Hapo kwenye suala la ukabila hoja yako haina mashiko. Katiba ya Kenya ya sasa haijatatua tatizo la ukabila. Ndio maana wakapendekeza mpango wa BBI (kama unajua ni nini). Hata ukifuatilia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea sasa, utagundua kwamba ukabila ndio unaendesha siasa za Kenya kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande mwingine, katiba ya sasa ya Tanzania ina misingi imara sana ya umoja wa kitaifa. Ni kweli ina mapungufu mengi na inahitaji mabadiliko makubwa, lakini ndiyo inayotufanya tusiwe na mawazo ya kikabila kwa kiwango kikubwa.
Ukabila unakumbatuwa siku zote na udikteta kama haujui Hilo. Kwenye Demokrasia ukabila unatoweka wenyewe.
Na Demokrasia ni zao la katiba Bora.
Hivi unajua Kenya ilikotoka chini ya Katiba ya Chama kushika hatamu na kila mtu kufuata Nyayo chini ya KANU?
Kwa Sasa wapo mbali sana. Uhuru Mkikuyu asingeweza kueleweka Kwa wakikuyu Kwa kumsapoti Raila Mjaluo.
Kuundwa Kwa BBI ni matokeo ya Katiba Bora ambayo Kwa kiwango kikubwa ilikubaliwa na waKenya wengi.
Tukubali Kwa Ile Kenya ya zamani Kwa Sasa imebadilika sana. Ukabila ulikua ni mbaya mana uliingia mpaka kwenye vyombo vya Dola.
Wakati wenzetu wamejitahidi kuhama Huko kwetu tunaelekea Huko na tunakwenda Kwa kusuasua Lakini ni wazi tunaelekea kwenye ukabila. Katiba inayompa Rais mamlaka makuba ni lazima iendane na ama Ukabila au Udini au Ukanda mana nguvu ya kuteua na kutengua ni lazima iendane na upande wa kutegemea Vinginevyo unaweza ukahujumiwa.
Lakini katiba iliyompunguzia mamlaka Rais inaipa mihimili mingine nguvu ya kuhimili misukiosuka ya kisheria na kisiasa.
Hivi katiba ya kifalme inampa inaendesha nchi ama kikanda au kidini au kikabila full stop. Kagame watoto wake anawapa position za juu kwenye vyombo vya Dola hakuna wa kuhoji, Museveni n.k. Lakini Katiba ya Kenya Rais hawezi kuendelea wakikuyu nakuwaacha makabila mengine, ataulizwa na hata kushtakiwa.
Hali hiyo inampa nafasi ya kusimamia haki bila kutegemea kabila Moja .
Ili utawale bila kukosolewa ni lazima uwe na nguvu ndani ya Dola yenye watu wa upande wako zaidi. Ili wengine waogope kwenda kinyume na wewe. Unaweza ukaengemea kwenye Udini ,ukabila au Ukanda.
Kuna awamu ilishambuliwa sana Kwa ukabila lakini ilifanya vile ili iwanyooshe watu. Unajipanga mpaka chini. Kila idara ili wasaliti waonekane mapema.Yote ni nguvu ya Katiba inayotoa mwanya wa kuteua kila mtu kwenye nafasi ya juu.
Ukabila unatakiwa udhibitiwe na sio eti sisi watanzania hatuna. Ukabila Kwa wananchi huku chini haupo lakini watawala wanautumia sana ili wajihakikishie kuwa wanapata kura.
Bahati mbaya wanaofanya hayo katiba inawalinda.
Angalia ishu ya Wamasai kule Ngorongoro. Woga ni ukabila unaotumika badala ya hoja. Watu wanatumia ukabila kisiasa badala ya hoja za kitaalam na za kimaendeleo.
Kenya tunajua ilipotoka na ilipo.
Watu maarufu wa makabila mengine walikua wanauawa sana ili TU Wakikuyu wasipate wapinzani ndani ya Dola. Moi aliwekwa kimkakati TU lakini Dola yote ilikua ni ya Wakikuyu. Ajira ndani ya vyombo vya Dola kipao mbele ilikua ni wakikuyu. Sasa Kenya imebadilika sana ni lazima tuwasifu. Watanzania tulikuwa pazuri lakini tunapuuza Misingi ya kuimarisha umoja ambayo ni katiba inayotambua ushindani wa haki kisiasa.
Umoja wetu ulikua wakati wa Chama kimoja na katiba yake.
Sasa Kuna vyama vingi na lengo ni kuingia madarakani unategemea Nini Kwa Watawala kama sio kutumia katiba inayowapa nguvu kuendelea kutawala na kudhibiti wapinzani wao.Hapo lazima waangalie mbinu za kudhibiti Dola. Mbinu Moja wapo ni ukabila ,Udini na Ukanda, mpaka umri Sasa ni kigezo Cha kuvuta chawa wadumu.