Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Sasa ni dhahiri kwamba kasi ya kuchafuana kwa makada wa chama cha mapinduzi Katika Jimbo la moshi mjini inazidi kushika kasi kadri siku zinavyozidi kuyoyoma kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Wapo vijana wanaoendesha harakati hizo kupitia magroup ya WhatsApp wakiwalenga makada wa CCM wanaodaiwa kuwa kwenye mpango wa kuomba kuteuliwa kuwania ubunge kwa tiketi ya ccm hapo mwakani kupitia kura za maoni .
Awali vijana hao wanadaiwa kuwa upande wa mfanyabiashara na mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline Fllling station ambako inadaiwa walikuwa walichafua viongozi akiwamo mbunge wa Sasa Jimbo la Moshi mjini(ccm),Priscus Tarimo,meya wa Manispaa ya Moshi,Zuberi Kidumo na aliyekuwa meya wa Manispaa hiyo ,Juma Raibu Juma.
Hali hiyo ilipekea baadhi ya makada waanodiwa kuwa katika mpango huo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya Chama hicho na kupewa onyo .
Hata hivyo haijawahi kudhibitika kama matendo ya kuwachafua viongozi hao nilikuwa na baraka zozote kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwani mara zote alikuwa akikana kufanya hivyo.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida vijana hao wanadiwa kumgeuka mfanyabiashara huyo na kuanza kumshambulia kwa maneno makali hatua ambayo imewaibua watu wengi na kudai vijana hao wanasunmbuliwa na njaa ya tumbo .
"Kaka nikuambie tu kwa ufupi hawa vijana wanasumbuliwa na njaa ya tumbo hakuna kitu kingine "
'Lakini hebu tujiulize hawa hawa walikuwa wanamchafua sana mheshimiwa mbunge Priscus Tarimo na mstahiki Meya Kidumo , leo wamegeuka na kuanza kumsifia,unadhani mheshimiwa Mbunge na mstahiki Meya watawaamini tena?,acha tuone lakini wanajidhalilisha sana kwa kweli".
Wengi wanahoji kulikoni vijana hawa Leo wamegeukia upande wa Priscus Tarimo na Kwa Mstahiki Meya,kuna nini,?,ni kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani ama ni kwa ajili ya tumbo?.
Baada ya vijana hao kuanza kurushq mashambulizi kwa kada huyo na mfanyabiashara ,baadhi ya watu waliokaribu nao wameanza kurusha picha za mnato zikiwaonye wakipata msosi pamoja na mfanyabiashara huyo .
Mpaka Sasa kunatajwa kuwepo makundi hasimu matatu yanayodaiwa kuwa katika harakati za kuwapigania watia nia ya ubunge .
Yetu macho ,kazi kwenu wanasiasa na siasa zenu za majitaka