Siasa za Kenya ni za kushangaza sana

Hao wasomi walioko ccm wameisaidia nini Tanzania ambayo mpaka leo ni nchi maskini
 
Bora hizo watu wanapeana makavu na nchi yao ina songa ,huko hakuna uchawa si unaona makamu anamzingua rais wake na fresh . Sasa njoo Stanza uone chawa walivyojaa.
Si uliona wakati ule aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa maoni yake kuwa huku tunakoelekea tunaelekea tutatumbukia shimoni, kutokana na mikopo mikubwa ya nje tunayochukua...........

Kilichofuatia baada ya hiyo kauli ni Mkuu wa mhimili mwingine ambaye ni Rais Samia kumtumbua Spika!

Hebu jiulize , hivi katika nchi yetu kweli Ile mihimili 3 inafanya kazi ikiwa huru, au ndiyo mhimili mmoja, ambao ni Rais kuimeza mihimili mingine 2 ya Bunge na Mahakama??😳
 
Mangi kama mzee Mbowe mnasema ni tajiri huku Sugu ni biionaire wao walifanyaje hadi wakawa matajiri mkuu,au utajiri wao wameutoa kenya?Fanya kazi aisee ,achana na siasa za majitaka kama akina Lema.
Usitake kubadilisha mada kijanja Hao ccm na wasomi wote miaka zaidi ya 60+ wamesaidia nini nchi huku umaskini ukitamalaki kila kona
 
Jibu swala Mzee Mbowe na Sugu waliwezaji kuwa mabilionaire ?
Inanihusu nini mambo ya maisha yao binafsi hayanihusu
Hoja yako ya kwanza umesema chadema haina wasomi na mimi nikakuuliza swali ccm kuwa na wasomi wengi kumesaidia nini nchi maskini Tanzania

unahamisha magoli kwa kuniambia utajiri wa familia ya mbowe na sugu
Mada inahusu chadema kutokua na wasomi na ccm kuwa na wasomi wengi
 
Bunge la Kenya kipindi hiki sio imara sana kama Mahakama.

Spika wa bunge Moses Wetangula a.k.a Papa wa Roma naona

amekuwa dhaifu anaisikiliza sana serikali.
Kwamba Bunge la speaker Justin Muturi lilikua Imara, right?🀣
 
Na dada yao Waziri kafanya hivyo. Labda ndio utamaduni wao wa

kushukuru kwa namna hiyo.
 
Kwani za kwetu hazina mshangao?

Ni bora tushangae kwanza hizi za kwetu tukimaliza tuwasaidie
Kenya kushangaa za kwao.
 
En

Lilikuwa na afadhali.
katiba ya Kenya ni ya kuchochea fursa za uongozi kulingana na nguvu za kikabila na wingi wa kura za raisi....

hata wairekebishe mara3000 hapatakua na ahuweni ya mapambano ya kila moja kujipiga kifua kwamba ndie anafaa zaidi ya mwingine, kua serikalini akionyesha mchango wa kura alizochangia ndio ikaundwa serikali..

Katiba gani hiyo kwanza,
eti governor wa Jimbo anamdindia rais au makamu wa rais wazi wazi hadharani? Mtafanya kazi ya wanainchi lini sasa?πŸ’
 
Kwa kweli haliwezi kutokea 🀣
sure,
katiba mpya ya 2010 ya Kenya ni useless sana...

eti rais anaweza kupoka majukumu ya Naibu wa Rais akampatia waziri, huko si ni kuchochea vita na uhasama ndani ya serikali?πŸ’
 
Kwa hiyo mkuu wewe ni muumini wa ndio mzee kwa kila kitu

hata kama unaona sio sawa.
 
Kwa hiyo mkuu wewe ni muumini wa ndio mzee kwa kila kitu

hata kama unaona sio sawa.
Kwa katiba mbovu ya Kenya,
Mbunge moja nadhani ilikua March akawasilisha muswada binafsi wa Sheria wa kumbandua waziri wa kilimo kwasababu tu eti inasemekana aliwahi kutembea na mke wake huko nyuma 🀣
 
sure,
katiba mpya ya 2010 ya Kenya ni useless sana...

eti rais anaweza kupoka majukumu ya Naibu wa Rais akampatia waziri, huko si ni kuchochea vita na uhasama ndani ya serikali?πŸ’
Sidhani mbona huku Speaker alivuliwa uspeaker wake na

na tupo vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…