Kenya waketuacha Mbali sana sana Karne nzima kisiasa.
Wakati Kenya imeepukana na ukabila na Udini na Ukanda ambao uliwasumbua Kwa muda mrefu chini ya Katiba ya kijinga inayolea utawala wa kidikteta na uchama Dola KANU, sisi chini ya CCM ndio asubuhi kabisa watu wanaendekeza UCCM,uchadema ,uACT, ujamaa feki ,ubepari uchwara, ukabila Ukanda,Udini,ujinsia,ujana ,uprofesa ,uDr ,darasa la Saba,udigree na ujinga mwingi unaotugawa wakati Mwalimu alijitahidi kiasi Fulani kutuambia kuwa tuungane na kuwa kitu kimoja.
Kenya Chini ya Katiba Mpya ukabila unafutika Kwa Kasi ya ajabu . Anachaguliwa mtu sio Kabila au dini yake .
Tanzania Chini ya Katiba ya maslahi tuliyonayo tunalea janga baya sana linalozidi kutugawa japo wachache wanafurahia mana kwao umoja wa watanzania sio shida alimradi wapate madaraka. Rais akiwa na madaraka makubwa sana anaweza akajenga hata mfumo wa familia yake kufanya anachotaka bila kuulizwa na yeyote. Bunge limewekwa mfukoni, Mahakama pia na vyombo vya Dola. Kila taasisi ipo chini ya mtu mmoja anayeteua nafasi zote zenye maslahi makubwa.Nani asiyetaka kuwa Jaji Akatajirika haraka haraka na mbaya zaidi wanateuliwa Vijana ambao wanamatamanio Mengi hivyo wanapenda sifa na kuwa na Mali na anasa za kila aina. Nani asiyetaka vyeo vikubwa kwenye vyombo vya Dola. Nani asiyetaka Ubunge wa kupewa Kwa nguvu ya Dola. Nani anayetaka biashara zake zifilisiwe?
Akitokea Rais mwenye hulka ya Ukanda ule wa akina Museveni na Kagame akajichomeka hapa Tanzania Chini ya Katiba hii tuliyonayo tutalia na kusaga meno. Ni rahisi sana kutumia katiba hii na kuipeleka nchi unakotaka. Ukitaka kuleta Udini ni rahisi sana. Ukitaka ukabila ni rahisi sana hasa Kwa makabila makubwa kama Wamasai,wasukuma,wachaga,wanyakyusa,Wangoni, Wagogo ,Wairaki na jamii yao n.k. Ni rahisi sana. Unaweka chawa wengi halafu unateua marafiki, unateua wa mrengo unaoutaka kuanzia kwenye Dola mpaka bungeni. Anayeleta chokochoko anapewa kesi ya Ugaidi na kufilisiwa. Akienda mahakamani anakutana na Jaji aliyepewa offer ya ujaji ili ale maisha. Ukienda Polisi unakutana na wanaoahidiwa uIGP wa Mchongo .
Ukienda bungeni unakutana na wabunge wa kupewa sio kuchaguliwa. Unaamua TU uitawale nchi kibabe, kidini ,kikabila ,kikanda, kirafiki,kifisadi ,Kijamaa,kibepari n.k. utakavyoona inafaa.
Katiba Mpya ni muhimu sana. Mtu mwenye sifa Bora atapata uongozi TU kupitia Chama chochote. Huu ujinga wa katiba chakavu wa kupata viongozi wabovu Kwa kubebwa na Dola na vyama chini ya chaguzi zilizojaa rushwa inabidi tuachane nao.
Tupate Katiba mpya ili tushindanishe hoja,uwezo na maono ya mtu sio ujinga ule wa kampeni kupambwa na nyimbo za wasanii na vijembe badala ya sere ,midahalo n k.