawa walivyojaa.
Nchi yao inasonga kwenda wapi!?..vurugu za kisiasa kila siku kabla na baada ya uchaguzi,kujilisha hawawezi
 
Siasa za Kenya kuna wakati zina shangaza sana sasa sijui ni
kusalitiana au vipi?

Bunge la Kenya linataka kumkong'oa Naibu wa Raisi wa Kenya
Rigadhi Gachagua.

Naibu Raisi huyo wa Kenya anakabiliwa na tuhuma za kuendeleza
ukabila kwa watu wa mlima Kenya pia kutokuelewana na Raisi William Ruto.
Wanaeleza kuwa ni mara kadhaa naibu wa Raisi Gachagua hajajudhuria hafla
za Raisi Ruto.

Siku za hivi karibuni pia Naibu Raisi huyo alilalamika kuondolewa
kwenye kundi la whatsapp la Raisi Ruto.

Gachagua na wandani wake wamelalamika kuwa pengine
washauri wa Raisi Ruto wana mshauri vibaya awadharua watu
wa mlima Kenya ilihali wao ndio walimpigia kura nyingi.

Nini kinakushangaza kwenye Siasa za Kenya ?
katiba yao mbovu sana 🐒
 
Mbovu tena mkuu wakati ni miongoni mwa katiba bora barani Afrika
Imeundwa 2010,
Tangu hapo Rais na Naibu wake wamewahi kuongoza Kenya bila kutofautiana na kua na uhasama? Lini?

unadhni kwa katiba yetu bora hivi hilo linaweza kutokea Tz?🐒
 
Hapo nimekupata vizuri ni kweli ni muhimu sana kwenye

kusuka mikakati na mipango nadhani kipindi kile
cha akina Wakili Masumbuko Lamwai, Wakili Mabere
Marando, Dr. Wilbroad Slaa na Prof Mwesiga Baregu
walisaidia sana upinzani kwenye mikakati.
Na ndio wakati upinzani ulikuwa juu kuliko kipindi chochote kile tangia uwepo wa siasa za ushindani
 
Mihimili ya Serikali kufanya kazi pamoja ndio tatizo linapoanzia ...

Kila mhimili unapaswa kusimama kivyake kua na sheria zake ..
 
Imeundwa 2010,
Tangu hapo Rais na Naibu wake wamewahi kuongoza Kenya bila kutofautiana na kua na uhasama? Lini?

unadhni kwa katiba yetu bora hivi hilo linaweza kutokea Tz?🐒
Kwa kweli haliwezi kutokea 🤣
 
Na ndio wakati upinzani ulikuwa juu kuliko kipindi chochote kile tangia uwepo wa siasa za ushindani
Ni kweli kipindi kile siasa za kimkakati zilikuwa vizuri sana.

Makupa nenda kamchallange Dr. Kimei Vunjo 2025 ndani ya Chama chako 🤣🤣
 
Back
Top Bottom